Kutoweka uzalendo kwa nchi: CCM haiwezi kuepuka lawama

Maana halisi ni ubaguzi dhidi ya wale wasio watanzania.

Kwa maana hiyo sitaki uzalendo.

Kwa sababu mimi Mtanzania lakini siishi Tanzania, na huku ninakoishi wakiamua kuwa "Wazalendo" na kubagua wageni, sisi Watanzania tuishio nje tutasalimika?
 
xtra,
Una mawazo mazuri sana. Nimefurahishwa na spirit yako. Hongera sana. Mungu akubariki uendelee kuwa na mawazo kama hayo.
 
MKUU Shayu!

Kila kiongozi katika CCM anaumwa saratani ya MISAADA. Nilishindwa kuamini masikio yangu siku ile Waziri wa Ujenzi Magufuli alivyo kuwa akimwambia Mkulu kwamba "ONGEZA SAFARI ZA NJE BABA KWANI NDIYO ZINAJENGA BARABARA".

Sasa ukiwa na viongozi kama hawa, ambao eti ndiyo viongozi wasomi ndani ya CCM halafu wamekosa mbinu za kugeuza fursa tulizonazo ili zilete maendeleo, inageuka kuwa JANGA.

Ni ukweli usio pingika kwamba, tumefikishwa hapa tulipo na uongozi wa CCM. wametanguliza UBINAFSI, UFISADI, KUTAFUTA MADARAKA KWA KUJIPENDEKEZA, UNAFIKI na mambo yote yanayo fanana na hayo.

Hivi inapofika kiwango cha hata waalimu kukosa chaki za kuandikia ubaoni, serikali hii itamudu kufanya kitu gani katika nchi hii? kila kiongozi amejaa uongo na ahadi zisizo tekelezwa.

Juzi sakata la Gesi, wazuri Mkuu na mawaziri wengine wanaelezea ahadi na mipango ya manufaa ya Gesi kwa wana Kusini. Muda kidogo anatoa taarifa kwamba wana Kusini wasitegemee kunufaika na Gesi katika muda mfupi ujao, hadi kati ya miaka 10 mpaka 20!!! Huyu ni kiongozi wa namna gani katika Tanganyika hii????

Na kwa vile wanajijuwa kwamba wameshindwa kazi tuliyo wapa kinacho fuata ni ubabe ndio unaotawala kwa sasa.

Hakuna njia nyingine ya kurekebisha haya zaidi ya kuiondoa CCM madarakani 2015. Kwani yeyote atakaye enda kinyume na sera zao za UFISADI huyo anakuwa ndiye adui yao mkubwa.
 
Last edited by a moderator:
Kwa maana hiyo sitaki uzalendo.

Kwa sababu mimi Mtanzania lakini siishi Tanzania, na huku ninakoishi wakiamua kuwa "Wazalendo" na kubagua wageni, sisi Watanzania tuishio nje tutasalimika?

Ndio maana uzalendo haujawahi kuwa mkakati endelevu, sababu hata hao ambao huwa wanahemuka nakuanza kuuhubiri huwa wanajua kwamba wanahubiri ubaguzi.
 
Hizi nyimbo za uzalendo chini ya maccm ni ndoto za mchana. Ndo maana hata tra wameachana na mambo ya kukusanyia kodi hazina badala yake wanakusanyia kwenye matumbo yao. Walishtuka baada ya kuona kuna watu wakiona hazina imejaa wanachanganyikiwa na kuwa wehu.

Sasa ni nani atakayeweza kurudisha uzalendo huu ni CHADEMA? Kwa sababu na uhakika unahitajika sana nchini kwetu.
 
1. walisema hawataki Serikali ile dhaifu kwa sababu Rais ana tabasamu tu. Leo hii kaja Rais mkali waliyekuwa wanamtaka wamegeuka wanamwita dikteta! Hizi ni akili au takataka? pumbavuuuuuu

2. walisema Serikali inakamata dagaa, wanataka vigogo na Mapapa wauzaji wa madawa ya kulevya watajwe hadharani. Leo hii wanatajwa hadharani na kukamatwa, wamegeuka na kusema si vizuri kuwataja hadharani ni kuwadhalilisha. Hizi ni akili au takataka?

