Kutumia Dola ni kukosa hoja?

Kutumia Dola ni kukosa hoja?

Chama kilichowekwa madarakani kwa ahadi ya kuwakomboa watanzania sasa kimekuwa Chama cha wababe kinatawala kimabavu na kufikia kuuwa watanzania wanaokikosoa hata wenye kuhoji Phd ya kiongozi wanaishia kwenye Chainsaw CCM kimekosa uhalali wa kuiongoza nchi hii sasa kinatumia Polisi na vyombo vingine katika kuliteketeza taifa

Busara zimetoweka badala yake amri matamko na mizengwe ndio imekuwa sera mpya

Wakuu wa mikoa ambao hawajachaguliwa na Watanzania ndio wanapewa fimbo za kukomoa na kuwatisha wananchi

Very well said 👏🏽, kwa kuongezea, kama kungekuwepo na midahalo ya wazi na mfumo mzuri, aliyoyahoji Ben Saanane yangeshapatiwa majibu kabla ya mtu kuingia ikulu na Ben kutekwa na kupoteza maisha yake.
 
Very well said 👏🏽, kwa kuongezea, kama kungekuwepo na midahalo ya wazi na mfumo mzuri, aliyoyahoji Ben Saanane yangeshapatiwa majibu kabla ya mtu kuingia ikulu na Ben kutekwa na kupoteza maisha yake.
Na sasa hivi CCM ni kama wanasema "ukikosoa tu tunakuua au kukusagasaga kama nyama za buchani au tunakumwagia mvua ya risasi na kukubambikia kesi"
Sasa huwezi kutawala kwa njia hizi tumewahi kuona na kusoma historia inaonyesha utawala ukifikia katika hali kama hii basi ni Adios amigo.
 
Mkuu nimekusoma nakuelewa ikabididi nitoe Like yangu ndiyo chama kinatumia dola ili kutekeleza ahadi zake sasa jawa nyumbu walitaka kitumie nini kuendelea kuwepo


Sent using Jamii Forums mobile app
Acha upotoshaji, na pia siyo vyema kutumia neno nyumbu kwasababu utapigwa ban!

Tukirejea kwenye hoja, kama unaitumia dola “kutekeleza ahadi zako”, kwanini usisimame na kuyazungumzia hayo mafanikio kwa wapiga kura badala yake dola hiyo hiyo inatumika kuwakandamiza wapinzani wenye hoja mbadala?

Kwa akili yako upinzani haustahili ulinzi wa dola kwenye kumwaga sera kwa wananchi?

Au Wewe unadhani alizungumzia matumizi ya dollars Na euros?🤦🏾‍♂️
 
Na sasa hivi CCM ni kama wanasema "ukikosoa tu tunakuua au kukusagasaga kama nyama za buchani au tunakumwagia mvua ya risasi na kukubambikia kesi"
Sasa huwezi kutawala kwa njia hizi tumewahi kuona na kusoma historia inaonyesha utawala ukifikia katika hali kama hii basi ni Adios amigo.
Wameshafikia kwenye hali hiyo mkuu, na ndiyo maana katibu mkuu anatumia saikolojia ya kuwafanya wananchi waamini kwamba haya ni matendo ya kawaida kwa chama ambacho kiko madarakani, ili wayazowee matendo hayo na kuyaona ni ya kawaida...Na kwamba hata chama kingine wakiingia madarakani watafanya hivyo hivyo, yani kuitumia dola.

Ukitizama kwa undani, hakuna pahala maslahi ya mwananchi wa kawaida yamezingatiwa, cha muhimu ni madaraka tu, power, that’s it!

