Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,437
- 1,025
Katibu mkuu wa CCM bwana wilson mukama amekituhumu chama cha chadema kuingiza nchini hususani jimbo la Igunga Tabora,vijana 33 waliopewa mafunzo ya kikomandoo.Alidai kwamba vijana hao wameletwa kwa malengo ya kufanya vurugu katika kampeni za uchaguzi na wengine wamefichwa sehemu fulani kujiandaa kufanya vurugu endapo mambo hayatakwenda vizuri kwa CHADEMA.Alidai zaidi kwamba vijana hao wamepewa mafunzo katika nchi za Libya,Afghanistan na Palestina.Alipohojiwa kuhusu hili suala,Slaa alikanusha na kudai kwamba si kweli.Slaa akaeleza zaidi kwamba kama ni kweli CHADEMA imefanikiwa kupenyeza vijana hao 33,basi serikali ya TZ iliyo chini ya CCM haiko makini na usalama wa Taifa lake na badala yake CHADEMA ndio chama makini.Hata hivyo Slaa hakutaka malumbano na Mukama na amemsamehe bure.source:TBC 1.