Kutoka viwanja vya Karimjee, Buriani kwa Mh Regia Mtema

Josephine

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
786
812
Watu ni wengi wameanza kujitokeza,waheshimiwa wabunge,viongozi wa serikali ngazi mbalimbali,na wananchi kwa ujumla wakiungana na wanafamilia pamoja na wanachadema.

Mda si mrefu mwili wa marehemu utawasili ndani ya viwanja hivi.

Napenda kuwakaribisha nyote,zoezi hili halitachukua mda mrefu zaidi ya masaa 2.na baadae safari ya kuelekea Ifakara.

Mshumaa wetu umezima.

Kwa picha bonyeza link hii chini:

[h=3]PICHA: Yaliyojiri Karimjee katika kumuaga Regia Mtema[/h]
 
Asante sana mama yetu Josephine.Tafadhali tujulishe kila kitakachoendelea
 
Lete habari Mammy yetu!
Sisi tulioko kisogoni mwa nchi tunategemea sana posts zenuili kwa njia moja ama nyingine tushiriki msiba huu mzito wa rafiki yetu!
RIP REGIA!

rip-regia.jpg

 
Mhe. Waziri Mkuu ndo anawasili. Zitto kishawasili na viongozi wengine wamefika
 
Hakika kitachoagwa ni mwili tu lakini matendo yake yatadumu milele. kalale pema peponi mpendwa shujaa wetu REGIA MTEMA. POLENI WANA JF WENZANGU, WANA FAMILIA, WANA CHADEMA NA WATANZANIA WOTE.
 
rest in peace dada.hadi sasa wabunge wengi sana wameshawasili,viongozi wa serikali,vyama vya siasa ndugu jamaa na marafiki.makam wa rais ataongoza shughuli.wapo mawaziri wengi sana.pinda ndo anaingia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom