Baadhi ya wanawake jaribuni kubadilika

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nisikuchoshe na usinichoshe, tusichoshane!

Kwanza kabisa nipende kuchukua nafasi hii kusema ya kwamba ujumbe huu si kwa wanawake wote bali ni baadhi ya wanawake tu.

Kumekuwa na wimbi kubwa la baadhi ya wanawake kuwa wachafu kupitiliza,leo sitazungumzia sana masuala ya mawigi na nywele hizo za kusuka zinazokaa vichwani miezi kadhaa na kusababisha kero kwa kutoa harufu kali!

Leo naomba nijikite zaidi hapa, unakuta mwanamke upo kwenye siku zako za hedhi (Menstrual Period), sasa unakuta umeondoka zako nyumbani asubuhi umeenda kwenye mapambano ya kutafuta njuruku eidha Kariakoo au Tandika(Kwa wakazi wa Dar).

Pamoja na mapambano ya kutwa nzima huku ukifahamu kabisa upo kwenye siku zako zinazohitaji usafi na uangalizi wa hali ya juu lakini wewe hujali hiyo hali. Ukishamaliza mapambano ikifika jioni utaingia na harufu yako kali kwenye usafiri wa uma iwe mwendokasi au daladala na kuwapa kero kubwa watu.

Kwasasa jiji la Dar es Salaam lina joto kali sana na ingependeza kama uko kwenye siku zako basi ukimaliza shughuli zako za utafutaji ile jioni, ingia kwenye vyoo vya uma au binafsi ukajisafishe na ujiweke kwenye mazingira ambayo hata wewe mwenyewe utayafurahia.

Nimeamua kuyaandika haya si kudharirisha utu wa mwanamke,bali ni kuwashauri na kuwaasa mama zetu,dada zetu, wachumba wetu, shangazi zetu na wake zetu ili mbadilike kwasababu mimi nawapenda sana wanawake.

Unakuta mwanamke kutwa nzima unafahamu kabisa hali yako si nzuri na inakupaswa ujisafishe kila mara,sasa kwamakusudi na dharau unakuta mwingine anapanda kwenye usafiri akiwa anatoa harufu mbaya ambayo ukiwa karibu yake lazima ugeuze shingo. Kwanini mnatufanyia hivi? Kwanini hamuoni aibu? Ina maana ile harufu nyie huwaga hamuisikii?

Hebu badilikeni, mimi nimeamua kuandika kwasababu nishakutana na hali hii na pia imekuwa kero kwa watu wengine.

Fanyeni yafuatayo mkiwa kwenye siku zenu:

1. Hakikisha kila unapotoka kwako uwe umebeba mkoba na kwenye mkoba hakikisha unazo khanga zaidi ya moja kama dharura.

2. Hakikisha kwenye mkoba umebeba pedi zaidi ya moja ili ujiwekee mazingira bora ya usafi!.

3. Hakikisha uwe na angalau nguo,chupi za kubadili pamoja na mafuta safi,pafyumu au spray pia isikose.

4. Ukimaliza kujisafisha chukua hiyo pedi chafu ifunge kwenye kanga kisha itunze kwenye mkoba ukifika kwako ichome moto, usitupe tupe hizo pedi zako ovyo kwasababu si vema kila mtu aone.

Ni aibu kubwa mwanamke mzima unajua upo kwenye siku zako halafu unatumia pedi moja kutwa nzima(Asubuhi hadi jioni)yaani ni aibu kubwa mno. Acheni hii tabia mbaya. Mwanamke ni usafi, mwanamke ni kujijali.

Mwanamke msafi anaisadifisha tabia yake ya usafi hadi kwake na mwanamke mchafu kimwili na kimuonekano hadi kwake kutakua kuchafu!

Nawapenda sana na nawaomba mbadilike.

Beesmom
Ave Mary
marapaula
Firdaus9

Hebu waambieni wenzenu wabadilike.
 
Mbaya zaidi unakuta akitembea anatoa kauvundo ukimpa salamu eti haitikii😁😁😁 ....ukimsimamisha anagoma kusimama yaani mpaka unabaki kushangaa huyu mtu ananuka uvundo sura yenyewe ya baba yake hivi anaringia nini?🤔
 
Back
Top Bottom