Kutoweka uzalendo kwa nchi: CCM haiwezi kuepuka lawama

Hebu elezea kidogo
ktk uzalendo nimeandika kuwa ni kuenenda ktk haki, hivyo ikiwa nchi yetu inaendeshwa ktk misingi ya kidemokrasia basi ana uhuru wa kukosoa na kuunga mkono lkn vitu hivyo viende ktk misingi ya haki na sheria.

Ukienda katika nyanja ya kiraia pia anahaki ya kukosoa na kuunga mkono hoja kwani ndie mtoa kodi,hivyo mawazo yake yanahitajika ktk kuendeleza gurudumu la maendeleo..
 
Tofauti kati ya uzalendo na utaifa ni kwamba mzalendo anajivunia nchi yake kwa kile inachokifanya, na mtaifa anajivunia nchi yake bila kujali ni nini kinachofanyika; mtazamo wa kwanza huleta hisia za uwajibikaji, wakati mtizamo wa pili, husababisha ama kuleta/kuchochea hisia za kiburi na upofu unaoweza kusababisha kuingia kwenye vita nk. Hiyo ni kwa mujibu wa quora.com.

Uzalendo unahusishwa sawa na kuwa na mapenzi ya dhati ya nchi yako na si vinginevyo. Sote tunatambuwa kuwa nchi ina consist mipaka. Na mipaka yetu sisi tuliwekewa na wakoloni. Kwahiyo uzalendo wetu unatokana na hilo(kupigania mipaka ya wakoloni/mabeberu). Hata hivyo, hilo ni la mjadala mwingine. Mjadala wa leo. Ni je wewe unasimamia nafasi gani kati ya uzalendo na utaifa?

Kutokana na tafsiri hii, ni wazi wengi wetu watakuwa wamechanganya sana kuhusina na tofauti kati ya uzalendo na utaifa.

Kuna wengi ambao ni wataifa lakini wanadhani wao ni wazalendo. Tukifahamu huo utaofauti, itatusaidia kama Taifa kwenye ujenzi wa nchi.
 
Mkuu hii kitu imeongelewa sana humu, ila nikwambie kwa hapa bongo siku hizi uzalendo ni ufia chama na wale wengine wa utaifa na wasiokipenda ni wasaliti!
 
Mkuu Hussein Melkiory , uko sahihi, kwa tafsiri iliyopo, ni sahihi kusema kuwa Professa Assad ni mzalendo? Kuhusiana na unazi wa chama, ni kweli kanisa wana ccm wanadhani kuwa mwananchama wa ccm ndo uzalendo.

Pia kwa tafsiri iliyopo, wale wanaofuata tu mkumbo kwasababu ya ushabiki wa siasa ama mapenzi kwa mtu Fulani kwasababu Fulani Fulanimfano kabila nk. Almuradi kasema flani, basi. Hilo ni utaifa na si uzalendo.

Wale wanaopedelea viongozi waabudiwe na kufananisha hayo ya kuabudu binadamu mwenzao na uzalendo, watakuwa wamekosea, wao ni wataifa!
 
UTANGULIZI
Uzalendo ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yake. Mzalendo wa kweli daima anaweka maslahi ya nchi mbele na ya kwake binafsi nyuma. Kwa maana hiyo hapo juu, mzalendo ni mtu yeyote mzawa na mwenye kuipenda na kujitoa mhanga na saa nyingine ikibidi kufa kwa ajili ya nchi yake. Uzalendo unabeba dhana nyingi sana ikianzia asili, utamaduni, lugha, siasa, historia, nk. Dhana zote zikifungwa kwenye dhana kuu ya utaifa.

SIFA ZA KUWA MZALENDO
Ili mtu aitwe mzalendo ni lazima awe na sifa hizi.

  1. Kuzaliwa nchini na angalau mzazi mmoja au wote wawili wawe ni wazawa
  2. Kuona fahari yeye kuzaliwa nchini bila kuona aibu wala haya.
  3. Ni lazima awe mwaminifu wa kulipa kodi, kutoibia nchi kwa njia yeyote.
  4. Kutokuwa mharibifu au mvujaji wa mali na rasilimali za nchi.
  5. Kuwapenda watu wote, hata viongozi wanaoijenga nchi bila kujali uchama, udini, ukabila wala rangi yake.
  6. Kuwapiga vita na kuwapinga kwa nguvu zote raia wote wanaobomoa na kuharibu nchi hata kama ni wa chama chake, dini yake, kabila lake, rangi yake au ndugu na jamaa zake.
  7. Kusaidiana na viongozi wake kuijenga nchi bila kujali uchama, udini, ukabila wala rangi yake.
  8. Kuweka juhudi kubwa katika kuisema na kuitangaza nchi yake vizuri ndani na nje ya mipaka yake.
  9. Kupenda vitu vinavyoihusu au kutoka au kutengenezwa nchini mwake kama lugha, utamaduni, vyakula, bidhaa za viwanda, timu za michezo, wana michezo wake, na kila kitu kizuri kinachotokana na nchi yake.
  10. Kuwafundisha na kuwahamasisha watu wake wa karibu kama familia, ndugu, majirani na marafiki kuwa wazalendo kwa kuipenda na kujitoa kwa ajili ya nchi yao.
MIFANO YA WAZALENDO WA KWELI
  1. Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anaweza kuwa mfano mzuri wa Mtanzania Mzalendo kwani anainguia katika sifa zote 10 hapo juu.
  2. Edward Moringe Sokoine pia anwekwa kwenye orodha ya watanzania wazalendo ambao kwa kweli waliipigania hii nchi na watu wake na rasilimali zake hata na kupoteza maisha yake,
Kuna wazalendo wengi ambao hata wewe unawajua wanaweza kuwepo kwenye orodha hii hapo juu

