Kutumia Dola ni kukosa hoja?

Kutumia Dola ni kukosa hoja?

Asanteni kwa hoja zenu, za kuzingatiwa nitazingatia.
Angalau nami nimeshiriki thread hii kwa kuchangia, mchango wangu huu.
P
Hivi mkuu uliposema(siyo zaidi ya mara moja), kuwa ccm itatawala milele, ulimaanisha kitu gani? Au ukimya wako ni kwasababu unajuwa ukweli?

Huwa unasema hupendi demokrasia za mabeberu kwasababu sisi tuna zetu, unapokuwa kimya hivi na kusapoti kila linaloonekana kuwa kinyume na katiba na sheria za nchi, pamoja na utawala wa kidemokrasia, tutakuelewa vipi unadhani?

Midahalo ni muhimu sana la sivyo mtu unakuwa wa ajabu ajabu tu. Mara unanuna, mara unasusa nk.
 
Tatizo letu ni kutaka viongozi mladi tu anasema atalala mbele na mafisadi basi tunahisi huyo ndo anayetufaa,,,,kiongozi ni zaidi ya kupinga mafisadi,,,kiongozi anatakiwa awe international figure sio anakuwa Local figure,,,kuna vitu vingi sana tutavikosa kiongozi akiwa na kariba ya Local figure
 
Asanteni kwa hoja zenu, za kuzingatiwa nitazingatia.
Angalau nami nimeshiriki thread hii kwa kuchangia, mchango wangu huu.
P
Paskali, ina maana huna cha kuongea kwa yaliyotea pale Hai kwenye mkutano wa Mh Mbowe ?. ina maana umechoka kutafakari au unaona hamna la ku discuss kama wadau wa siasa za KiTaifa ?.
 
Tatizo letu ni kutaka viongozi mladi tu anasema atalala mbele na mafisadi basi tunahisi huyo ndo anayetufaa,,,,kiongozi ni zaidi ya kupinga mafisadi,,,kiongozi anatakiwa awe international figure sio anakuwa Local figure,,,kuna vitu vingi sana tutavikosa kiongozi akiwa na kariba ya Local figure
Halafu Pascal Mayalla , anadai kuwa chadema ni chama cha matukio, na wakati matukio ya ufisadi ndo yalileta dhana ya “tumbua tumbua” ya “majipu” yenye usaha!🤨

Inakuwaje tunakuwa na viongozi kama rais na hatuwahi kuwasikia kwenye mdahalo? Midahalo huwa ina maswali, hawa wa ccm huwa wanasukumiziwa huko kutokana na mfumo wao mbovu kabisa. Refer to Magu mwenyewe ambaye wengi wanaamini kuingia kwake ikulu ilikuwa ni sawa na kuokota dodo bivu chini ya mnazi!

Bila mjadala huwezi kumfahamu kiongozi vyema. Especially nini haswa anachotaka kulifanyia Taifa na ni kwa njia gani atayafikia malengo yake hayo. Wananchi ndo wadau, siyo mbuzi au kondoo unaowaburuza vile utakavyo wewe.
 
Paskali, ina maana huna cha kuongea kwa yaliyotea pale Hai kwenye mkutano wa Mh Mbowe ?. ina maana umechoka kutafakari au unaona hamna la ku discuss kama wadau wa siasa za KiTaifa ?.
Kuna wanaoamini kuwa jamaa ni mkabila sana. Na hilo limesababishwa na jinsi anavyoyafumbia macho matendo maovu huku akitumia justifications za ajabu ajabu kabisa. Na pia anaona kuwa Bashite anatufaa zaidi baada ya Maghufuli kuongeza muda kwenye utawala wake. Pia anasema tatizo ni kwamba wao wasukuma wako wengi. Ukichangia na haya ya ukabila yanayoendelea, watu kama kina Pascal Mayalla wanaweza kuja kuwa “held responsible”

Watu wauwawe, wapotezwe, potelea mbali,wala hajawahi kuonyesha masikitiko dhidi ya watanzania wenzake.🤦🏾‍♂️
 
Wanajamvi, hivi kutumia dola dhidi ya wapinzani wako siyo dalili za kuishiwa na hoja kwenye taifa linalojinadi kufuata mfumo wa kidemokrasia?