3. walisema Serikali imejaa anasa kwa kulipana posho za hovyo hovyo na safari za nje zimezidi. Leo hii hakuna posho, semina wala safari za nje wanasema vyuma vimekaza kwa sababu hakuna dezo dezo. Hii ni akili au matope? pumbavuuuu

4. walililia marekebisho ya mikataba nyonyaji ya madini . Haya mikataba inachunguzwa, inarekebishwa wamegeuka na kuwa Watetezi wa mataifa ya nje waliokuwa wakiwalalamikia wanatunyonya kwenye madini. Hii ni akili au takataka? pumbavuuu na malofa

5. walisema si vizuri kuhama chama ili kuonyesha unamuunga mkono Rais. Leo hii anapoibuka kiongozi miongoni mwao na kumuunga mkono Rais Magufuli akiwa ndani ya vyama vyao hivyo hivyo wanamuona wa ajabu sana na kuanza kumuita msaliti, mnafki na kusahau kauli zao za awali! Hizi ni akili au takataka? Hovyoooooo

6. Walisema kuna watu waiba fedha nyingi serikalini na kuhujumu uchumi, sasa leo wanakamatwa na pengine kufilisiwa kelele zinaanza mara ooh wanaonewa hawakua peke yao, haya basi wenzao wanakamatwa kelele tena pumbavuu

unafki na uongo unafanya niwe na mashaka na uzalendo wao na nia zao kwa Taifa hatutakii kuyumbishwa na yoyote pumbavuuu

*Tuendelee kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli*

Tuendelee kukemea mambo ya hovyo hovyo ili nchi inyooke

Tusitumike na wale wenye nywele za mtelezo mwisho wa siku wao ndio wanatucheka kwa pongezi za kinafiki mara ooh thank you Mr President, you made wonderful achievement in controlling National resources, we all appreciate your positive efforts and we hope we will be good bussines partners, pumbavuuuu,

Gizani wanaanza chokochoko kwa kuwatumia weusi sana ili tuwe kama Libya,Somalia,Yemen, Qatar, Iraq na Iran God forbide. Yule wa kushoto haipendi Venezuela kabisa sasa hebu angalia Venezuela ya sasa ilivyo aaah,

Tuchague marafiki wema na wenye nia njema
Nasema sikai kimya kabisa

Comrade igwe
Januari. 12. 2018 saa kumi usiku baharini
 
Habarini wadau! Natumai mmeamka salama na kwa mlioko private sector najua wengi mnajiandaa kuwahi makazini.

Nchi hii naona imefika mahali ambako kwa hakika mambo yanaenda ndivyo sivyo kwa kisingizio cha neno uzalendo.
Nimeona tujadiliane humu ili tuwe na elimu ya uzalendo lakini hasa msingi wake ni nini?

Mimi kwa mtazamo wangu, uzalendo ni kuipenda nchi yako, kuiwakilisha, kujitanabaisha kuwa unatokea wapi pamoja na kukosoa serikali pale panapobidi ili tuweze songa mbele kimaendeleo.

Na msingi wake hasa huwa ni furaha ya nafsi katika shughuli zako za kila siku katika nchi husika kulingana na katiba ya nchi.

Je kwa kinachoendelea sasa hasa katika anga za kisiasa tunaweza kusema kuna uzalendo au watu wapo kupigania matumbo yao kupitia kukubaliana kinafiki kila kukicha na rais wa nchi?

Haiwezekani kila siku tunaambiwa tuwe wazalendo, yaani tufuate matamko ilhali kuna katiba na inapindishwa kila siku kwa makusudi ili tu kukandamiza wengine.

Katiba inaruhusu vyama vingi ila upande wa kijani kwasababu tu imeunda serikali, kazi yao ni kukandamiza upinzani na kuwaona maadui na siyi wazalendo kwa kutofautiana kimawazo.

Watu wanahoji madaraka ya bunge yako wapi siku hizi kama tu mtu anaamua tu kuchota hazina anavyojiskia na kufanya matumizi bila kutaka kuwa audited na watu wakihoji wengine watakuwa 'pyu pyu', wengine watapotea na wengine kuwekwa ndani.

Je, uzalendo hapa ni upi?
Karibu tujadiliane kwa lengo la kuelimishana.
 
Uzalendo ulienda na Nyerere, wamebaki manyang'au walimbacho si watendacho.Uzalendo unajengwa si kuimbwa.
 
