Kuwa Mwaminifu;- Nitajie Maksi Zako Kama Ulikuwa Unapata!

nyumbatatu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,076
939
IMG-20170401-WA0003.jpg
 
48/50 ikipungua si ikipungua sana haishuki 45/50. Ni somo nalolipenda sana
 
Dah! Hesabu, mathematics... Sikuwa vizuri. Kijana wangu (yupo form one kwa sasa), akitaka tugombane aje kuniuliza maswali ya hesabu, hasa hayo maumbo. Kiukweli kwa upande wangu nilikuwa napigania nisishuke chini ya hamsini tu. Ila kwenye sayansi na lugha nilihakikisha nalipa kisasi...
 
Kiukweli kabisa hapo labda nilikuwa nakosa swali 1 au mawili tena kwa errors za mwalimu Kukosea kutunga swali.
 
Nilikuwa na umbile dogo na mwenye kuvalia sshati kubwa nikikimbia linajaza upepo mpaka nashindwa kukimbia.

HISABATI ni soma nililolipenda sana nilikuwa mkali mara nyingi nilipata 100% Mwl. Wangu ilimlazimu kuniandikia 99% nilipomwuuliza hio 1% umeninyima kwa kosa lipi?

Alitabasamu na kuniambia KAZANA NIDHAMU.
Alijaribu kunilinda nisijivune, kujiganga, ama kuota Kiburi.
NA NILIFAULU VIZURI STD VII.

Na bado mpaka leo nina uwezo wa kupata alama 45 hadi 50 jap mie sio Teacher.
 
Nimewahi kupata 46/50. Sikuwa vibaya sana kwenye hesabu as sikuwahi kupata chini ya 35/50. Ila Maarifa na Lugha nilikuwa moto wa kuotea mbali sana. Mwaka 97 huo
 
Back
Top Bottom