Kuwa Mwaminifu;- Nitajie Maksi Zako Kama Ulikuwa Unapata!

Hahaha! Umenikumbusha mbali sana katika hicho kitu.(2008). Ilinipa umaarufu mkubwa shuleni na mitaani muda huo.

Japo kwa jumla ya masomo yote siingii kumi bora, lakini katika karatasi hilo nawaburuza wote hadi wale vichwa. {(45/50).to (50/50

Ila kitu ambacho siwezi kusahau, ni kukosa lile swali moja tu katika mtihani wa Mocko. (Swali la kutafuta namba mraba ya 56), nilikosea kuzidisha, ikasababisisha nipate 49/50. Basi hadi leo naumia sana kwa swali hili.

N.B. Nilikuwa najua na najiamini saana katika Hisabati, na maswali mawili matatu ninayokosa ni multiplication/addition/minision or addition error.
Lakini kwenye Basic Mathematics nilikuwa wa kawaida sana, japo nilionekana najua kwa sababu niliishi kwenye kundi la wasiojua!
 
Ase tuache utani nlikuwa nkifaulu sana nafikisha kama 23 ivi chni ya 50.ila mara zote nlikuwa nakuwa below 20
 
Swali la kwanza mpaka la 30 nilikuwa na uwezo wa kufanya mimi mwenyewe. Lakini pale yalipokuwa yanaanza maumbo na yale mafumbo ya Umri, sijui umbali na mengineyo nilikuwa nayaangalia tu kama hakuna pa kuibia.
Hahahah poa mkuu
 
Mi nimewahipata 90 ya 100 upande wa hesabu nilipokua pre-form one St.Joseph,Kaengesa Seminary,baada ya hapo kadri nilivyokua napanda vidato,nilokuja hadi kupata 0 ya 100,R.I.P mwl. Mkinze & Itala.Lakini nilikaza kwenye masomo mengine hadi nikamaliza bila kuchujwa na wastani wao wa 50.
 
Kwa mtu aliyesoma hesabu mpaka form four na akapata japo C tu, hapo ni 48-50/50. Hakuna swali la kusumbua hapo.
 
Dah! Umenikumbusha mbali,nilikuwa naupenda sana upanda wa swali la 26-50....Huku mwanzo nilikuwa nakosea sana vikosa vidogodogo tu.
 
Back
Top Bottom