Kutoka Newala: Mkuchika na Wana Newala....

Kutoka Newala: Mkuchika na Wana Newala....

ha ha ha! jamaa anatumia kipaza sauti kuwaomba watu wasogee karibu...ila hakuna mwananchi anaeinuka kusogea pale kwa mbele kabisa watu hawafiki 15. ila kwenye mzunguko wa juu barabarani vijana ni wengi sana...mgeni rasmi bado hajaingia (Mkuchika)

Kwani wameambiwa anakuja kujilipua?
 
Wakuu ndiyo naingia newala sasa, na nimefika viwanja vya mahakama ya mwanzo ambapo Mheshimiwa Mkuchika amepanga kufanya mkutano wa hadhara,
ninachokiona hapa kinanishangaza, watu wanashangaa tu inshort wamesimama kwa mbali sana...leo pana shida hapa!

Vipi kale ka video ka Lwakatare kuhujumu waandishi hakaja wasaidia?? Mgamba bwana!!
 
Mkuchika sasa!! analalamika sasa..anasema kwa newala hii yeye anaweza kutembea hata saa nane za usiku, bila askari! mbaya anaongea kilugha! anajisifu kwa mkutano aliofanya masasi...anadai, watu wa newala wakatae ujinga wa kudanganywa kuhusu gesi.
 
anaanza kwenye gesi..anasema atatoa elimu kuhusu gesi...mbaya anaongea kilugha na mimi sikipati...
 
Anasema yeye ni waziri wa maadili, na takukuru, na anasema wenzie wanamwita mr. clean! hana anachoongea zaidi ya kujisifu tu
 
Vijana wanazomea sana!! baada ya kusema wilaya ya newala imeendelea kuliko nyingine! Wanasema uongooo uongooo
 
Haya! twende sasa, anasema mambo mazuri aliyoyafanya atalipwa na Mungu...ila kashazomewa
 
Tupe vyombo mkuu usisahau picha ndo magamba wataamini
 
One measure of leadership is the caliber of people who choose to follow you. mkuchika hili alielewi
 
ndiyo maana mimi napendekeza kuanza kutumika kwa VIDEO LIVE COVERAGE kwa kutumia stream yoyote kwa walio na laptop za webcam au wenye video camera.kwa kifurushi cha tsh 10,000.(2gb vodacom) unarusha live kwa takribani massa 7.

tukifika hapo basi tunaweza kuondoa longo longo nyingi! nitakuja na idea moja kwa uongozi wa JF
 
Wamzomee sana ila wasimkong'ote jamani, hata mimi ningezomea sana. Ni namna tu ya kutoa maoni.
 
Anasema halmashauri inamiliki radio...
 
Haya! twende sasa, anasema mambo mazuri aliyoyafanya atalipwa na Mungu...ila kashazomewa

hayo mazuri aliyofanya alikua anatoa hela mfukoni kwake au ni kodi zetu? sadaka zetu baraka apewe mchungaji non sense, mwambie huyo mungu wake makao yake makuu yatakuwa pale lumumba
 
Watu wamekaa atention sana...waliokuja kwa lengo la kumsikiliza ni wachache sana!! wengi wamekuja kuzomea...kama kuna gamba aliyepo hapa, apinge sasa kinachoendelea hapa...
 
ndiyo maana mimi napendekeza kuanza kutumika kwa VIDEO LIVE COVERAGE kwa kutumia stream yoyote kwa walio na laptop za webcam au wenye video camera.kwa kifurushi cha tsh 10,000.(2gb vodacom) unarusha live kwa takribani massa 7.

tukifika hapo basi tunaweza kuondoa longo longo nyingi! nitakuja na idea moja kwa uongozi wa JF
Its good and am ready to support that technically, hata skype ingesaidia. Lakini ni wajibu wa JF admins kuweka hiyo mechanisim ya kuweza kurusha audio au video live kwenye website yao.
 
yeye kama mbunge anamarafiki na yeye ana kipato, amenunua bati 3000 amegawa kwenye makanisa, misikiti na mashuleni, amenunua baiskeli 47 za walemavu...maendeleo yake hayo!!
 
Anasali! "Baba uwasemehe wanaonizomea kwa kuwa hawajui watendalo"...akasema amen!
 
Back
Top Bottom