Kutumia Dola ni kukosa hoja?

Kutumia Dola ni kukosa hoja?

Hapo tatizo siyo usomi ni ushamba na ulimbukeni wa madaraka
Hao ni wasomi ambao hawajaelimika. Inawezekana wameenda Shule kukariri tu.

ccm haiendeshwi kitaalamu tena, inaongoza kimabavu. Ndiyo maana hata hao kina Bashiru, Palamagamba nk, wanaongea vitu ambavyo haviakisi usomi hata kidogo.

Kwanza ukiwa msomi ccm huwezi kutumia kipaji chako inavyotakiwa. Mfano hata uwe msomi kiasi gani, huna nguvu wala hoja kumzidi Makonda!🤦🏾‍♂️
 
Maneno aliyoyatamka katibu mkuu wa ccm ambaye na yeye kiukweli ulinzi wake ni mkubwa kupitiliza kwa maoni yangu, nadhani baada ya waziri mkuu(nimeshawahi kushuhudia msafara wake), yanaonyesha ulevi mbwa wa madaraka!
Mada yako Ni Moto unaounguza,nasikitika watu wa ajabu Kama mtu anejiita Mzee Mwanakijiji na Pascal Mayala wangekua na wao walimsikia Bashiri Ali Katibu Mkuu wa CCM alipokua akiyatamka hayo kwa kinywa chake.Lakini bahati mbaya hawakumsikia.
 
Statements za katibu wa CCM zinaonyesha ukakasi kwa demokrasia yetu!!

Ati mwenye dola atumie dola yake kujiwekea uzio wa kisiasa dhidi ya wenzake..hii hoja haikubaliki kabisa.
Hapo alikuwa anamaanisha chama chake Ccm ni chama dola.

Kitaendelea kubakia madarakani kwa msaada wa vyombo vya dola.
 
Halafu wengine wanamtetea eti tumemuelewa vibaya...msomi kama yeye anawezaje kusema vitu halafu hadhira isielewe..??
Kauli za Katibu Mkuu wa chama dola hadi ipate wakalimani ndiyo waifafanue?Tena wakalimani wake wengi ni STD VII failures.
 
Mimi ninachojua ,Bashiru alikuwa anaiongelea dola(serikali) na sio vyombo vya dola (polisi n.k). Mafanikio ya serikali ndio uhakika Wa chama chenye madaraka kuendelea kutawala kwa kuwa serikali ndio dola inayochaguliwa na watu.
Sasa na we jamaa umechemka vibaya sana.
Hiv hujui maana ya serikali? Na hiyo serikali inaundwa na organs zipi?
Unawezaje kutenganisha polisi (au vyombo vya usalama) na serikali?
 
Mada yako Ni Moto unaounguza,nasikitika watu wa ajabu Kama mtu anejiita Mzee Mwanakijiji na Pascal Mayala wangekua na wao walimsikia Bashiri Ali Katibu Mkuu wa CCM alipokua akiyatamka hayo kwa kinywa chake.Lakini bahati mbaya hawakumsikia.
Mzee Mwanakijiji pamoja na Pascal Mayalla , hata mimi kiukweli wamenishangaza sana. The latter yeye ni muumini wa ccm kutawala milele na rais kuongezewa muda! Tena yeye ana wish kwamba baada ya Maghufuli ni zamu ya Makonda!!

The former yeye ameshangaza sana kwasababu pamoja na kwamba ni mwandishi na mtu ambaye amekuwa akijinadi kwamba ni mtu mwenye kupenda mijadala ya hoja badala ya viroja, usemi ambao yeye ndiye aliyeufanya kuwa maarufu humu, ndiye sasa amekuwa champion wa viroja! Ni kweli kabisa humu JF ungekuta yeye ndo mwenye thread ya nguvu kuhusiana na haya yanayoendelea. Anaishi marekani na anafahamu umuhimu wa midahalo na uwezo wa viongozi kujenga hoja ulivyokuwa muhimu mbele ya wapiga kura! Halafu sidhani kama alishawahi hata kulaani ya member mwenzetu humu, ndugu yetu na comrade wetu Ben Saanane. Sijawahi kumsikia akipingana na ukandamizaji wa habari, uvunjwaji wa katiba na mengineyo mengi.

Kweli kuishi kwingi ni kuona mengi. Leo hii Mwanakijiji ni muumini wa ccm!!🤦🏾‍♂️
Hii ni sawa tu na kuyabugia matapishi yako ukijiaminisha ni mlo wa ukweli!
 
Pascal Mayala hawezi kuja kwa uzi huu na yule mtu Mwanakijiji.
Pascal Mayalla hawezi kuleta pua hapa. Hana hoja ya kuweza kupambana. Atakuja na hoja gani? Na wakati yeye mwenyewe yuko kwenye mission? Ni mwandishi ambaye hata ushirikiano wake na waandishi wenzake una utata. Mfano nchi za wenzetu, wana habari wanashirikiana sana inapokuja kwenye maslahi ya kazi zao, hata kama wana mitazamo ya tofauti.
 
Una uwezo mdogo wa kufikiri sawa na wafuasi wa ccm, so neno serikali linahitaji tasfida mpaka atumie neno dola? Kichwa chako kazi yake siyo kufugia nywele, kitumie vizuri kwa kazi kusudiwa
Mimi ninachojua ,Bashiru alikuwa anaiongelea dola(serikali) na sio vyombo vya dola (polisi n.k). Mafanikio ya serikali ndio uhakika Wa chama chenye madaraka kuendelea kutawala kwa kuwa serikali ndio dola inayochaguliwa na watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una uwezo mdogo wa kufikiri sawa na wafuasi wa ccm, so neno serikali linahitaji tasfida mpaka atumie neno dola? Kichwa chako kazi yake siyo kufugua nywele, kitumie vizuri kwa kazi kusudiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawana hoja na hawezi kurudi kukujibu. Huwezi kuona kina thetallest na BASIASI wakileta pua hapa maana hawana hoja. The latter ameanzisha thread yenye kumtetea katibu mkuu ina pumba kishenzi. Akija kusoma hapa hatothubutu kuchangia maana ni upupu tu.
 
Mada yako Ni Moto unaounguza,nasikitika watu wa ajabu Kama mtu anejiita Mzee Mwanakijiji na Pascal Mayala wangekua na wao walimsikia Bashiri Ali Katibu Mkuu wa CCM alipokua akiyatamka hayo kwa kinywa chake.Lakini bahati mbaya hawakumsikia.
Huwa ananikumbushia sana Pascal Mayalla , wamefanana sana uandishi nk.
Pascal Mayala hawezi kuja kwa uzi huu na yule mtu Mwanakijiji.
Mzee Mwanakijiji pamoja na Pascal Mayalla , hata mimi kiukweli wamenishangaza sana. The latter yeye ni muumini wa ccm kutawala milele na rais kuongezewa muda! Tena yeye ana wish kwamba baada ya Maghufuli ni zamu ya Makonda!!

Kweli kuishi kwingi ni kuona mengi. Leo hii Mwanakijiji ni muumini wa ccm!!🤦🏾‍♂️
Hii ni sawa tu na kuyabugia matapishi yako ukijiaminisha ni mlo wa ukweli!
Pascal Mayalla hawezi kuleta pua hapa. Hana hoja ya kuweza kupambana. Atakuja na hoja gani? Na wakati yeye mwenyewe yuko kwenye mission?
Asanteni kwa hoja zenu, za kuzingatiwa nitazingatia.
Angalau nami nimeshiriki thread hii kwa kuchangia, mchango wangu huu.
P
 
Asanteni kwa hoja zenu, za kuzingatiwa nitazingatia.
Angalau nami nimeshiriki thread hii kwa kuchangia, mchango wangu huu.
P
Asante Mkuu,lakini sijakusikia walau ukilaani tu ule uhuni aliofanyiwa mbowe hai,lakini pia Nini maoni yako Kama vijana wa CDM wangekua wamevamia mkutano wa CCM namna ile unafikiri Ni Nini kingetokea hapa chini.Tuseme tu mkutano wa Bashiri au Polepole.
Au vipi vijana wa CDM wangewashushia kipigo UVCCM wale ingekuaje?
Mkuu tunaamini wewe Ni Maandishi,Sasa muandishi hujayaona hayo? Ongeza na kauli ya Bashiru ya kujivunia mbeleko ya dola,ongeza na Mapolisi walivyokua wakimtendea Mbowe hukohuko Moshi,wewe hujasema chochote uko kimya tu.Huo ndio utawala Bora?
 
Asanteni kwa hoja zenu, za kuzingatiwa nitazingatia.
Angalau nami nimeshiriki thread hii kwa kuchangia, mchango wangu huu.
P
Mkuu Pascal Asante walau kwa kujibu tu,kitu kikubwa ulichojaaliwa na Mungu Ni heshima,huna dharau huna kisirani,huchukii.

Heshima Ni kwamba angalau umetujibu kistaarabu angekua mtu mwingine tayari tungekua tumeshakimbilia Urusi kununua S400 kwa ajili ya kizuia makombora ya majibu,Tena majibu makali kwelikweli,lakini wewe hauko Hivyo.
Lakini Mkuu tatizo lako kubwa ni moja,haujulikani wewe Kama Ni ndege au mnyama linapokuja suala la Vyama.
Wanaokulalamikia wengi saaana humu Ni CDM,wanaokusifu wengi Ni CCM.hujiulizi.hivi kweli huna macho?sio tu macho ya rohoni,namaana macho ya nyama kuona jinsi Vyama vya upinzani vinavyofanyiwa hapa Nchini kwa Sasa?hasa CDM huoni?
Kweli Katiba yetu Ni mbovu lakini je hiyo mbovu inaheshimiwa hata kwa Yale yaliyomo tu?
Kaka hivi Ni wewe kweli?
Pointi yangu Ni kuwa Kama unataka kuripoti kiuandishi Basi ripoti kwa Haki bila kupendelea upande.
 
