Kutoka kinywani mwa Dada @AshaDii!!!!

Kutoka kinywani mwa Dada @AshaDii!!!!

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Posts
2,377
Reaction score
3,394
avatar42040_16.gif


Inategemea kua hio shida ni of what nature.... Kuna ile kama inahusiana na chakula ndani, anaona tu aibu kusema nenda angalau kwa wazazi kaombe unga kidogo tumekwama... anaona bora akwambie kua "fanya maarifa"..... Kawaida ya mwanamke ambae ni mwerevu (walau that is what I think) ni kutambua kua sio kila siku mume wake ataweza provide - na kwamba hata kama anaweza inaweza tokea in rare cases akakwama. Daima kulinda heshima ndani ya ndoa yenu inatakiwa kua na akili ya ziada mkichwa na maarifa pia....

Hivo basi daima hata kama woote wanafanya kazi na woote wana provide, ni lazima aweke akiba pembeni popote pale ndani ya nyumba ambayo inakua ni kinga ya kutatua tatizo pale ambapo litajitokeza na woote wasiwe na pesa (yaani mume na yeye mwenyewe mke); Hio akiba sio wanaume woote hujua kua inakuwepo.... Inapotokea kua kuna siku mlikwama kabisa mara nyingi akina mama huchukua hio akiba kuokoa jahazi kwa kumshirikisha mumeo na kumwambia "mume wangu nimeazima kwenye kikundi chetu kile cha upaku" sababu ya kusema hivi sio kwamba humuamini mumeo.... No! Ila tu ni ile haitakiwi hajenge kichwani mwake kuna akiba ndani for next time akikwama he wont try harder..... Hivo baas mara nyingi wanaume husema hivo sababu wanakua weshawahi pita in jams na mke aliokoa jahazi.... Siamini kua hua wanasema hivo kwa maana kwamba nenda kwa mpango wa kando ukatafute pesa.

Aliyasema hayo wakati alipokuwa akichangia uzi huu hapa: https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/222523-kumwambia-mwanamke-fanya-maarifa.html
 
hilo nalo neno,vp Zinduna kwenye kibubu umefikisha Tshs ngapi au we unamalizia saloon na sare za kitchen party
 
Sikujua kama kuna michango ya watu ambayo kwa kweli ukiisoma inakuwa ni darasa tosha, muuliza swali The Boss alikuwa anataka kufahamu ni maarifa gani, kwani wanaume wengi walikuwa na mtazamo kuwa ni mambo ya mpango wa kando, lakini maoni ya dada AshaDii yamefafanua vizuri ili kuondoa hiyo dhana potofu...


Kutoka kinywani mwa mwanaJF itakuwa ni segment ambayo nimeianzisha itakayokuwa ikikumbusha maoni au majibu ya post mbalimbali zilizowahi kuwekwa hapa na kuwafikirisha watu.
 
hilo nalo neno,vp Zinduna kwenye kibubu umefikisha Tshs ngapi au we unamalizia saloon na sare za kitchen party
Kwa kweli n=nimepata darsa hapo kwenye hiyo posti ya da AshaDii na sasa nimeanza utaratibu wa kujifunza kuwek akiba mwenzangu, wanaume hawa, siku ukiambiwa fanya maarifa usijeenda kukopa kwa mpemba utaanguka naye!
 
ukiwa unaenda gengeni uwe unajitahidi kumtabasamia muuza genge ukikwama anakupa bure na nyongeza,au we ni wa supermarket kila kitu
 
Kutoka kinywani mwa mwanaJF itakuwa ni segment ambayo nimeianzisha itakayokuwa ikikumbusha maoni au majibu ya post mbalimbali zilizowahi kuwekwa hapa na kuwafikirisha watu.[/QUOTE]


ubunifu mzuri hongera
 
ukiwa unaenda gengeni uwe unajitahidi kumtabasamia muuza genge ukikwama anakupa bure na nyongeza,au we ni wa supermarket kila kitu
Huku kwetu waume ndio waendao markiti, sie twajua kupika tu basi kwa hiyo kauli hiyo ya kufanya maarifa labda nikiolewa huko Bara, lakini huku kwetu Wanaume ndio wafanyao maarifa
 
Kutoka kinywani mwa mwanaJF itakuwa ni segment ambayo nimeianzisha itakayokuwa ikikumbusha maoni au majibu ya post mbalimbali zilizowahi kuwekwa hapa na kuwafikirisha watu.


ubunifu mzuri hongera[/QUOTE]

Najaribu vionjo tofauti tofauti ili kuleta ladha mpya hapa MMU.
 
Huku kwetu waume ndio waendao markiti, sie twajua kupika tu basi kwa hiyo kauli hiyo ya kufanya maarifa labda nikiolewa huko Bara, lakini huku kwetu Wanaume ndio wafanyao maarifa

pole yenu aisee kwa hiyo kitu kinachoitwa ganji hamkijui kabisa,ndo maana mko laini laini mkiachwa mnakimbilia kuolewa tena coz hamjajizoesha kutafuta na kutumia maarifa,duh hebu ngoja nikutafutie wa bara fasta.
 
pole yenu aisee kwa hiyo kitu kinachoitwa ganji hamkijui kabisa,ndo maana mko laini laini mkiachwa mnakimbilia kuolewa tena coz hamjajizoesha kutafuta na kutumia maarifa,duh hebu ngoja nikutafutie wa bara fasta.
Yalisemwa haya,