HITIMISHO
Kuwa mzalendo ni zaidi ya kuifia nchi yako. Kwa sababu aidha kwa uzembe au kwa ujinga au kwa imani yake mtu aweza kufa lakini kumbe hakuipenda nchi ila kwa matakwa yake binafsi. Shinikizo la kuifia nchi ni lazima liwe tunda la uaminifu, upendo kujitoa, kuipigania na kuitetea nchi yako. Wako wazalendo ambao wameitetea nchi yao toka utototni, ujanani na uzeeni na hawakuifia nchi.

Watu wasio wazalendo ni hawa hapa: watu wanaoihujumu nchi kwa kuiba, kutumia rasilimali za nchi viabaya, kuharibu miundo mbinu, kuweka pesa nje ya nchi, kuisema vibaya nchi na viongozi au watu wake, kushabikia wizi na ufisadi, kuvunja sheria za nchi, kuthamini vitu na mambo kutoka nje, nk.

Unaweza kweli ukawa Mzawa, mwaminifu, mkweli lakini unakuwa kimpya watu wanapoiba na kutumia vibaya rasilimali za nchi, wewe pia sio mzalendo kwa mfano huo.
 
Uzalendo ni kuunga mkono harakati za Jiwe
Mzalendo ni Jiwe
 
Asante kwa somo lako
Umeliongelea vizuri ila tatizo linakuja ni pale mzalendo kwetu anajulikana tofauti kabisa na ulivyoliezea kwani hakuna mafundisho hayo katika serikali nyingi duniani especially Africa

Wazungu wanaojitahidi sana na kujali wazawa kama wazalendo pia wapo wengi na hao ndio wanaopaswa kufuatwa.
UK kwa mfano, wamefundisha hili kwa sababu mfumo wao haubagui likija suala la uzalendo yaani ukizaliwa tu una haki zote bila kubaguliwa aidha unatoka Afghan au unatoka Lesotho origin.

Maadam umezaliwa hapo wewe ni mzawa na uzalendo unategemea na upendo wako wa nchi uliozaliwa
Kidogo wakenya wamefuata kanuni na sheria za Uingereza ambapo mpaka mawaziri wasomali wamejaa na kila sekta wapo na haijalishi rangi wala dini wala asili. Na huo ndio uzalendo kwani wanalitumikia taifa walilozaliwa na hawapajua mahali pengine zaidi ya hapo walipozaliwa.

Sasa sisi hilo darasa lilitupita na ndio maana akitokea mmoja aliesoma na kuingia siasa au kazi kubwa ataitwa majina ya kila aina.

Kwanini? Kwa sababu hatujafundishwa kuwa nao ni wazawa kama wewe.

Angalia USA wanajeshi weusi wamejaa na wanapigania nchi yao na haijalishi asili yake ni Guyana au Jamaica
UK mayor wa London ana asili ya Pakistan na Waziri wa mambo ya ndani ni mpakistan na ni wazawa na wazalendo haswa.

Mkubwa wa kitengo cha Scotland yard ana asili ya India sasa angalia kazi zote hizo nyeti zimeshikiliwa na hao bila kujali wana asili ya wapi.

Mkuu wa police Haringey ni mweusi pia na wengi tu
Sasa kwanza ni lazima tuwakubali watu wa aina zote kulijenga taifa bila kuwabagua la sivyo tutabaki na chuki na watu wengine wenye asili tofauti

Wengine huwa wanasema ooh hatutaki tuingiliwe maana watatuibia siri zetu what joke
Vipi hao kina Saddiq Khan?
Uzalendo hauna sura bali upendo wa nchi yako
20190510_204127.jpg
20190510_204109.jpg
 
Hebu tuwekane sawa. Hivi nchi ikiwa na viongozi ambao hawafuati katiba, waonevu wabaguzi na wa hovyohovyo na vilevile kuna wananchi humohumo wahuniwahuni na mambo yao ni hovyohovyo, nikiwasema kwa tabia zao ndiyo uzalendo umenitoka?Tuchukue mfano wa Al-Bashir wa Sudan (the ex-president) na Robert Mugabe (the former president of Zimbabwe) a few to mention.
 