Mada yako Ni Moto unaounguza,nasikitika watu wa ajabu Kama mtu anejiita Mzee Mwanakijiji na Pascal Mayala wangekua na wao walimsikia Bashiri Ali Katibu Mkuu wa CCM alipokua akiyatamka hayo kwa kinywa chake.Lakini bahati mbaya hawakumsikia.
Nawaonana wakifuatilia kwa makini,matamko ya Dr Bashiru yangetamkwa na minor,angekuwa Segerea via Kisutu.
 
Asanteni kwa hoja zenu, za kuzingatiwa nitazingatia.
Angalau nami nimeshiriki thread hii kwa kuchangia, mchango wangu huu.
P
Tunahitaji kusoma mawazo yako kuhusiana na hoja za Dr Bashiru,Pascal you deserves more than what you gave us.
Kauli ya Dr Bashiru ni sahihi kutolewa katika nchi ya kidemokrasia inayojigamba itaendesha uchaguzi huru,haki na Amani?
 
Wanajamvi, hivi kutumia dola dhidi ya wapinzani wako siyo dalili za kuishiwa na hoja kwenye taifa linalojinadi kufuata mfumo wa kidemokrasia?

Sidhani kama ni sahihi kumfananisha Trump na siasa zetu kwenye suala la matumizi ya dola. Hakuna usawa wa mifano hiyo hata chembe!

Mambo mengi ambayo yanafanywa na dola ya Tanzania dhidi ya upinzani yana ufanano gani na yale anayoyafanya Trump na serikali yake dhidi ya chama pinzani cha Democrats?

Hakuna kufanana hata kidogo, kwanza wagombea wote kuna wakati inafikia wanapewa ulinzi “secret services” ambao ndo wako specialized kwenye usalama wa viongozi hao bila ya kujali chama anachotokea.

Kikubwa kinachofanyika, ni kuwahakikishia ulinzi wakati wanamwaga sera zao kwa wananchi. Tena akitokea anayevuruga mkutano anabebwa juu juu kama karatasi na kutupwa nje. Sasa huku kwetu dola ndo inasimamia ukandamizwaji wa haki, uvunjifu wa sheria na ukiukwaji wa katiba ya nchi yetu halafu katibu mkuu wa ccm ambaye ni professor anaongea maneno kama vile ni mipasho?

Mbunge wa chama chochote cha upinzani marekani anaweza kupigwa risasi mahali popote pale iwe ndani ama nje ya marekani(achilia mbali kwenye maeneo ya bunge kama Lissu), na dola isitumike kufanya uchunguzi? Unaifananisha marekani na Tanzania kwenye utu wa kuthaminiana wenyewe kwa wenyewe? Au mkuu alizungumzia matumizi ya dola kivipi? Anajitia upofu? Ama ni ulevi wa madaraka?

Viongozi ump wanaweza kuthubutu kuzivamia studio za CNN pamoja na kuziita “fake news” kila uchwao? Yaliyotokea cloudsvideo si zipo? Hivyo ndivyo namna ya kutumia dola kubaki madarakani ama ni udikteta?

Mifano iko mingi sana! Lakini kwa kifupi kauli hiyo ya katibu mkuu wa ccm inadhihirisha ukweli kwamba serikali inayotumia dola ili iweze kubaki madarakani, basi imeishiwa na hoja za kuwashawishi watanzania kuweza kuwachagua.

Dola kazi yake kwenye demokrasia, ni kusimamia uwanja sawa wa kila upande uweze kuziwakilisha hoja zake kwa wananchi bila bughudha yoyote ile! Na siyo kutumika na chama kimoja. Hilo likitokea, tunaweza kusema ni udikteta!

Pia nashauri kuwepo na midahalo ili wananchi tuweze kujiridhisha na siyo kupachikiwa viongozi tu bila kusikia uwezo wao wa kusimamia hoja.

Rais ni nembo ya kwanza na mwakilishi wa kwanza kwa Taifa hata nje ya nchi.

Ukimpata rais ambaye hajui mdahalo, kuna uwezekano akawa katili. Ndo maana hatuoni mijadala ya bunge live ili wananchi tuwe proud kuhusu demokrasia yetu na kuona mchango wetu kwa Taifa kupitia wawakilishi wetu nk.

Tungekuwa na midahalo ya wazi na mfumo mzuri, aliyoyahoji Ben Saanane yangeshapatiwa majibu kabla ya mtu kuingia ikulu na Ben kutekwa na kupoteza maisha yake.
ccm ya magu,polepole na bashiru ni zaidi ya corona!
 
Back
Top Bottom