Kutoka Newala: Mkuchika na Wana Newala....

Kutoka Newala: Mkuchika na Wana Newala....

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
19,490
Reaction score
18,386
Wakuu ndiyo naingia newala sasa, na nimefika viwanja vya mahakama ya mwanzo ambapo Mheshimiwa Mkuchika amepanga kufanya mkutano wa hadhara,
ninachokiona hapa kinanishangaza,
watu wanashangaa tu inshort wamesimama kwa mbali sana...
leo pana shida hapa!

Additional Updates;
Wakuu, kuna kitu jana kilinifurahisha wakati mkutano wa Mkuchika unaendelea...
jana jamaa walikuwa wana usalama wengi sana ambao wengi wao walivalia kiraia na wengine walijifanya vichaa..

sasa nikiwa pale mkutanoni kuna jamaa mmoja, huyu alivaa kichizi chizi, na alikuwa makini sana kunifuatilia Na nilimshtukia mapema sana kwa sababu kila nikishika simu alijitahidi sana kujua nina andika nini.. Alishindwa kwa sababu nina mzidi urefu..

Alinifuatilia kwa karibu sana, na alivyojua nimemgundua siyokichaa na nilijua anazuga, alizidisha mbwembwe za uchizi.. Mwisho wa siku huyu jamaa chizi (TISS)..

aliniomba simu apige ila nilivunga kama sijamsikia..
Basi akajidai kutaka kunipokonya ila kuna vijana pale wakamzonga na kutaka kumpiga ni kichaa asiyejulikana Newala...

kilichomsaidia ni ile hali aliyokuwa nayo ya ukichaa..Hakufanikiwa kwa lolote..
Na baada ya ule mkutano bado nilimwona kama alikuwa na interest na mimi coz alinifuata kwa nyuma..

Nilimwambia jamaa yangu kuhusu huyu mtu aliyekuwa anakuja nyuma yetu kidogo kuwa ni mwana usalama...

na tulizuga kuingia kona moja ili atufuate na tulipanga kumshika na kumkagua..sema alishtuka na hakuendelea kutufuatilia...

Ana bahati sana yule kichaa feki..jana tungemwaibisha na TISS yake.. kwa mbinu zao za kishamba kufuatilia watu...
 
wapige picha na waambie viwanda vya korosho wameua ccm na sasa gas wanauza ccm 2015 kura ccm!
 
Tuvute subira hapana shaka anaendelea kutafiti kinachojili pale.Usiunajua hapa ni mahali pa kubadilishana mawazo pevu na sahihi,japo ndugu zetu wachache wanataka kupatumia vibaya.Utafiti ni jambo moja la msingi sana kabla hujaandika neno lolote hapa jukwaani ili wenzako wachangie.Na ni vyema kupata vyanzo sahihi vingi zaidi ili kupunguza mianya ya upotoshaji.
Tunamsubiri mwenzetu,na itapendeza akija na agenda za mkutano huo na kwa namna gani wanawanchi wamezipokea kutoka kwa kiongozi wao.
 
Updates:
ki ukweli hali hapa haijakaa vizuri watu wamejawa na hofu kubwa..baadhi ya maduka yamefungwa kwa hofu!
 
nitaandika kila kinachoendelea...tatizo la network hapa newala..voda internet haipo vizuri! ila nitajitahidi kupost na kupiga picha! mpaka sasa watu ni wachache na vijana wengi wamesimama kwa mbali, mkabala wa barabara ya masasi, na s/m Luchingu...
 
ha ha ha! jamaa anatumia kipaza sauti kuwaomba watu wasogee karibu...ila hakuna mwananchi anaeinuka kusogea pale kwa mbele kabisa watu hawafiki 15. ila kwenye mzunguko wa juu barabarani vijana ni wengi sana...mgeni rasmi bado hajaingia (Mkuchika)
 
Mkuchika ndiyo anaingia na watu wanaombwa kusogea, lakini raia bado wapo mbali!! na msemaji anazidi kuomba wananchi wasogee, pia anasisitiza hakuna shida yoyote!! na sasa anakaribishwa mwenyekiti wa kitongoji Anaongea,mungu wangu! hali ishachafuka
 
Ukweli wanajamvi mkuchika hakubaliki Newala na Mtwara yote,hana jipya na kudhihilisha hilo amefanya ziara vijijini huku akiwa na ulinzi wa zaidi ya askari polisi 15,ni mbunge gani anaefanya ziara jimboni kwake na ulinzi wote huo? na cha kushangaza ameitisha halmashauli ya wilaya ya ccm na kuilazimisha itoe tamko la kuunga mkono gesi kusafirishwa kwenda Dar ilihali newala hawana maamuzi yoyote juu ya gesi wenye kutoa tamko likawa na mashiko ni kule gesi iliko yaani mtwara.

Pia baada ya kuona wilaya ya Tandahimba ina resistance kubwa na imeamka amelazimisha ushirika wa Tandahimba Newala uvunjwe ili kila wilaya ibaki na ushirika wake kinyume kabisa na sera ya ushirika nchini unaotaka kuwe na mkusanyiko mkubwa wenye kupigania maslahi ya wakulima wengi,lakini pia anatofautiana na matakwa ya mh.rais na sera ya chama chake juu ya ushirika na pia anatofautiana na wananewala.Huku huyu hakubaliki na wanainchi wamemsusa na wanasubiri muda ufike wambwage.

Huyu bwana ubabe, ubinafsi na ukubwa ndivyo vinavyomharibu pia hana mvuto wala uwezo wa kuongoza.
 
Wananchi wanazomea sana sana...wengine wanakimbia bila mpangilio..nimebaki na watu wachache, watu wamekimbia.
 
Mwenyekiti wa ccm wilaya, anaongea pumba tu, naona anamsifia tu mkuchika,
anauliza Newala hii kuna muuza nyanya gani wa 1967 alifikia hatua ya kununua pikipiki?..wahindi walikimbia newala kwa sababu wana newala wanajiweza...(uongo).
 
Wanaosumbua Newala ni wale waliokuja hapa miaka ya 1980..ambao hawaijui Newala!!
 
Back
Top Bottom