SoC02 Kutoka si kitu hadi kuwa shujaa wa kijiji

Stories of Change - 2022 Competition

Rupia Marko D

Member
Aug 29, 2022
38
63
Jina lake anaitwa Jonathan, mtu mashuhuru ambaye kila jina lake likitajwa vichwani mwa kijiji cha Umoja kilichopo katika nchi ya Kusadikika hubaki na fikra zilizotukuka juu ya mtu huyu. Mambo makubwa aliyo yafanya katika kijiji chake ili hali tu akiwa bado ni Kijana mdogo tu katika mwishoni mwa mwaka wake wa 17 tu toka azaliwe.

KUZALIWA KWAKE
Wazazi wake Jonathan ambao walikua wakiitwa Nathaniel na Paulina, walikua hawajabahatika kupata mtoto wa kiume, ila walikua na mabinti wawili ambao ndio dada zake Jonathan mmoja akiitwa Anna na mwingine Anitha, ikiwa Anna ndio kifungua mimba na Anitha akifuatia. Ilipita miaka saba baada ya Anitha ndipo Jonathan alipozaliwa katika usiku mmoja ulioambatana na mvua kubwa yenye radi na ngurumo katika mwaka wa 1983.

AANZA KWA KUWA MKIA
Basi Jonathan alipofikisha miaka saba wazazi wake Nathaniel na Paulina walimpeleka shule ya Msingi Nguvu Moja ili kuanza masomo yake ya awali. Basi Jonathan akaanza kuhudhuria Masomo yake hayo.

Hii ilfanya matokeo ya Jonathan kuwa mabaya kuliko wanafunzi wotee kwani alikua akishika mkia darasani.

Basi siku moja wazazi wake wakaingilia kati swala hili kwa kumwambia aache kabisa kucheza na kuanza kwenda maktaba kujisomea hadithi za wanyama na vitabu mbalimbali vya jiografia na sayansi na ilimbidi kufanya hivyo kwani wazazi wake walimwambia akishindwa kufanya ivo adhabu yake itakua kunyimwa chakula.
Basi alianza kutimiza amri hii na kuanza kushinda maktaba, siku ya kwanza kuingia maktaba alishindwa achague kitabu kipi ili asome kwani alikua hajawahi kabisa kuingia maktaba, basi pembezoni mwa Shelvu alikiona kitabu ambacho kilikua kimeandikwa "mimi na rafiki zangu wanyama".

Ndani ya kitabu hiki kulikua na kila aina ya mnyama basi Jonathan alikisoma kitabu kile na kujua utamu halisi upatikanao na kusoma kwani aliweza kutambua majina mengi ya wanyama.

Basi siku moja wakiwa darasani mwalimu aliwaonyesha wanafunzi picha ya Ngiri, na kuwauliza kua yule mnyama anaitwa nani, darasa nzima lilishindwa kujibu na ndipo Jonathan alipo nyosha mkono, kwa kunyosha kwake mkono darasa nzima walicheka, kwani walitambua kua yeye hawezi kitu, ila Jonathan alijibu kwa kujiamini kuwa ile ni picha ya Ngiri. Ndipo Mwalimu akasema excellent (vizuri sana). Na ndipo darasa zima wakabaki midomo wazi kwa jibu hilo.

Toka siku hiyo Jonathan akawa kichwa na si mkia tena, akawa akiwaongozea katika kila mitihani.

NJIA YAWA NYEMBAMBA
Ingawa Jonathan alifanikiwa kufaulu kuingia elimu ya sekondari,sasa njia ya masomo yake ikageuka kuwa nyembamba, kwani ilitakiwa alipie ada na familia yake ilikua haina uwezo wa kumlipia ada.

Na mbaya zaidi katika mwaka wa 1999 ulitokea ukame mkubwa katika kijiji cha Umoja hivyo kufanya kijiji hicho kuwa na upungufu wa nafaka kiasi kwamba serikali ikileta nafaka wachache tu, nao wenye nguvu ndio walikua wakipata na serikali ya kijiji hicho kama serikali nyingine za kilaghai ilikua ikifurahia na kuitafuna Keki ya taifa.

NJIA YA MAFANIKIO YAONEKANA KWA MBALI
Kwa bahati tu Moja Kati ya walimu wa shule aliyo kua akisoma alikuwa akimpenda Anna dada yake mkubwa na mwalimu huyo alikua akimtumia Anna barua kupitia kwa Jonathan, basi mwalimu mkuu alipo wafukuza wanafunzi ambao walikua hawajalipa ada akiwemo Jonathan, Jonathan alimfuata mwalimu yule aliye kua akiitwa Nullima, na kumwambia asipo mruhusu kuingia japo maktaba kujisomea atawaambia wazazi wake kua mwalimu huyo anatoka na dada yake.

