Si sawa Kurudia nguo bila kufua, hasa wakazi wa Maeneo yenye Joto

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,181
11,606
Na hasa nguo za ndani mfano chupi, bra, boxer, vests. Wanao kuwa jirani nawe wanapata tabu sana kwa uzito wa fukuto la hewa nzito ya kiutu uzima, isiyostahimilika kutoka maeneo mbalimbali ya mwili wako, huku ukiwa umechomekea mwenyewe. 🐒

Kumbuka mwili una hema, na vilevile mwili unapumua. Dah, ndugu yangu una kijasho kina kuchemka na kinapumua si mchezo 🐒

Kugusana ni kero zaidi, miili ina nata mno. Ni hatari kwa Afya ya ngozi.
kuchukua Tahadhari binafsi ni muhimu sana.

Na sasa kuna wale wa kukandamizia na Pafyumu ati kuficha chafu au harufu za jasho au ya mavazi yao ya jana, ndio wanaharibu zaidi. harufu ya uvundo na jasho mchanganyo wa la jana na leo plus Pafyumu, inakua kali zaidi na ya kipekee mno.

Jitahidi kua msafi wa kinywa, sehemu zote za mwili na mavazi katika kipindi hiki cha joto na fukuto kali, ili kuepuka kua kero na usumbufu kwa wengine, hususani kwenye makusanyiko na misongamano ya watu wengi, mathalani kwenye daladala, kwenye nyumba za ibada, maombi na maombezi, michezoni, mazishini na harusini n.k, harufu mbaya ni kali eti...

Imarisha unadhifu wako kwa usafi wa mwili na usafi wa mavazi katika kipindi hiki cha jojotDar.

Aidha nawapa pole kwa joto kali sana, linalokosesha wengi kua nadhifu, sina hakika kama limepungua kwa sasa🐒
 
Kale kaboksa kanavyorudiwa Sasa mpaka akikavua kanasimama...

Njoo Sasa kwa Ile jinsi ya bluu na nyeusi pale katikati Pana ukungu

Ongezea na kale kasidiria keusi kanakovaliwa hakajui maji..
 
Na hasa nguo za ndani kama mathalani undershirt, underwear, underskirt, undertrouser n.k

Wanao kua jirani nawe wanapata tabu sana kwa uzito wa fukuto la hewa nzito ya kiutu uzima, isiyostahimilika kutoka maeneo mbalimbali ya mwili wako, huku ukiwa umechomekea mwenyewe. 🐒

Kumbuka mwili una hema, na vilevile mwili unapumua. Dah, ndugu yangu una kijasho kina kuchemka na kinapumua si mchezo 🐒

Kugusana ni kero zaidi, miili ina nata mno. Ni hatari kwa Afya ya ngozi.
kuchukua Tahadhari binafsi ni muhimu sana.

Na sasa kuna wale wa kukandamizia na Pafyumu ati kuficha chafu au harufu za jasho au ya mavazi yao ya jana, ndio wanaharibu zaidi. harufu ya uvundo na jasho mchanganyo wa la jana na leo plus Pafyumu, inakua kali zaidi na ya kipekee mno.

Jitahidi kua msafi wa kinywa, sehemu zote za mwili na mavazi katika kipindi hiki cha joto na fukuto kali, ili kuepuka kua kero na usumbufu kwa wengine, hususani kwenye makusanyiko na misongamano ya watu wengi, mathalani kwenye daladala, kwenye nyumba za ibada, maombi na maombezi, michezoni, mazishini na harusini n.k, harufu mbaya ni kali eti...

Imarisha unadhifu wako kwa usafi wa mwili na usafi wa mavazi katika kipindi hiki cha jojotDar.

Aidha nawapa pole kwa joto kali sana, linalokosesha wengi kua nadhifu, sina hakika kama limepungua kwa sasa🐒
Sahivi kuna baridi
 
Jaman kuna kaka alinikuta nimekaa nimetulia sehem, aliponisongelea alivonisogelea akaanza kuniongelesha kaka anaharufu mbaya,sjui kibeberu kile sjui kijasho kidogo nitapike mpaka sa hivi nikimkumbuke nahisi kichefuchefu
 
Leo nimepishana na mtu kavaa jezi ya yanga jamani nusu nitapike harufu ni kali mno
kulala na nguo mthalani jezi au track kisha ukiamka unaduda nazo mtaani ni kazini ina matokeo mazito sana kwa wasio husika, kama ulichokutana nacho :pedroP:
 
Back
Top Bottom