Sidhani kama ni sahihi kumfananisha Trump na siasa zetu kwenye suala la matumizi ya dola. Hakuna usawa wa mifano hiyo hata chembe!

Mambo mengi ambayo yanafanywa na dola ya Tanzania dhidi ya upinzani yana ufanano gani na yale anayoyafanya Trump na serikali yake dhidi ya chama pinzani cha Democrats?

Hakuna kufanana hata kidogo, kwanza wagombea wote kuna wakati inafikia wanapewa ulinzi “secret services” ambao ndo wako specialized kwenye usalama wa viongozi hao bila ya kujali chama anachotokea.

Kikubwa kinachofanyika, ni kuwahakikishia ulinzi wakati wanamwaga sera zao kwa wananchi. Tena akitokea anayevuruga mkutano anabebwa juu juu kama karatasi na kutupwa nje. Sasa huku kwetu dola ndo inasimamia ukandamizwaji wa haki, uvunjifu wa sheria na ukiukwaji wa katiba ya nchi yetu halafu katibu mkuu wa ccm ambaye ni professor anaongea maneno kama vile ni mipasho?

Mbunge wa chama chochote cha upinzani marekani anaweza kupigwa risasi mahali popote pale iwe ndani ama nje ya marekani(achilia mbali kwenye maeneo ya bunge kama Lissu), na dola isitumike kufanya uchunguzi? Unaifananisha marekani na Tanzania kwenye utu wa kuthaminiana wenyewe kwa wenyewe? Au mkuu alizungumzia matumizi ya dola kivipi? Anajitia upofu? Ama ni ulevi wa madaraka?

Viongozi ump wanaweza kuthubutu kuzivamia studio za CNN pamoja na kuziita “fake news” kila uchwao? Yaliyotokea cloudsvideo si zipo? Hivyo ndivyo namna ya kutumia dola kubaki madarakani ama ni udikteta?

Mifano iko mingi sana! Lakini kwa kifupi kauli hiyo ya katibu mkuu wa ccm inadhihirisha ukweli kwamba serikali inayotumia dola ili iweze kubaki madarakani, basi imeishiwa na hoja za kuwashawishi watanzania kuweza kuwachagua.

Dola kazi yake kwenye demokrasia, ni kusimamia uwanja sawa wa kila upande uweze kuziwakilisha hoja zake kwa wananchi bila bughudha yoyote ile! Na siyo kutumika na chama kimoja. Hilo likitokea, tunaweza kusema ni udikteta!

Pia nashauri kuwepo na midahalo ili wananchi tuweze kujiridhisha na siyo kupachikiwa viongozi tu bila kusikia uwezo wao wa kusimamia hoja.

Rais ni nembo ya kwanza na mwakilishi wa kwanza kwa Taifa hata nje ya nchi.

Ukimpata rais ambaye hajui mdahalo, kuna uwezekano akawa katili. Ndo maana hatuoni mijadala ya bunge live ili wananchi tuwe proud kuhusu demokrasia yetu na kuona mchango wetu kwa Taifa kupitia wawakilishi wetu nk.

Tungekuwa na midahalo ya wazi na mfumo mzuri, aliyoyahoji Ben Saanane yangeshapatiwa majibu kabla ya mtu kuingia ikulu na Ben kutekwa na kupoteza maisha yake.
WAKOSA HOJA KATIKA UBORA WENGI.

WANANCHI WANATAKA SERA SIO KULIA LIA.

LIST ZITAPIGWA VIYOUNI,NYINYI MMENGANGANIA MITANDAONI?

