MUGASHA THE HERO
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 327
- 204
Hi! jf members
Mimi ni mkazi na mzawa wa wilaya ya Mufindi katika mkoa wa Iringa jimbo la Mufindi kusini. Naandika huu uzi kwa masikitiko makubwa sana.
Kwanza tambueni kwamba jimbo la Mufindi Kusini ni miongono mwa majimbo tajiri sana, tumebalikiwa kuwa na utajiri ufuatao ambao ni fursa kubwa sana kwa wanamufindi wote na watamnzania wote:
Jambo linalokera watu wengi wa hili jimbo ni barabara ya kutoka Mafinga mpaka Mtwango kuelekea Mgololo na kutoka Mtwango mpaka Nyololo kuelekea Makambako. Hii barabara ni mbovu kupita kiasi kikubwa, gari zinazobeba karatasi, mbao, nguzo za umeme, majani ya chai zinapita katika hii barabara hii.
Kila siku tunadanganywa kwamba watajenga barabara kwa kiwango cha lami lakini hakuna kitu mpaka leo.
Huduma za kijamii ndio mbovu zaidi lakini jambo la kushangaza ni kwamba wahehe wanaoishi haya maeneo ni wabishi sana haswa pale unapowaambia kuhusu suala la mabadiliko ya kiuongozi.
Haya maeneo hutaona bendela ya ACT au CHADEMA.
Ushauri wangu kwa hii serikaLi ni kwamba wangejenga hata barabara kwa kiwango cha lami lakini sio kutoa ahadi hewa kiasi hiki.
WANAMUFINDI BADILIKENI.
(Nimeambatanisha na baadhi ya picha kutoka Mufindi)

- Kiwanda kikubwa cha karatasi mgololo (Mufindi Paper Mills/ MPM).
- Kampuni kubwa 2 za kilimo cha chai ambazo ni Unilever na Mufindi Tea Company.
- Shamba kubwa la miti ya mbao na nguzo za umeme (Sao hill).
- Kampuni ya upandaji miti (Green resources).
- Kiwanda cha utengenezaji wa nguzo za umeme (Merabu).
- Hoteli 1 ya kitalii (Fox Farm).
- Viwanda vidogo vidogo.