Hivyo basi wanachama wake na wanazi wanazidi kujiamini kwasababu si dola wako nayo? Ndiyo maana huwezi kushangazwa unapoona wanachama na viongozi waandamizi wa chama na serikali wakiwa kama miungu watu na wakatili kabisa! Wanatumia polisi wanavyotaka, na in return, polisi nao wanatumia madaraka hayo kwa manufaa binafsi wakati mwingine dhidi ya raia bila kujali chama chake! Yote ni uozo wa chama hiki ambacho kimekuwa cha kifashisti.
 
jmushi1,
Juzi nilikuwa namsoma Laurent Gbagbo wa Ivory Coast ni somo zuri sana kwa hawa watawala na Chama chao cha Kipolisi

Iko siku watakosa pa kukimbilia dunia itakuwa chungu Maafsa waandamizi wa Polisi watafikishwa mahakamani kutoa ushahidi siku hiyo ndio ulevi woote wa madaraka utakapowatoka ghafla jeuri zitawaisha

Wataenda kubanana magerezani kama sardines kwenye kopo

Nyuso zitawafubaa kama Laurent Gbagbo na wenzake.
 
imhotep,
Mkuu umegonga penyewe haswa kwenye mfano huu wa Gbagbo. Alikataa tume huru na wasimamizi wa kimataifa na UN wakayakataa matokeo yaliyompa yeye ushindi! Na mambo aliyoyafanya akiwa madarakani hayana tofauti hata chembe na haya yanayoendelea sasa nchini.
 
Wanajamvi, hivi kutumia dola dhidi ya wapinzani wako siyo dalili za kuishiwa na hoja kwenye taifa linalojinadi kufuata mfumo wa kidemokrasia?

Sidhani kama ni sahihi kumfananisha Trump na siasa zetu kwenye suala la matumizi ya dola. Hakuna usawa wa mifano hiyo hata chembe!

Mambo mengi ambayo yanafanywa na dola ya Tanzania dhidi ya upinzani yana ufanano gani na yale anayoyafanya Trump na serikali yake dhidi ya chama pinzani cha Democrats?

Hakuna kufanana hata kidogo, kwanza wagombea wote kuna wakati inafikia wanapewa ulinzi “secret services” ambao ndo wako specialized kwenye usalama wa viongozi hao bila ya kujali chama anachotokea.

Kikubwa kinachofanyika, ni kuwahakikishia ulinzi wakati wanamwaga sera zao kwa wananchi. Tena akitokea anayevuruga mkutano anabebwa juu juu kama karatasi na kutupwa nje. Sasa huku kwetu dola ndo inasimamia ukandamizwaji wa haki, uvunjifu wa sheria na ukiukwaji wa katiba ya nchi yetu halafu katibu mkuu wa ccm ambaye ni professor anaongea maneno kama vile ni mipasho?

Mbunge wa chama chochote cha upinzani marekani anaweza kupigwa risasi mahali popote pale iwe ndani ama nje ya marekani(achilia mbali kwenye maeneo ya bunge kama Lissu), na dola isitumike kufanya uchunguzi? Unaifananisha marekani na Tanzania kwenye utu wa kuthaminiana wenyewe kwa wenyewe? Au mkuu alizungumzia matumizi ya dola kivipi? Anajitia upofu? Ama ni ulevi wa madaraka?

Viongozi ump wanaweza kuthubutu kuzivamia studio za CNN pamoja na kuziita “fake news” kila uchwao? Yaliyotokea cloudsvideo si zipo? Hivyo ndivyo namna ya kutumia dola kubaki madarakani ama ni udikteta?

Mifano iko mingi sana! Lakini kwa kifupi kauli hiyo ya katibu mkuu wa ccm inadhihirisha ukweli kwamba serikali inayotumia dola ili iweze kubaki madarakani, basi imeishiwa na hoja za kuwashawishi watanzania kuweza kuwachagua.

Dola kazi yake kwenye demokrasia, ni kusimamia uwanja sawa wa kila upande uweze kuziwakilisha hoja zake kwa wananchi bila bughudha yoyote ile! Na siyo kutumika na chama kimoja. Hilo likitokea, tunaweza kusema ni udikteta!

Pia nashauri kuwepo na midahalo ili wananchi tuweze kujiridhisha na siyo kupachikiwa viongozi tu bila kusikia uwezo wao wa kusimamia hoja.

Rais ni nembo ya kwanza na mwakilishi wa kwanza kwa Taifa hata nje ya nchi.

Ukimpata rais ambaye hajui mdahalo, kuna uwezekano akawa katili. Ndo maana hatuoni mijadala ya bunge live ili wananchi tuwe proud kuhusu demokrasia yetu na kuona mchango wetu kwa Taifa kupitia wawakilishi wetu nk.