TUONANE KWENYE DEBE!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Midahalo inapima uwezo wa kujieleza kwa kiongozi anayekusudia kuomba nafasi kubwa za uongozi,na lengo ni kujua na kutambua uwezo wa huyo kiongozi tarajiwa kwenye mambo mbalimbali ya kidunia ili ikitokea amepewa nafasi ya kuongea kwenye mikutano ya kimataifa asibabaike au kuogopa mikutano ya kimataifa.

Ni aibu kwa nchi kuwa na kiongozi parochial kwenye mambo ya kidunia maana Rais ni nembo ya Taifa akiwa empty minded ni sawa na kuwa nchi na wananchi wake ni empty minded pia

Nadhani madhumuni ya mdahalo siyo kupima uwezo wa kujieleza tu bali ufahamu wa sera za chama chake, mikakati ya kuitekeleza na upeo wake kuhusu mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
 
And the question still lingers...
 
Hivi hawa watu hawanaga washauri? Ina maana CCM wote hawana akili? Hata kama kweli intention yao ni kutumia dola je yawezekana vipi mtu timamu akalizungumza hilo katika media? SMH
Achilia mbali kuzungumzia! Nadhani vitendo vinaonekana! Halafu tunasema tuna polisi ya Tanzania?
 
Tuna utawala wa kipumbavu sana, enzi za Nyerere watawala wa namna hii aliwaita WASHENZI NA WENDAWAZIMU. Kushindwa kuwajibika kwa serikali hii katika matukio ya kifedhuli yanayoendelea nchini, inamaana TANZANIA HATUNA SERIKALI. Bali kuna GENGE TU linalotawala kihuni na kihalifu, utawala wa namna hii SASA BASI.

MITANO YA MKONO WA CHUMA, INATOSHA...
 
Tuna utawala wa kipumbavu sana, enzi za Nyerere watawala wa namna hii aliwaita WASHENZI NA WENDAWAZIMU. Kushindwa kuwajibika kwa serikali hii katika matukio ya kifedhuli yanayoendelea nchini, inamaana TANZANIA HATUNA SERIKALI. Bali kuna GENGE TU linalotawala kihuni na kihalifu, utawala wa namna hii SASA BASI.

MITANO YA MKONO WA CHUMA, INATOSHA...
Nadhani ccm inawa beep wananchi. Ni wajibu wa wananchi kupiga!(kwa sauti ya Darasa)😀
 
Nadhani madhumuni ya mdahalo siyo kupima uwezo wa kujieleza tu bali ufahamu wa sera za chama chake, mikakati ya kuitekeleza na upeo wake kuhusu mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
Well said🙏🏾 Mdahalo ni LAZIMA.
 
Mkuu niliwahi kushuhudia msafara wa huyu jamaa! Kwanza nilidhani ni kiongozi mkubwa wa serikali, kuja kuona ni yeye katibu mkuu wa ccm nilishangazwa sana. Nadhani yeye anafahamu kile kitu kinaitwa “chama kushika hatamu”, anapewa ulinzi kwa namna ambayo inaonyesha kuwa mfumo tulio nao siyo mzuri. Yeye mwenyewe nadhani anashangaa kuona anaishi kama yuko peponi na wakati kazi ya uprofesa pengine ilikuwa ngumu zaidi.

ccm haifai hata kwa kurumangia.
alikuwa mjamaa alipokuwa na njaa chuoni baada ya kushiba nae amekuwa walewale,unapinga ufisadi hali unaishi unahudumiwa kifisadi hapa tofauti ni nini sasa
 
Policeccm ndio wanawabeba,ndio mana police n traffic awamu hii wanachukua rushwa hadharani mana wanajua meko anawategemea wao kutawala

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu polisi ni genge la wahuni? Polisi ya Tanzania siyo polisi, ni genge la uhalifu! Kauli siwezi kuifuta hata niwekewe bastola kichwani!
 
Back
Top Bottom