CHADEMA mnatakaje Tume ya majaji kwa kila kitu na jambo wakati huwa mnasema wanapokea maagizo kutoka mamlaka za juu?

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,280
9,719
Ndugu zangu Watanzania,

Kuna mambo ukiwasililiza CHADEMA na wafuasi wake unabaki unacheka mwenyewe tu. Na kama kiongozi ukitaka uwasikilize CHADEMA kwa kila kitu ni lazima wakupoteza tu ,maana ni vigeu geu,walalamishi na watu wasio lizika wala kuwa na moyo wa shukurani au kupongeza jambo. Wao kila kitu kwao ni kibaya na hakifai .leo wanaweza zungumza jambo fulani juu ya kundi fulani kulikandia na kuliponda halafu kesho wakalitaka tena.kwa hiyo kama huna msimamo thabiti na madhubuti ni lazima uyumbe tu.

Mfano utawasikia CHADEMA wakisema katika mchakato huu wa miswaada hii ya sheria za uchaguzi na tume huru ya uchaguzi basi kuwe na tume ya kijaji ambayo ndio itakayo fanya na kuwafanyia usaili wajumbe mbalimbali pamoja na mkurugenzi wake na kusimamia na kuongoza michakato yote Na kwamba Rais Asihusike wala kuhusishwa kwa lolote lile.

Swali ni je hao majaji wanateuliwa na nani? Wanakula kiapo na kuapishwa na nani baada ya kuteuliwa? nani atawapendekeza hao majaji? Ni vipi Rais Anaweza kushindwa kupenyeza na kuweka mkono wake anapotaka asipokuwa na dhamira njema? Ni wapi katika mifumo yetu ya kiafrika ambapo Rais anaweza kushindwa kufikisha mkono wake akitaka? Hivi ninyi kwa akili yenu mnaichukuliaje taasisi ya Urais? Hivi mnafikiri ni mtu mmoja mnayemuona kama Rais? Ni wapi ambako watu wa Rais na taasisi yake unakoweza kuwakwepa?

Kwa ufupi ni kuwa hao majaji mnawatoa wapi kama siyo hawahawa walioteuliwa na kuapishwa na mheshimiwa Rais wetu mpendwa?

Hapo kenya tu wakati wa chebukati hamkusikia Raila Odinga akijiliza liza kuwa mwenyekiti wa tume huru ya kenya na mipaka ikiwa chini ya chebukati ilifanya hujuma? Lakini si ndio tume ambayo mlikuwa mnaisifia sana pamoja na katiba yake? Je pamoja na ubora wa katiba ya kenya pamoja na tume ya uchaguzi na mifumo ya mahakama kuna siku Raila Odinga ameacha kulalamika na kuilalamikia?

Je siyo ninyi CHADEMA ambao kila siku huwatukana waheshimiwa majaji wetu kuwa wanapokea maagizo kutoka juu? Siyo ninyi ambao husema hamna imani na majaji wetu? Siyo ninyi ambao husema hawana weledi katika kusimamia sheria kwa uhuru na kwamba hata hukumu huandikiwa kwa matakwa ya watu fulani wa juu kupindisha hukumu? Siyo ninyi ambao huwaponda sana hasa pale mnapokuwa mmeshindwa kesi?

Sasa leo ni vipi hawa majaji wanakuwa malaika kwenu? Mara ngapi mmewadhalilisha na kuwashushia heshima?

Ningependa kuwaambieni kuwa muaminini sana Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan, mpeni ushirikiano na muungeni mkono katika dhamira yake njema ya kutaka kuona uchaguzi unafanyika katika mazingira huru na ya haki na yenye kuleta na kujenga hali ya kuaminiana,yenye kuweka uwanja sawa katika mchakato wote wa uchaguzi.

Acheni vichoko choko vyenu.acheni kuwa walalamishi kupita kiasi.msipende kudeka deka na kuonekana ninyi tu ndio mnaoonewa kila siku na kila wakati ,.mkileta yale ya 2014 ya kujifanya mnatoka ndani ya bunge la katiba na kususa mchakato nawaambieni kuwa hakuna atakaye wabembeleza,hakuna atakayesimamisha mchakato kuwasubilini bali mchakato utaendelea kama kawaida bila uwepo wenu .

Pia nawashaulini katika siasa usitake na kulazimisha upate kila kitu kwa wakati mmoja .kubali wakati mwingine kupata hiki na kuachia hiki na kuendelea kutafuta ulichokikosa kwa wakati huo.mimi kama mwana siasa nawashaulini sana katika hili CHADEMA kuwa kwenye siasa hupati vyote na yote kwa wakati mmoja .chukua kinachopatikana kwa wakati huo kitakachokuwezesha kupata kingine ulichokosa kwa wakati huo.

Ni lazima mjue namna ya kuyaendea mambo.acheni mihemuko ya vijana wenu waliokosa maadili na uelewa mzuri.fanyeni mambo Kiutu uzima na kiukomavu na siyo kukimbilia kususa susa kila kitu kama watoto wadogo .mtalala na njaa na hasara itakuwa kwenu. Ni lazima mkue kiakili na kupevuka kifikra. ni lazima mjenge ukomavu wa kiakili na kuwa watulivu kwa kila jambo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
..kamati ya usaili yenye wajumbe ambao ni wadau ktk suala husika itapunguza influence ya Raisi ktk uteuzi.

..hivi kuna ulazima gani wa Ccm kung'ang'ania Mwenyekiti wenu na makada wenu wawe na kivuli kikubwa ktk kuendesha uchaguzi?
 
Kwani hao majaji mnaowataka wanateuliwa na nani? Mtawatoa wapi nje na hawa walioteuliwa na kuapishwa na Rais Mwenyewe? Mmeanza lini kuwa na imani na majaji wetu wakati kila siku mnasema wanapokea maagizo kutoka juu?
 
..kwani ni uongo hakuna majaji wahuni wanaopokea maagizo toka kwa mwenyekiti?
 
Kwani hao majaji mnaowataka wanateuliwa na nani? Mtawatoa wapi nje na hawa walioteuliwa na kuapishwa na Rais Mwenyewe? Mmeanza lini kuwa na imani na majaji wetu wakati kila siku mnasema wanapokea maagizo kutoka juu?

Usiwe mpotoshaji. Nchi hii imewahi kuwa na majaji wenye heshima kubwa, na majina yao hayatafutika katika kutetea haki na kupigania nchi kuwa na sheria nzuri.

Ukiwa na nafasi na uelewa mzuri, kapitie taarifa ya Tume ya Jaji Nyalali, ndiyo utaelewa.

Majaji wa mchongo wanaopokea maelekezo ya ikulu ni wale maafisa wa TISS waliopachikwa ujaji ili watekeleze matakwa ya ikulu. Na hawa, wengi wao waliteuliwa wakati wa awamu ya 5, na baadhi wanafahamika kwa majina.

Wazo la majaji kutumika katika kuteua watendaji wa Tume ya Uchaguzi halina ubaya, alimradi wajumbe wote wa hiyo Tume ya majaji wawe wameridhiwa na wadau wa uchaguzi.
 
..halafu 2014 mchakato wa katiba uliendelea mpaka ikapatikana katiba pendekezwa.

..sasa tuwaulize ccm waliopitisha katiba pendekezwa kwanini hawakuendelea na mchakato?
 
Usiwe mpotoshaji. Nchi hii imewahi kuwa na majaji wenye heshima kubwa, na majina yao hayatafutika katika kutetea haki na kupigania nchi kuwa na sheria nzuri.

Ukiwa na nafasi na uelewa mzuri, kapitie taarifa ya Tume ya Jaji Nyalali, ndiyo utaelewa.

Majaji wa mchongo wanaopokea maelekezo ya ikulu ni wale maafisa wa TISS waliopachikwa ujaji ili watekeleze matakwa ya ikulu. Na hawa, wengi wao waliteuliwa wakati wa awamu ya 5, na baadhi wanafahamika kwa majina.

Wazo la majaji kutumika katika kuteua watendaji wa Tume ya Uchaguzi halina ubaya, alimradi wajumbe wote wa hiyo Tume ya majaji wawe wameridhiwa na wadau wa uchaguzi.
Hao majaji utawapata kwa njia ipi? Nani atawateua? Nani atawaapisha?
 
Back
Top Bottom