Kuwa Mwaminifu;- Nitajie Maksi Zako Kama Ulikuwa Unapata!

kiukweli sikua na shuka 40/50 namkumbuka sana mwl muhagama pale mnazi mmoja primary school alinijenga sana miaka iyo hadi leo nagonga namba ile mbayaaaa
 
Mimi nimeeleza ukweli uliopo, bado unalalama, Badala ya wewe kutueleza huo uongo wako katika Hisabati ulikuwaje, umetujumuisha wote ktk Upotovu wako.

Mwizi hutilia mashaka kila mtu akidhania na hao ni wevi, ila ni vema utambue na kusadiki kuwa kuna vichwa kwenye Hesabu ni vikali kupita maelezo.
 
Mimi hapo nilikuwa nadonyoaa tule twepesi twepesi miumbo mimi nilikuwa chaka.
 
ktk mazoezi sikuwahi kufika hata 20/50! necta nikakaa na mkali wa vitu nikapanga hisabati 46, lugha 40 na maarifa 49!

nikachaguliwa milambo wanaume na mshikaji tabora wav.

kuanzia milambo nikaanza kujikongoja na csee nikapata C ya namba na mengine B flat.

alev nikaenda egm nikatoka na CCD nikaingia Udsm Baed, nikatoka na GPA ya 3.7

nikaajiriwa kuwa mwalimu shule Fulani biharamulo na baadae nirudi Udsm kupiga mph, na sasa nafanya PhD huku nikiwa afisa afya wa halmashauri Fulani mkoa wa kagera.
Sawa afisa afya
 
Hahaha! Umenikumbusha mbali sana katika hicho kitu.(2008). Ilinipa umaarufu mkubwa shuleni na mitaani muda huo.

Japo kwa jumla ya masomo yote siingii kumi bora, lakini katika karatasi hilo nawaburuza wote hadi wale vichwa. {(45/50).to (50/50

Ila kitu ambacho siwezi kusahau, ni kukosa lile swali moja tu katika mtihani wa Mocko. (Swali la kutafuta namba mraba ya 56), nilikosea kuzidisha, ikasababisisha nipate 49/50. Basi hadi leo naumia sana kwa swali hili.

N.B. Nilikuwa najua na najiamini saana katika Hisabati, na maswali mawili matatu ninayokosa ni multiplication/addition/minision or addition error.
Lakini kwenye Basic Mathematics nilikuwa wa kawaida sana, japo nilionekana najua kwa sababu niliishi kwenye kundi la wasiojua!
sawa mkuu
 
Hayo makitu nilikua napiga 100 au 50/50 Mwalimu wangu aliwahi kunipa 1000 kipindi hiko ilikia pesa nyingi dah nikapeleka home mama akatoa 800 akanunua chakula ya usiku
 
Nakumbuka form 1 nshawah kupata mathematics 97% tena ulikuwa ni mtihani wa interschool nilikuwa wa kwanza haijawah kutokea tena kwangu
 
Back
Top Bottom