Kutoka Igunga

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Katibu mkuu wa CCM bwana wilson mukama amekituhumu chama cha chadema kuingiza nchini hususani jimbo la Igunga Tabora,vijana 33 waliopewa mafunzo ya kikomandoo.Alidai kwamba vijana hao wameletwa kwa malengo ya kufanya vurugu katika kampeni za uchaguzi na wengine wamefichwa sehemu fulani kujiandaa kufanya vurugu endapo mambo hayatakwenda vizuri kwa CHADEMA.Alidai zaidi kwamba vijana hao wamepewa mafunzo katika nchi za Libya,Afghanistan na Palestina.Alipohojiwa kuhusu hili suala,Slaa alikanusha na kudai kwamba si kweli.Slaa akaeleza zaidi kwamba kama ni kweli CHADEMA imefanikiwa kupenyeza vijana hao 33,basi serikali ya TZ iliyo chini ya CCM haiko makini na usalama wa Taifa lake na badala yake CHADEMA ndio chama makini.Hata hivyo Slaa hakutaka malumbano na Mukama na amemsamehe bure.source:TBC 1.
 
Katibu mkuu wa CCM bwana wilson mukama amekituhumu chama cha chadema kuingiza nchini hususani jimbo la Igunga Tabora,vijana 33 waliopewa mafunzo ya kikomandoo.Alidai kwamba vijana hao wameletwa kwa malengo ya kufanya vurugu katika kampeni za uchaguzi na wengine wamefichwa sehemu fulani kujiandaa kufanya vurugu endapo mambo hayatakwenda vizuri kwa CHADEMA.Alidai zaidi kwamba vijana hao wamepewa mafunzo katika nchi za Libya,Afghanistan na Palestina.source:TBC 1.

Mbona hujaandika majibu ya Dr. Slaa kuhusu hili suala? Nina shaka na lengo lako au edit iwe balanced.
 
Kama ana uhakika huo kwanini wasiwakamate! halafu huko Libya, Palestina na Afghanistan hao Chadema waliwapeleka lini hao vijana maana RA kajiuzulu takribani miezi miwili tu iliyopita, eti wamewaficha sehemu fulani hawa TBC1 nao ushabiki utawarudisha enzi zile za TvT na watakosa watazamaji! hii sio habari ya kurusha hewani ina mapungufu mengi sana kwa watu makini!
 
Wakati wa uchaguzi mkuu CCM walikuwa na green guard, mbona hakuna mwana CCM aliyeliongelea hilo? Iwe ni kweli au uongo ccm wamejitakia yote!
 
Slaa alipohojiwa,alikanusha na akasema huu wote ni uzushi.Slaa akaelezea zaidi kwamba kama ni kweli CHADEMA wamefanikiwa kupenyeza hao vijana 33 hapa nchini,serikali ya TZ chini ya CCM haiko makini na usalama wa Taifa lake na CHADEMA ndio wako makini zaidi.Slaa amesema amemsamehe bure bwana Mukama kwa kuongea uwongo na uzushi.
 
Halafu bwana mukama anadai CHADEMA wana kikosi chao kinachoenda kwa jina la RED GUARD!
 
Slaa alipohojiwa,alikanusha na akasema huu wote ni uzushi.Slaa akaelezea zaidi kwamba kama ni kweli CHADEMA wamefanikiwa kupenyeza hao vijana 33 hapa nchini,serikali ya TZ chini ya CCM haiko makini na usalama wa Taifa lake na CHADEMA ndio wako makini zaidi.Slaa amesema amemsamehe bure bwana Mukama kwa kuongea uwongo na uzushi.

haya maelezo ulipaswa kuyaweka kwenye thread vinginevyo watakuelewa unania kama ya tbc
 
Ukweli CCM itajutia sana kumchagua Mkama kama katibu mkuu, awali ilidhaniwa kuwa Makamba ndiyo mchawi lakini ukweli umedhihiri kuwa mchawi mwingine bado yupo tena ni Mkama. Kwa jinsi alivyoongea amewafedhehesha sana UWT kuwa ni wazembe wasiofuatilia watu. Kifupi alidhani atakinukisha chama cha CDM kumbe indirect ameinukisha serikali kwa kutokuwa makini.
Igunga iitaibua mabo mengi sana.
 
Watajuta sio kidogo... Ngoja tusubiri
 
naomaba mods hizi thread zote zaigunga ziwekwe sehemu moja ilikupunguza misongamano kwenye server...
 
Kama ana uhakika huo kwanini wasiwakamate! halafu huko Libya, Palestina na Afghanistan hao Chadema waliwapeleka lini hao vijana maana RA kajiuzulu takribani miezi miwili tu iliyopita, eti wamewaficha sehemu fulani hawa TBC1 nao ushabiki utawarudisha enzi zile za TvT na watakosa watazamaji! hii sio habari ya kurusha hewani ina mapungufu mengi sana kwa watu makini!

big up sana mkuu nakuunga mkono 100%.
 
Back
Top Bottom