Maxence Melo
JF Founder
- Feb 10, 2006
- 4,230
- 13,415
Hongera kwa kuanza na hilo i.e. kukusanya madeni,.....anza na idara za serikali, maana pesa wanazo za kuwafadhili hata Brazil.................lol
...Huo si wajibu wao wa kila siku! ... Wao wangekaa na kujiuliza kwa nini watu hawalipi madeni yao halafu wafanye mpango wa kuwarahisishia kulipa. Kumkatia mtu umeme si jawabu maana unajipunguzia mapato! Naona huyu mtu mpya anaendeleza yale yale ya kuendesha shirika kibabe. Angekaa na kutueleza atafanya nini kuondoa au kupunguza kero wanazopata wateja wake badala ya kukomalia kitu ambacho hakina haja ya kampeni!
Amandla.......
Nani kasema watoe umeme bure? Au unataka kutafuta sababu tu ya kupinga fikra sahihi za Fundi Mchundo?Na kumpa mtu umeme wa bure pia hakutawaongezea mapato.
Na huwezi kudhani tu kwamba uamuzi huu ni mpango mpya wa Mkurugenzi aliyekuja mwanzoni mwa wiki.
Na huwezi kudhani tu kwamba Tanesco hawajakaa na kujiuliza ni kwa nini watu hawalipi.
Na huwezi kudhani tu kwamba watu hawalipi kwa sababu Tanesco haijawarahisishia jinsi ya kulipa.
Inawezekana wameona ni kwa sababu hawashurutishi ulipaji ikiwa ni pamoja na kusitisha hudu
Mipango mizuri sana... tatizo ni utekelezaji.
hivi yule wa nyuma hakuwahi kuwa na kampeni za kukusanya madeni?
Nani kasema watoe umeme bure?
Kumkatia mtu umeme si jawabu maana unajipunguzia mapato!
Huyu nani:
Ukitoa umeme bure ndio utaongeza mapato? Hujajibu, unalia!
Naharibu jamvi, nakufatafata. Nakunyima haki yako ya kudhaniadhania.
Ume assume TANESCO hawakuwa na mpango wa kushurutisha ulipaji ankara kabla ya ujio wa Mkurugenzi mwenye wiki, umetumia assumption kukosoa Mkurugenzi mteule.
Ume assume TANESCO hawajui kwa nini watu hawalipi ankara, umetumia assumption kukosoa mpango kazi wa kampuni. Unatumia assumption kukosoa halafu unasema una haki ya kudhani dhani bila kuambiwa dhihirisha, huna. Sasa usilie, ni hivi:
Hili ni jamvi la vina vya mahojiano. Sio Facebook hapa. Sio jamvi la Jay Dee hili, sio Michuzi. Kama Fundi Mchundo analia kwamba anaesaili alichokisema anamfatafata basi kweli jamvi limepelea, limepwaya. Na akina mimi tunaonekana tunaharibu jamvi. Mnataka palegee legee pawe nini, "Twitter" hapa?
Mjadala tuliokuwa nao kwingine sikudhani unahusiki hapa. Lakini kama unahusika basi anaeharibu ni yule aliyemwambia mwenzake akafikiri kwanza au anyamaze! Hizo ndio fikra ndefu? Kwa wenye nywele hilo ni tusi. Unasema sitafika mbali, unajuaje nilipo? Na nilipofika unajuaje ninapotaka kwenda?
Ulishasema unapoteza muda "kubishana," basi ukiona yangu yapite. Ila ukihubiri michongo imepindapinda, imejaa ma assumption pasi vina wengine watayabwia, si wote.
hivi yule wa nyuma hakuwahi kuwa na kampeni za kukusanya madeni?