Kutoka G20 hadi APEC, China yatoa mipango yake juu ya maendeleo na usalama ya dunia

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
1129130810_16685341611971n.jpg


1129131285_16685348673211n.jpg

Kuanzia tarehe 14 hadi 19 Novemba 2022, Rais Xi Jinping wa China alihudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kundi la G20 (G20) kisiwani Bali, Indonesia, na Mkutano wa Viongozi wa Kibiashara wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC) mjini Bangkok, Thailand. Katika siku hizi sita, rais Xi alihudhuria shughuli zaidi ya 30, iwe ni hotuba zake katika mikutano au mazungumzo yake ya ana kwa ana na viongozi wa nchi mbalimbali na mashirika ya kimataifa, huku mipango ya China kuhusu maendeleo na usalama duniani ikipewa msisitizo. Hii sio tu inalingana na ripoti ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) iliyosema kwamba "China daima inashikilia sera ya mambo ya nje ya kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo ya pamoja, na kujitahidi kukuza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja", lakini pia inaonyesha nguvu ya China katika kushirikisha pande zote kukabiliana na changamoto za pamoja.

Katika zama za leo, dunia inagawanyika kutokana na tofauti za itikadi, huku pengo la maendeleo kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea linazidi kuongezeka, na mambo kama vile janga la COVID-19 na mabadiliko ya hali ya hewa yameathiri sana uchumi wa dunia, mambo ambayo yanatoa changamoto kubwa kwa nchi mbalimbali hasa zinazoendelea. Kwenye mazingira haya, nchi zinaweza kupata maendeleo ya aina gani? Rais Xi Jinping alitoa mapendekezo matatu: "ujumuishi, kunufaishana na ustahimilivu". Ujumuishi unamaanisha kwamba nchi zote zinapaswa kuweka kando tofauti na kukuza maoni ya pamoja huku zikijenga uchumi ulio wazi; kunufaishana ni kusisitiza kwamba kila nchi ina haki ya kujiendeleza kisasa; na ustahimilivu nao unatoa wito wa kusaidia nchi zinazoendelea kujenga uchumi unaoweza kustahimili hatari na changamoto.

Ni wazi kwamba, mapendekezo haya matatu yanatolewa kwa kuangazia maslahi ya nchi zinazoendelea na kutia msukumo katika kuleta maendeleo endelevu duniani. Rais Xi Jinping pia ameeleza kuunga mkono Umoja wa Afrika kujiunga na G20, jambo ambalo limesifiwa na nchi nyingi zinazoendelea. Mwakilishi wa Umoja wa Afrika nchini China Rahamtalla M. Osman amesema kuwa, ni nchi chache sana kama China ambazo zinaweza kutimiza ahadi zao, na ikiwa Umoja wa Afrika unaweza kujiunga na G20, utafaidika na uchumi wa dunia.

Maendeleo duniani yanapatikana katika mazingira ya kimataifa yenye amani na utulivu. Jambo lingine muhimu rais Xi Jinping alilozungumzia ni "usalama". Amesisitiza kuwa machafuko na migogoro inapaswa kutatuliwa kwa njia za amani kama vile mazungumzo na mashauriano kwenye msingi wa Katiba ya Umoja wa Mataifa. Kuhusu mgogoro kati ya Russia na Ukraine, China siku zote imesimama kwa upande wa amani, ambapo Rais Xi Jinping amerudia tena msimamo kuwa, silaha za nyuklia hazipaswi kutumiwa, na vita vya nyuklia havipaswi kupigwa. Kwenye masuala ya usalama mpya kama vile usalama wa chakula na nishati, Xi Jinping alisema moja kwa moja kwamba "Chanzo kikuu cha mizozo hiyo si masuala ya uzalishaji na mahitaji, lakini ni tatizo la mnyororo wa ugavi, ambalo limevuruga ushirikiano wa kimataifa. China imetoa pendekezo la ushirikiano wa kimataifa wa usalama wa chakula, na inatarajia kuimarisha ushirikiano na pande zote.” Haya yote yanaonyesha busara, kujiamini na uwajibikaji wa China kama nchi kubwa duniani.

Dunia inazidi kuwa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ambapo mimi niko miongoni mwenu na wewe ni miongoni mwetu. Ripoti ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC ilieleza kuwa "kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja ni njia ya kutimiza mustakabali mzuri kwa watu wa nchi zote duniani." Inapokabiliwa na masuala ya kimataifa kama vile maendeleo na usalama, hakuna nchi inayoweza kuyatatua peke yake. Jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja ndio lengo na pia njia ya kufikia maendeleo na usalama.

Leo, maendeleo ya haraka ya uchumi wa China na utulivu wa kijamii wa muda mrefu umezihimiza nchi zinazoendelea zikiwemo nchi za Afrika kutimiza ndoto zao za maendeleo. Kama alivyosema Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi cha Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, “Naamini kuwa Chama cha Kikomunisti cha China kitawaongoza Wachina kusonga mbele kwa ujasiri katika safari mpya ya ujenzi wa nchi ya kisasa ya ujamaa katika pande zote, na kuendelea kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. Natarajia China itaendelea kutoa fursa mpya kwa dunia kupitia maendeleo yake mapya, na kuchangia hekima na nguvu zaidi kwa amani na maendeleo ya dunia pamoja na ustaarabu wa binadamu."
 
Back
Top Bottom