Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,189
- 128,283
Nilijiuliza sana sababu ya kumuweka Mukama kumrithi Makamba mropokaji, leo hii ndo nimegundua kuwa kumbe mukama ni mtupu kichwani namna hii. Dr Slaa ameshatoa jibu ingawa muandishi wa thread ameonyesha bias. Mukama anaishutumu wizara ya ndani na usalama wa raia kushindwa kuzibiti hao anaowasema ni makomandoo kutoka mataifa mbalimbali. Said mwema anapaswa kumuhoji mukama kupata ushaidi wa kuwakamata hawa makomandoo waliopitiliza mpaka igunga bila kukamatwa licha ya makamanda maalumu wa polisi waliojazwa Igunga kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wakati wa uchaguzi.Katibu mkuu wa CCM bwana wilson mukama amekituhumu chama cha chadema kuingiza nchini hususani jimbo la Igunga Tabora,vijana 33 waliopewa mafunzo ya kikomandoo.Alidai kwamba vijana hao wameletwa kwa malengo ya kufanya vurugu katika kampeni za uchaguzi na wengine wamefichwa sehemu fulani kujiandaa kufanya vurugu endapo mambo hayatakwenda vizuri kwa CHADEMA.Alidai zaidi kwamba vijana hao wamepewa mafunzo katika nchi za Libya,Afghanistan na Palestina.source:TBC 1.