Kutumia Quran/ Biblia kwenye kiapo kuangaliwe upya

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,591
4,279
Nimekuwa natafakari hili jambo la kutumia Quran/Biblia kwenye kiapo naona kama halipo sawa; kwani linakosa uhalisia; hii ni kwa sababu zifuatazo;

1. Kile kinacho apiwa hakitumii sheria wala taratibu za dini husika.

2. Kuapa kwa kutumia kitabu kitakatifu na ndani ya muda mfupi mtu aende kinyume Mf: Kudanganya mahakamani ni kutenda kosa la pili kwa mwenyezi Mungu (Kudanganya).

3. Baadhi ya wanao apa hawana elimu yoyote ya dini husika zaidi ya kuitwa jina linalo endana na hiyo dini hivyo ni sawa na kudhalilisha kitabu husika.

5. Baadhi ya wanao apa wangestahili waongozwe na masheikh/wachungaji sala ya toba wamrudie kwanza Mungu kabla ya kushika kitabu kitakatifu na kuapa kitu ambacho hakifanyiki

Kwa sababu hizo, Napendekeza viapo vyote vifanywe kwa kutumia KATIBA ambayo ndiyo Sheria itakayo muhukumu muapaji pale atakapokwenda kinyume na kiapo chake.
 
Kwasababu wanaenda kutumukia wananchi na serikali siyo na dini waape kwa kushika katiba mana ndio muongozo wao.

Pia utaratibu feki wa kilaghai wa kuita viongozi wa kidini kwenye matukio ya kiserikali uachwe mara moja.
 
Aliyeleta hizi kwa nchi za Kiafrika alituweza kweli. Siamini hizi dini kabisa. Ila naamini katika mungu yupo. Naamini sana imani zetu za kuomba mungu kupitia njia za jadi. Kama matambiko na mambo mengine. Sio Gwajiboy na Mwampesa
 
Back
Top Bottom