Mwanamke atazaa kwa uchungu na mwanaume atakula kwa jasho, sasa nimzalie kisha ni msaidie kula kw ajasho, hiyo ni kazi yake bibi wewe (Just Kidding)
Mila na desturi za ZNZ we ziache kama zilivyo
 
Yalisemwa haya,

Mwanamke atazaa kwa uchungu na mwanaume atakula kwa jasho, sasa nimzalie kisha ni msaidie kula kw ajasho, hiyo ni kazi yake bibi wewe (Just Kidding)
Mila na desturi za ZNZ we ziache kama zilivyo

Ukisubiri ulishwe kwa jasho utasubiri sana..Mithal 31 Inasema mwanamke mwenye hekima huwalisha wa nyumbani kwake..
tuachane na hayo zenji hawajambo
 
Shida yenu( Zinduna et al ) mmekuwa monotonous mno.
Mtu kama AshaDii almost kila siku ataongea neno ambalo watu watalifurahia hapa.

Sioni sababu ya kuendelea kupaste tena kauli zake, maana zilishajipambanua tokea dahari... Tuwekeeni undergrounds na wengine ambao ni wakongwe, lakini hawapo majamvini kwa sasa, provided wamecomment kauli zenye mafunzo kwa jamii.

No wonder kesho ikabandikwa hapa post ya Lara 1, TB, Prisoner, gfsonwin, yani tunachezea mulemule.
Thats my view.
 
Last edited by a moderator:
Ukisubiri ulishwe kwa jasho utasubiri sana..Mithal 31 Inasema mwanamke mwenye hekima huwalisha wa nyumbani kwake..
tuachane na hayo zenji hawajambo

Hayo maandishi yanajichanganya kwanza.
Hawajambo leo jioni natua Dar, kwa maandalizi ya White Party kesho, nitafikia Msasani Peninsula
 
Shida yenu( Zinduna et al ) mmekuwa monotonous mno.
Mtu kama AshaDii almost kila siku ataongea neno ambalo watu watalifurahia hapa.

Sioni sababu ya kuendelea kupaste tena kauli zake, maana zilishajipambanua tokea dahari... Tuwekeeni undergrounds na wengine ambao ni wakongwe, lakini hawapo majamvini kwa sasa.
Thats my view.
PakaJimmy huo ni mwanzo tu, mpaka sasa nimeshakusanya nukuu za kina Faiza foxy, Chauro, Mrembo by Nature, cheusimangala, @Blakberry, The Finest, Kabakabana, @ETM na wengineo
 
Last edited by a moderator:
Mpaka siku mtu atambue kuwa kwenye ardhi kuna madini tofauti na haya tunayoyajua ndipo tutatambua umuhimu wa kufikiri nje ya box.
'
Dunia ina mambo muhimu kuliko tuliyonayo!
 
Zinduna,

Sie wa 1947, tunajua kuwa wake zetu hutunza pesa kwenye vipochi pochi vyao na nyingine tunazijua kabisa...kwa hiyo kauli kama hiyo hutumika ili kuwapa confidence kwamba ni wake bora ambao thamani yao haina cha kulinganisha nacho...

Kama mwanamume mbabe, huingia mwenyewe kwenye pochi na kuzibeba...tena kuna wengine huzipeleka kwenye yale mambo yao yale!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Babu Dark City, vijana wa leo hawaelewi kabisaaa. Manake wanaingia kwenye ndoa kuvuna na kula. Hawajaui kuna wakati wa kutindikiwa. Mwanamke humsitiri mwanaume na familia kwa ujumla. Hili ni fundisho kwa wanaume wanaotaka kucontrol mapato ya wake zao kwenye kutunza familia. Kuna siku utakuwa juu ya mawe kama january hii, afu unakuta kuna mjomba wako bila aibu anaamua kufariki (you wish ungemuambia subiri mwisho wa mwezi). Wife anakutoa kimasomaso na mnaenda msibani bila yeyote kujua!
 
Last edited by a moderator:
ubunifu mzuri hongera

Najaribu vionjo tofauti tofauti ili kuleta ladha mpya hapa MMU.[/QUOTE]

Thanks! hii kitu inawashinda watu wengu sana ndio maana maisha yakuwa magumu au wengine unasikia wameishia kuachana hata kwenye mahusiano unajua mahusiano ni kama sanaa hivyo inahitaji kuwa mmbunifu ili kila siku muwe wapya yaani mupenzi wako awe mpya na hii sio kwa wanawake tu hata wanaume. inabidi watu tuwe wabunifu kuanzia tunapoamka asubuhi vitandani mwetu, kwenye kazi na biashara zetu, tunapokuwa jikoni unajua kwamfano hii nyanja ya jiko unaweza kuta mapishi kwamfano ya mchele, ukawapa watu watano the same mchele lakini ukija mezani unaweza kuona mambo ya ajabu sana . na hatimaye kunako tendo la ndoa kote huko inatakiwa kila siku tuwe wapya. hapo maisha yatakuwa mazuri.
sio ukiona mwenzako kaazisha sehemu ya kufanyia bishara yake au aina flani ya kazi ukaona kesho wateja wawili wameingia unasema hiyo kazi inalipa na wewe unaenda kufungua tena next to him na kila ndio maana mafanikio yanakuwa magumu haswa katika dunia ya leo ya mdororo wa kiuchumi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom