Kuwa makini na maoni ya wajumbe JF, changanya na zako

Kwa uchache sana nataka kutoa tahadhari kwenu kuhusu ushauri unaotolewa humu Jukwaa la Mapenzi.
Wajumbe wanatoa ushauri mwingi sana, lakini uchukue kwa tahadhari huku ukichanganya na akili zako. Ukiuchukua kama ulivyo unaweza kuharibikiwa vibaya sana. Jitegemee zaidi kwenye maamuzi ya mwisho badala ya kutegemea akili za kushikiwa. Kumbuka ukiharibikiwa sisi humu tutakuwa hatupo.

Mfano humu kuna Team Kataa ndoa inakuja na hoja na tena anasema kwa hisia kali sana. Sasa wewe bro upo 40 unachukua ushauri wao kama ulivyo, kesho unapatwa na maradhi mazito huna mke wa kukutawaza makalio. Shauri yako. Lakini wewe hawa jamaa unawajua? Take dont it too serious, kuna wengine wanakukataza kuoa wao wapo na wake zao wanakulana mashine.

Mimi hapa nakataza kutoa toa hela kwa mademu. Natokwa povu kama nini, lakini nikiwa na baby wangu nakata mshiko kama nimechanganyikiwa. Nahakikisha amependeza kama wale wa Insta. Mwanamke kumchuna men ni asili. Ipo toka enzi na enzi. Sasa wewe jichanganye ufuate comment yangu bila tahadhari uone kama kuna demu utadumu naye na ubahiri wako.

Mnaelewa nachosema?
Chukua maoni yetu kwa tahadhari
Kwaiyo bro ubahili umeweka kando vp kwa yule anaechamga 100 nae anakaa kundi gn maana wote humu hawaringani life style
 
Back
Top Bottom