Kwa kuogopa hilo mwalimu Nullima alimruhusu Jonathan kuingia maktaba kujisomea, na Jonathan alipoingia kule alikiona kitabu kimeandikwa Modern Physics, na alipokifunua akakutana na Mada imeandikwa Electricity( Umeme). Ndani yake kukiwa na formula mbali mbali za kuvuna umeme ikiwa ni kwa njia ya Maji, Jua na Upepo.

Basi kitabu hiki kilimfungua sana akili Jonathan na hapo akapata wazo la kutengeneza mtambo wa kuvuna umeme kwa njia ya upepo, akiwa na lengo kuu la kurahisisha upatikanaji wa maji, kwani mtambo huo ungeweza kusukuma maji kutoka katika kisima kikubwa cha maji na kisha kuyasambaza mashambani ambayo yalikua tayari yamekumbwa na ukame hivyo kuikoa jamii.

UPINZANI MKUBWA TOKA KWA BABA
Basi wazo hili aliamua kulifanyia kazi na kuwambia marafiki zake ambao walikua ni Yona, Andrea na Kugta ambao wote kwa pamoja walimuunga mkono. Na vifaa vilivyokua vikihitajika ni Dinamo,Matairi Ya Baisikeli,nyaya, Nguzo za Miti, mabomba ya kusafirishia maji, Betri la gari kwa ajili ya kuwezesha mwendelezo wa kupitisha mkondo wa umeme (constant flow).

Basi Dainamo waliweza kuazima kwa Mwalimu Nullima akawapatia, mmoja kati ya wanakijiji akajitolea Betri, miti wakaikata,nyaya wakazinunua.

lakini Jonathan alipomshirikisha baba yake (Nathaniel) kuhusu jambo hili akang'aka na kuwa mkali kama pilipili, tena mchungu kuzidi Shubiri, akimwamdama kua amechukua akili za kipuuzi kutoka kwa mamaye.

NGUVU YA MAMA.
Lakini mamake Jonathan akakaa kitako na kumshauri mmewe kua bora kujaribu kuliko kuacha na wasiache mbachao hata kwa msala upitao, kwani hawawezi juu litakalo tokea, Ndipo Nathaniel alipokubali na yeye mwenyewe kuiharibu baiskeli yake na kutoa matairi na kumpa mwanae Jonathan ili ausuke mtambo wa kuvuna umeme kwa upepo.

Basi miti ile ikatengezwa vizuri na kua Nguzo, ndipo Jonathan alipo panda juu na wanakijiji kumpa yale matairi na kuyasuka vizuri, kwa pembeni aliweka Dinamo kwalengo la kuzalisha umeme pale Upepo utakapo vuma na kuendesha Tairi zile kisha kuunga nyaya zilizoenda moja kwa moja hadi kwenye betri kutoka katika betri hadi kwenye kajimashine kadogo kakusukuma maji toka kisimani hadi kwenye bomba.

Baada ya kusuka ule mtambo Jonathan akashuka chini na Upepo ulipoanza akauwasha mtambo ule. Gafla ukafanya kazi, Hapo vigelegele, miruzi pamoja na vifijo ndivyo vilivyosikika baada ya maji kuonekana na kuanza kusambazwa mashambani.

Kwa mtambo wa kuvuna umeme kwa upepo kijiji cha Umoja kilipata umeme pamoja na maji ya kutosha hivyo ukame ukatokomea kabisa. Na Jonathan akawa Shujaa na wafadhili walitokea na kumfadhili kwenda kuongeza elimu yake ugaibuni hadi akawa professa Jonathan Nathaniel.

MWISHO
Ndugu zangu uandishi huu ni wa kufikirika wenye lengo la kutusukuma vijana kuwa wabunifu pia tuwe na juhudi katika kujifunza walatini husema "Coginito, ergo sum" yaani "nakua mimi kwa vile ninavyo fikiria"- mawazo yetu hutufanya tuwe vile tunatamani tuwe.

Asanteni sana ni mimi.
Marko D Rupia.
 
Filamu yake ni mzuri pia
 

Attachments

  • The_Boy_Who_Harnessed_the_Wind.jpg
    The_Boy_Who_Harnessed_the_Wind.jpg
    11.4 KB · Views: 24
Back
Top Bottom