Kumwambia mwanamke 'FANYA MAARIFA' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumwambia mwanamke 'FANYA MAARIFA'

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by The Boss, Feb 10, 2012.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Kuna baadhi ya familia ....mwanaume akishindwa baadhi ya majukumu yake hasa ya kipato ni kawaida kusikia mume akimwambia mkewe 'fanya maarifa' au ufanye maarifa basi'.......

  Hivi hili hasa linaamaanisha nini?

  Maarifa gani ambayo mwanaume akishindwa, mwanamke ndo ataweza?

  Halafu unakuta mwanamke 'anafanya kweli maarifa' na maisha yanakwenda...

  Sasa 'haya maarifa' ya wanawake ni yapi?
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  maarifa ni mengi kwa mwanamke
  hasa village girls
  utaomba unga kwa jirani
  utakuwa na bustani ya viazi
  utakuwa na bustani ya mboga mboga
  utakusanya kuni uuze

  so many
   
 3. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  maarifa ni kuwa na kibuzi,lol
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  kwa mjini
  unaweza enda kopa kwa mangi
  mme akipata pesa unaenda lipa
  au unakopa kwa mama jirani
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  hakuna mme anayemaanisha mke atafute kibuzi unless ni marioo

   
 6. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Ndio zako hizo basi marufuku kufanya hayo maarifa
   
 7. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Sio siri wanaume tunawadharau wanawake ila katika kufanya maarifa nawapa big up sana maana anaweza akafanya maarifa mpaka ukashangaa mwanaume mimacho inakutoka udhani kagawa nje kumbe hapana
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  wanawake wengi wa mjini
  kufanya maarifa ni kwenda kwa kibuzi......ndo maana hili neno la kufanya maarifa linanitatiza mno...
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  na mimi naona weengi ndo wanachofanya...
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  utamchotea mtu maji upate hela
  utapita kwa watu kufua nguo
  utachoma chapati, mandazi and the like
  utapika uji uuze stend jioni
   
 11. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #11
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Inategemea kua hio shida ni of what nature.... Kuna ile kama inahusiana na chakula ndani, anaona tu aibu kusema nenda angalau kwa wazazi kaombe unga kidogo tumekwama... anaona bora akwambie kua "fanya maarifa"..... Kawaida ya mwanamke ambae ni mwerevu (walau that is what I think) ni kutambua kua sio kila siku mume wake ataweza provide - na kwamba hata kama anaweza inaweza tokea in rare cases akakwama. Daima kulinda heshima ndani ya ndoa yenu inatakiwa kua na akili ya ziada mkichwa na maarifa pia....

  Hivo basi daima hata kama woote wanafanya kazi na woote wana provide, ni lazima aweke akiba pembeni popote pale ndani ya nyumba ambayo inakua ni kinga ya kutatua tatizo pale ambapo litajitokeza na woote wasiwe na pesa (yaani mume na yeye mwenyewe mke); Hio akiba sio wanaume woote hujua kua inakuwepo.... Inapotokea kua kuna siku mlikwama kabisa mara nyingi akina mama huchukua hio akiba kuokoa jahazi kwa kumshirikisha mumeo na kumwambia "mume wangu nimeazima kwenye kikundi chetu kile cha upaku" sababu ya kusema hivi sio kwamba humuamini mumeo.... No! Ila tu ni ile haitakiwi hajenge kichwani mwake kuna akiba ndani for next time akikwama he wont try harder..... Hivo baas mara nyingi wanaume husema hivo sababu wanakua weshawahi pita in jams na mke aliokoa jahazi.... Siamini kua hua wanasema hivo kwa maana kwamba nenda kwa mpango wa kando ukatafute pesa.


  Boss it has been Long.... Usiku mwema.
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Sasa hayo maambo ni mpaka yaonekane...
  mwingine huoni chochote but pesa tu imepatikana
   
 13. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Mwanamme anafikiri,anatafuta,anahenya,anateseka ili familia yake ipate kuishi (namzungumzia mtu wa aina hiyo)..Inafikia nyakati kila anachkifanya kinagonga mwamba,mambo si kama yalivyokuwa awali.....Kwa kiswahili cha kisiasa inabidi kufunga mkanda..tuingie kwenye dharula ya muda.

  Mambo yasiyo ya kawaida katika familia kama kunywa chai,kununua nguo mpya,kutumia mafuta mengi kwenye mboga,viungo visivyo vya lazima kama pilipili hoho vyote vinasitishwa..Mwendo unakuwa ni wa kula ili kuishi.Na ni nani waziri wa jiko na mambo ya dharula ? - Ni mwanamke..ndipo mwanaume anatoa wito..fanya maarifa - yaani tumia kila kilichopo kwa akili.
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  wengi ni wangapi?
  Na sehemu gani ulofanya hii observation?

  machangu ni wengi
  lakini si kila mwanamke anatafuta suluhisho kwa kuwa na kibuzi
  wapo wenye maisha magumu ya kuunga na bado ni decent tu

  kama mtu kaoa kicheche kilichokua bila kufanya kazi kitatafuta buzi
  vinginevyo, wanawake wengi wanafanya a lot kwa ajili ya familia zao bila kujishusha.

   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  umeongea vizuri..
  na nina uhakika hakuna mwanaume anaetegemea mkewe
  aende nje kwa 'kufanya maarifa'
  ishu hapa ni je hii haiwezi kuwa kisingizio kwa baadhi ya wanawake...????
  na je ni sahihi kwa mwanaume kumwambia mkewe 'fanya maarifa'??
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  mme akipokea atakuwa yeye ndo ana tatizo
  ni sawa na kumwona binti yako wa std 6 ana simu afu unatizama tu

  kama mme lazima uulize kapataje hizo pesa

   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  nielewe my point...
  nafahamu weengi wanafanya maarifa bila kujishusha
  na wana mipango kadhaa wa kadhaa kama vikundi vya kukopeshana na kadhalika..

  but wapo baadhi nionavyo mimi 'kumwambia fanya maarifa'
  ni kama umemtuma 'akafanye maarifa' hayo jestina aliyozungumzia..
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  kwa nini udhani 'kagawa nje'??????
   
 19. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #19
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  asante nitonye, angalau unawapata wanawake wa ukweli wanaweza fanya tukio bila kugawa ugoro

  me love all mamas out there waho stood up for their families bwana.

   
 20. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Ni kwa sababu ameweza kufanya kile ambacho kimekushinda kwa hiyo huamini macho yako unaishia kuwa hisia tofauti
   
Loading...