UTANGULIZI
Uzalendo ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yake. Mzalendo wa kweli daima anaweka maslahi ya nchi mbele na ya kwake binafsi nyuma. Kwa maana hiyo hapo juu, mzalendo ni mtu yeyote mzawa na mwenye kuipenda na kujitoa mhanga na saa nyingine ikibidi kufa kwa ajili ya nchi yake. Uzalendo unabeba dhana nyingi sana ikianzia asili, utamaduni, lugha, siasa, historia, nk. Dhana zote zikifungwa kwenye dhana kuu ya utaifa.

SIFA ZA KUWA MZALENDO
Ili mtu aitwe mzalendo ni lazima awe na sifa hizi.

1. Kuzaliwa nchini na angalau mzazi mmoja au wote wawili wawe ni wazawa
2. Kuona fahari yeye kuzaliwa nchini bila kuona aibu wala haya
3. Ni lazima awe mwaminifu wa kulipa kodi, kutoibia nchi kwa njia yeyote.
4. Kutokuwa mharibifu au mvujaji wa mali na rasilimali za nchi
5. Kuwapenda watu wote, hata viongozi wanaoijenga nchi bila kujali uchama, udini, ukabila wala rangi yake.
6. Kuwapiga vita na kuwapinga kwa nguvu zote raia wote wanaobomoa na kuharibu nchi hata kama ni wa chama chake, dini yake, kabila lake, rangi yake au ndugu na jamaa zake.
7. Kusaidiana na viongozi wake kuijenga nchi bila kujali uchama, udini, ukabila wala rangi yake
8. Kuweka juhudi kubwa katika kuisema na kuitangaza nchi yake vizuri ndani na nje ya mipaka yake.
9. Kupenda vitu vinavyoihusu au kutoka au kutengenezwa nchini mwake kama lugha, utamaduni, vyakula, bidhaa za viwanda, timu za michezo, wana michezo wake, na kila kitu kizuri kinachotokana na nchi yake.
10. Kuwafundisha na kuwahamasisha watu wake wa karibu kama familia, ndugu, majirani na marafiki kuwa wazalendo kwa kuipenda na kujitoa kwa ajili ya nchi yao.

MIFANO YA WAZALENDO WA KWELI

11. Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anaweza kuwa mfano mzuri wa Mtanzania Mzalendo kwani anainguia katika sifa zote 10 hapo juu.
12. Edward Moringe Sokoine pia anwekwa kwenye orodha ya watanzania wazalendo ambao kwa kweli waliipigania hii nchi na watu wake na rasilimali zake hata na kupoteza maisha yake,

Kuna wazalendo wengi ambao hata wewe unawajua wanaweza kuwepo kwenye orodha hii hapo juu

HITIMISHO
Kuwa mzalendo ni zaidi ya kuifia nchi yako. Kwa sababu aidha kwa uzembe au kwa ujinga au kwa imani yake mtu aweza kufa lakini kumbe hakuipenda nchi ila kwa matakwa yake binafsi. Shinikizo la kuifia nchi ni lazima liwe tunda la uaminifu, upendo kujitoa, kuipigania na kuitetea nchi yako. Wako wazalendo ambao wameitetea nchi yao toka utototni, ujanani na uzeeni na hawakuifia nchi. Watu wasio wazalendo ni hawa hapa: watu wanaoihujumu nchi kwa kuiba, kutumia rasilimali za nchi viabaya, kuharibu miundo mbinu, kuweka pesa nje ya nchi, kuisema vibaya nchi na viongozi au watu wake, kushabikia wizi na ufisadi, kuvunja sheria za nchi, kuthamini vitu na mambo kutoka nje, nk.

Unaweza kweli ukawa Mzawa, mwaminifu, mkweli lakini unakuwa kimpya watu wanapoiba na kutumia vibaya rasilimali za nchi, wewe pia sio mzalendo kwa mfano huo.
 
Tafsiri ya wanasiasa Mzalendo ni kuwa masikini na kukubali hoja zao bila kupinga hata kama ni za hovyo...Tanzania kuwa dona kauntry ukikataa sio Mzalendo bara bara ya Chalinze imetushinda kisa kukosa mkopo na nyumba zilishabomolewa..
 
Uzalendo siku hizi ni kushabikia Serikali, Kutoipinga ama kukosoa serikali, kuwa sifu viongozi na kusema ndio kwa kila jambo hata kama unaamini haliko sawa.

Uzalendo ni kuamini You cant think and You dont know Bu the Government will think and do for You.
 
Back
Top Bottom