Kuuawa kwa majenerali wa Urusi na vita kuchukua muda mrefu ni ishara kuwa jeshi hilo halina uwezo unaosemwa

Nkobe

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
2,162
3,162
Kwa mujibu wa taarifa za ndani ni kwamba Russia ilipanga kuwa imeiteka ikulu ya Kiev ndani ya siku mbili, wapachike vibaraka wao madarakani kisha warudi nyumbani. Lakini sasa hali imekuwa tofauti kama ambavyo ulimwengu umekuwa ukiitizama nguvu ya kijeshi ya Russia.

Hadi sasa majenerali 5 wa Russia wameuawa, kuuawa kwa Jenerali wa vita ni jambo la nadra sana kwani wao ni viongozi wakuu wa vita na mara nyingi wao ukaa eneo salama huku wakitoa maelekezo, mfano mara ya mwisho kwa Marekani kupoteza kiongozi wa juu kwenye uwanja wa mapambano ilikuwa ni vita dhidi ya Vietnam mwaka 1970. Lakini hii kwa Russia imekuwa tofauti, kwa mujibu wa wataalam wa masuala ya kivita, inaonekana hali ya upambanaji ya wanajeshi wa Russia iko chini sana kiasi kwamba inalazimika kiongozi mkuu aende uwanja wa mapigano (frontline) kutoa maelekezo na kuamsha molari ya vijana wao.

Kitendo cha Majenerali hao kwenda frontline kimasababisha kuuawa kwao. Majenelari waliouawa mpaka sasa ni Andrei Sukhovetsky, Vitaly Gerasimov, Andrey Kolesnikov, Denis Glebov, Konstantin Zizevsky.

Kwa mujibu wa taarifa kitoka vyanzo mbalimbali, hizi ndizo sababu za Russia kutopiga hatua haraka ili kuiteka Kiev

1. Makadirio ya dharau kwa jeshi la Ukraine. Iko wazi kuwa serikali ya Russia uwekeza kwenye jeshi zaidi kuliko maendeleo ya watu, uwekezaji huu umeifanya Russia iingine vitani kwa kijiamini mno na kushindwa kujua uhalisia juu ya nguvu ya Kijeshi ya mpinzani wake. Ikumbukwe kuwa Ukraine ni nchi ya 12 duniani kwa kuuza vifaa vya kivita nje. Lakini ikumbukwe kuwa wakati Ukraine ikiwa sehemu ya Muungano wa kijamaa wa Kisovieti (Soviet Union), ilikuwa ikichangia uzalishaji wa silaha katika muungano huo kwa asilimia 30, lakini pia asilimia 40 ya utafiti wa kisayansi wa silaha ulifanyika Ukraine. Hivyo lilikuwa ni kosa kubwa kwa Russia kuwachukulia poa

Sababu ya pili ya Russia kushindwa kusonga mbele kwenye vita hii ni Rais Putin na wenzie kuwadanganya wanajeshi pamoja wananchi. Mpaka majeshi ya Russia yanaanza mashambulizi hawakujua hasa wanapigania nini, wao waliambiwa mnakwenda Ukraine kwa ajili ya kulinda amani, lakini kadri siku zilivyosonga walishangaa vita ikipamba moto na wanajeshi wengi kupoteza maisha. Kwa mujibu wa wanajeshi wa Russia waliosalim amri, walinukuliwa wakisema "Tuliambiwa tunakwenda Ukraine kulinda amani, tumefika huku tunaona kila mtu anakufa, imebadilika na kuwa vita kubwa"

Sababu ya tatu ni kuwa, kwa sababu ya kuikosea mahesabu Ukraine, mfumo wa Logistics wa jeshi la Russia ni mbovu. Wanajeshi wamejikuta hawapati huduma kwa wakati, ikiwepo kuletewa mafuta, chakula, maji nk hasa baada ya kukwama kwenye foleni iliyosababishwa na mashambulizi ya Ukraine. Kuna baadhi ya video zimesambaa zikionesha wanajeshi wa Russia wakiiba chakula Supermarket, jambo ambalo ni aibu.

Uwezo mdogo wa kupigana vita vya mtaani. Itakumbukwa kuwa Putin aliomba wanajeshi wa Syria wajitolee kuwasaidia, hii ni baada ya wanajeshi wa Russia kuwa na uwezo mdogo wa vita vya mtaa kwa mtaa, badala ya kupigana mtaani badala yake wamekuwa wakibomoa majengo ya raia kwa makombola ya kutoka mbali.

