Tindikali
JF-Expert Member
- Mar 26, 2010
- 2,013
- 2,663
...watu ambao baada ya kukatiwa umeme kwa kile walichoona ni uonevu wameamua kutafuta njia mbadala kama solar n.k.
Watanzania ambao bado wanahangaika kutawala nishati ya mkaa na mafuta ya taa hawana anasa ya nishati mbadala ya jua, umeishi wapi we mja? Ni mtu aliye nje ya mguso tu ndie anaweza kudai hilo. Ijue jamii ya watu unayoiongelea kabla ya kuoni njozi. Baada ya kudai kwamba kutoa umeme bure kutawaongezea TANESCO mapato unaendelea kufyatua mchemko mwingine.
Kusema kumkatia mtu umeme si jawabu hakuna maana kuwa wampe umeme bure.
Mtu halipi, hajalipa daima, unasema aendelee kupewa umeme, maana yake apewe bure!
Umedai kukatia watu umeme hakutawaongezea TANESCO mapato. Ukiwapa bure ndio utawaongezea mapato? Nani huwa anaendelea kukopesha mtu ambae halipi? Kweli hujambo we ndugu? Kampuni inapokata huduma kushurutisha ulipaji na kukosa mapato ya ankara hizo ni heri kuliko kuendelea kutoa umeme bure, itakula kwao TANESCO!
Unaweza uka assume mambo mpaka ng'ombe warudi zizini lakini huwezi kutumia assumption 1) kutoa hitimisho 2) kukosoa watu/idara. Hujafanya tafiti kujua kwamba sababu ya wateja kutolipa umeme ni makarani wa TANESCO kutopokea malipo haraka. Huwezi ku assume kwamba mteja akiendelea kulimbikizwa deni ndio atashika dini na kukimbia kulipa, hujui hilo, ni kukosoa kiholela, utapelea.
Hayo mengine ya mimi kuwa "fools," "juvenile" asiyefikiri na ushauri wa maisha sikuyapa taadhima kwa sababu nimekuachia wewe kaka.