Tungekuwa na midahalo ya wazi na mfumo mzuri, aliyoyahoji Ben Saanane yangeshapatiwa majibu kabla ya mtu kuingia ikulu na Ben kutekwa na kupoteza maisha yake.
Bashiru ni profesa wa ukweli, alikuwa akifundisha UJINGA pale jalalani alikookotwa na mwezie profesa kabundi.
Wote walisomea ujinga, wanafundisha ujinga na wanaishi kijinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bashiru ni profesa wa ukweli, alikuwa akifundisha UJINGA pale jalalani alikookotwa na mwezie profesa kabundi.
Wote walisomea ujinga, wanafundisha ujinga na wanaishi kijinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
Siwezi kuwatetea hata kidogo. Nashangazwa tu na huo ujinga.
 
Ni kweli Mwl. Nyerere alikuwa katili kweli kwa sababu hakupenda midahalo na wapinzani wake ndio maana aliamua kufuta vyama vingi na kwenye nafasi ya Urais akawa anaweka kivuli kishindane naye!

Rais wa Urusi, Vladimir Putin anapenda sana midahalo lakini kama ukitaka kumjua zaidi, ingia kwenye anga zake!

Rais Kagame mpaka anapewa uwanja wa midahalo kwenye vyuo kama George Washington University lakini jaribu kuingia kwenye anga zake utapata jibu sahihi!

Hoja ya msingi ni kuwa, kupenda midahalo sio kigezo cha kiongozi kutokuwa katili na kutopenda midahalo sio kigezo cha kuonyesha kiongozi atakuwa katili!

Ni ukweli kuwa siasa za Tanzania simefungamanishwa sio na na dola pekee bali hata taasisi zingine muhimu za kijamii ndio maana unasikia kuwa Tanzania ni nchi mojawapo Afrika ambayo ina amani kwa muda mrefu.

Mwl. Nyerere aliposema, ''Rais wa Tanzania anaweza kutoka chama chochote cha siasa lakini Rais bora atatoka CCM'' alikuwa na maana pana sana kwa watu wanaojua siasa za Tanzania!
Tanzania Hakuna amani Kuna Uoga Full Stop.



Njoo Botswana uone amani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..CCM inavitumia kisiasa VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA. Hayo ndiyo malalamiko ya vyama mbadala.
Hili haliwezi kubadilika bila ya kuwa na katiba itakayotupatia mfumo mpya kabisa. Hili dubwasha linaloitwa ccm halitufai tena. Na kwa maoni yangu limeshikilia Taifa hili chini kwenye maendeleo.

Katibu mkuu yeye anataka kutumia saikolojia ili wananchi wazoee haya matendo mabaya kwa kisingizio eti wananufaika na dola kama Trump! Daah!
 
Hapa kwa kifupi umesema kwamba ccm haiwezi kuacha kutumia dola dhidi ya wapinzani wa kisiasa.

Pia nimekuelewa kwamba wapinzani watumie nguvu ya umma dhidi ya dola inapotumwa na ccm.

Huko binafsi ninaombea tusifike, kwasababu inaweza kusabanisha “civil strifes”, kwasababu ccm ni chama dola lakini si kina wanachama mtaani ambao pia wanatumika wakisaidiwa na dola? Mfano mkutano wa juzi wa Mbowe na pia Alphonce Mawazo na wengine wengi tu.
Ndiyo maana ya gharama hata ya maisha ya watu. Hao dola wasikusumbue maana hawana ubavu mbele ya nguvu ya umma yenye kudhamiria. Usisahau hata watawala wana hofu ya nguvu ya umma Ndiyo maana wanatumia vitisho.
 
Ndiyo maana ya gharama hata ya maisha ya watu. Hao dola wasikusumbue maana hawana ubavu mbele ya nguvu ya umma yenye kudhamiria. Usisahau hata watawala wana hofu ya nguvu ya umma Ndiyo maana wanatumia vitisho.
Nadhani ccm wamefikia mwisho. Chama kinapokuwa na umuhimu kuliko taifa, matokeo yake ndo haya. Kinakuwa chama cha kifashisti ambacho kimelikaba Taifa letu shingoni.
 
Back
Top Bottom