Sababu ya mwisho. Russia imeshindwa kulitawala anga la Ukraine kwa ndege za kivita, kuna idadi kubwa ya ndege za Russia zimedunguliwa kwa silaha za kubeba mkononi (Stinger missiles au MANPAD) kila zikiingia anga la Ukraine. Kuna duru zinasema nchi za NATO zilipenyeza vifaa vya kisasa vya kudungua ndege za kivita pamoja na vifaru. Hii imesababisha Russia kurusha makombora ambayo hayaendi kushambulia maeneo ya jeshi bali majengo ya wananchi

Mpaka sasa hakuna mji hata mmoja ambao Russia imejiahakikishia kuuteka kwa asilimia mia moja, kuna mji kama Mariupol na Kharkiv ambayo kwa muda wa wiki tatu sasa imekuwa kwa kiasi kikubwa chini ya Russia lakini bado wanapata upinzani kwa njia ya kuviziwa.

Ikumbukwe kuwa Russia ilishindwa vita na Chechnya mwaka 1996 hadi pale ambapo ilibidi wakae chini na kuweka maridhiano, Russia ilipoteza wanajeshi 5,700. Kwa mtizamo wangu, sioni hii vita kama itakwisha kirahisi kama ambavyo wengi walidhania, hii itakuwa vita ya aina yake kwani sababu zake haziko wazi, lakini pia namna ambavyo Russia wanatumia muda mrefu ndivyo ambavyo wanaruhusu NATO kupenyeza silaha, lakini pia kupeleka wanajeshi wazoefu kuisaidia Ukraine huku wakijifanya ni raia wasio na uzoefu bali wanaenda kujitolea. Wakati huohuo mbinyo wa kiuchumi ukiendelea kuwatafuna raia wa kawaida wa Russia.

NB: Kuvamia nchi hata kama ina uwezo mdogo wa kijeshi ni kazi ngumu kuliko kulinda nchi, kwani uwavamiao wako kwao na wanazijua chocho zote. Nina uhakika baada ya vita hii dunia itakuwa salama, hatutashuhudia tena nchi ikivamia nchi nyingine, najua Putin tayari anajuta na atakoma kama ambavyo USA amekoma kwa Iraq na Afghanistan.

Uchambuzi huu umetolewa na ndugu yenu Nkobe baada ya kusoma makala mbalimbali juu ya mwenendo wa vita hii
 
Ni kazi kuvamia nchi kama watu wanavofikiria mfano tosha miaka ya nyuma tanzania ilipokwenda kuipiga uganda na kupoteza wanajeshi wengi,usa ilivokwenda iraq na kupoteza wanajeshi wengi.
Unalosema ni kweli kuivamia nchi moja sio kirahisi kama watu wanavyodhani. Chukulia tu mfano vita ya pili ya dunia. Wanajeshi wengi walioenda frontline kwenye battle walikufa kama nzi. Kuna DJ mmoja wa Arusha wa kutafsiri hizi movies, anakwambia VITA SIO MAMA YAKO maana haina macho.
 
Hauna picha na hao majenerali wakiwa hai na wakiwa wamekufa? Tujiridhishe
IMG_20220318_204455_096.jpg

Hao hapo viongozi waandamizi wa jeshi la Russia walioelekea jingomeo🤔
 
Mkuu Hebu nitajie vita ambayo Marekani + NATO wamepigana kwa muda mfupi zaidi, ndipo tutathmini kama Urusi katumia Muda mrefu au ni propaganda tu.

Ili tuweze Kutathmini kama Jeshi la Urusi ni dhaifu ama siyo dhaifu basi ilibidi ulete Mfano wa Vita ambayo NATO yenye nchi karibu Thelathini imewahi kupigana kwa Muda mfupi zaidi.
 
Urusi ina historia ya kutoa kafara askari wake katika vita zote wanazopigana. Chini ya wiki 1 Nato ilikuwa tayali imeitiisha Kabul na walipoteza Askari kama 10 tu na kwa miaka yote 20 ya kuikalia Afghanistan wamepotezea askari kama 2 elfu.

Wakati Urus kwa miaka 9 ya kuikalia Afghanistan alipoteza zaid 15 elfu askari. Sijui wanashida gani ndani ya jeshi lao!!.

Uko Somalia wakati kikosi cha US kikiwa cornerd na City nzima na kila raia ana bunduki lakini walipoteza 19 askari tu. Hii ilikuwa ni Fwathaa iliyokuwa imeitishwa M, F Aidid kuyapiga majeshi ya kigen yaliyoletwa kulinda Amani.

NB: Before ya hii vita nilijua Urusi ni Mbabe wa US ila sasa picha ipo Clear kuwa nchi ya kuipiga US kijeshi haipo.
 
View attachment 2160167

Ukiangalia tu katika Map.. ukraine ni kubwA ni mara mbili ya ukubwa wa Tanzania.. sasa usidhani na kanchi kadogo kama mnavyodhani.. ni Taifa kubwa na lina nguvu pia.. kwahiyo upinzani mkubwa lazima uwepo.

kumbuka Urusi ni nchi iliyokuwa inasemwa kuwa na uwezo wa kupiga nchi 30 za Nato kwa wakati mmoja.
 
Back
Top Bottom