Mkuchika ni failure na mwoga kiongozi shupavu hawezi kutumia mabavu kuongoza,huu ni udhaifu na anatumia mabavu kuficha madudu yake.Jamani newala leo tunasaidiwa na mvua zinazonyesha vinginevyo maji ni janga la kiwilaya,barabara usiseme ni mahandaki,afya ni sufuri kabisa,elimu ndio jehanamu kabisaa na maisha bora ni ndoto hakuna uwezeshaji wala nini wananewala wanaishi kwa kudra za mwenyezi mungu tu,malipo ya pili ya korosho hayajulikani yatatoka lini,wakulima wamechoka.
Newala yote leo imeamka na kamwe asitarajie wananewala wataendelea kuogopa vitisho vyake.Huyu mzee ana kesi nyingi za kujibu kuanzia milioni 800 za bodi ya maji 2010,amechota pesa za ushuru wa korosho milioni 550 eti mchakato wa kuanzisha benki na leo anataka kula nyingine,ameifilisi NDF na hadi leo imekufa na yeye amekufa nayo kama mwenyekiti wa maisha,pesa za mfuko wa jimbo toka ulipoanza mpaka leo hazifahamiki zinafanya kazi gani,mfuko wa pembejeo ameugeuza ni wa kwake hauna manufaa kwa wananewala kwani pembejeo ni aghali na hazipatikani wakati zinapohitajika.ameihujumu Tanecu vya kutosha na ni yeye anayewafumbia macho kupe wanaoifilisi.
KITU ANACHOPASWA KUJUA MKUCHIKA NI KWAMBA HAWEZI TENA WATISHA WANANEWALA.NA hulka zake za kuwagawa ili uwatawale zimepitwa na wakati.wananewala wameamka na asidhani kama newala ni kisiwa na ataendelea kufanya kila anachotaka.wananewala wamechoka na wameamka na akilazimisha kutumia mabavu ajue anasubiriwa the hague uholanzi kwenda kujibia murder na concipiracy.
Angalizo kwa polisi wa newala msitumike kufanikisha maslahi ya mkuchika hili pia ni kwa viongozi akiwemo mkurugenzi wa halmashauli ya wilaya,mkuu wa wilaya,afisa usalama wa taifa wilaya na yeyote mwingine anaefikili kumkumbatia mkuchika ni kufanikiwa.tafadhali muacheni ashindwe kivyake msimbebe huyo habebeki.