Tafsir ya uzalendo kwa sasa ni kuunga mkono juhudi za serikali basi, mtu anahisi akiwa CCM hapo ndio anaunga mkono juhudi za serikali
 
Uzalendo kwa sasa ni kumuunga mhe rais mkono badala ya kuipenda nchi yako.

Ndio maana wanaohama wanasema wanamuunga rais mkono badala ya kuipenda nchi yao. Uzalendo ni kuipenda nchi yako si kumpenda rais.
 
Hii ndio maana halisi ya uzalendo.
FB_IMG_1533187404272.jpg
 
Kwasasahivi ukitaka ujue maana ya Uzalendo angalia TBC

Tunaanza kuaminishwa kuwa Uzalendo ni kusifia kila jambo na wewe unaekosoa sio mzalendo na ni adui wa Nchi. (hapa tunajenga kizazi cha hovyo sana)

Kuipenda Serikali iliyoko madarakani si Uzalendo.
Unaweza kuipenda nchi na usiipende Serikali iliyoko madarakani na unaweza Usiipende Serikali iliyoko madarakani na ukaipenda nchi.
 
Ndg wana JF naomba tuweze kueleweshana juu ya dhana hizi ambazo kwakweli yalijitokeza sana katika karne ya 17 na 18 lakini hadi leo yanaendelea na hayatakoma kamwe.

1. Dhana ya uzalendo
2. Dhana ya utaifa
3. Dhana ya Uraia

Kimsingi dhana hizi ama hazieleweki kwa wengi au zinapotoshwa kwa makusudi , sasa kama GT naomba tusaidiane kutoa mawazo na uelewa wetu juu ya hizi dhana , lengo ni kuweka recodi sawa na kueleweshana . Nawasilisha
 
Kwa kipindi hiki kumekuwepo na dhana kwamba rais wa awamu ya tano anarudisha uzalendo kwa watanzania.

Hoja hiyo imeweza kuibua makundi mawili, kundi moja linaonekana kuchukulia uzalendo kama kuunga mkono chochote anachokifanya mheshimiwa rais na serikali yake bila kujali namna inavyofanywa.

Ukienda kinyume nao wanaweza kukuita kwamba wewe siyo mzalendo au na kwamba hauipendi nchi yako. kwao hakuna utofauti kati ya kupenda nchi na kupenda serikali na viongozi wake.

Lakini kundi lingine pia wamekumbwa na jinamizi la kupinga kwa maana ya kukosoa yanayofanywa na serikali. Hawa nao wanapinga vinavyofanywa ama namna (strategies) zinazotumika kutimiza yanayofanywa.

Wao wanajitetea kwamba uzalendo ni kwa nchi "homeland" na si lazima uwe utiifu na kuunga mkono kila kitu kinachofanywa na serikali.

Tumeona pia watu fulani fulani wakifuatiliwa uraia wao katika wakati ambao wameonekana kukosoa mambo fulani fulani, kumbuka kufuatilia uraia wa watu ni kazi mojawapo ya uhamiaji ila timing ndiyo inaweza kuleta shida, je ni kwamba huenda wanaoonekana kukosoa wakasukumwa na kutokuwa raia halisi au kutokuwa wazalendo au huu ufuatiliaji wao ni coincidence tu na wala hauna muunganiko wowote na ukosoaji wao?

Katika mazingira kama haya ambapo vijana wengi wanashindwa kutofautisha dhana ya serikali, uzalendo , utaifa na uraia naomba basi pasipo kejeli wala matusi tuweze kutoa mawazo yetu na uelewa wetu juu ya dhana hizi.
 
Uzalendo,ni kuenenda ktk misingi ya haki(kutenda haki)pasipo kuweka matabaka ama kughushi kitu kwaajili ya manufaa ya mtu binafsi bali wote.

Utaifa,Ni muunganiko wa watu wenye serekali inayotambulika,mengine ni kuwa na jeshi,mipaka(eneo) n.k

Uraia,ni watu wanaoishi ktk taifa na kutambulika na serikali husika ktk namna yao.
 
KENZY,

Nini nafasi ya ukosoaji na uungaji mkono wa serikali katika dhana hizo hapo juu au hakuna uhusiano wa moja kwa moja?
 
Back
Top Bottom