Kutoka bungeni: Jimbo la Mtera limekosa mbunge!

Mchango wa wenje ulikuwa mzuri sana...nilipenda pale alikopiga kwamba.serikali hii hii ndiyo iliyotupa fursa za kusoma lakini hiyo hiyo ndiyo iliyowanyima wengine fursa ya kusoma kama akina Livingstone Lusinde ! ! !
 
Mchango wa wenje ulikuwa mzuri sana...nilipenda pale alikopiga kwamba,serikali hii hii ndiyo iliyotupa fursa za kusoma lakini hiyo hiyo ndiyo iliyowanyima wengine fursa ya kusoma kama akina Livingstone Lusinde
 
Jamani kuna mbuge huyu wa jimbo la Mtera ama kweli ni kilaza,hivi sasa amemaliza kuchangia hoja bungeni kuhusu bajeti ya Wizara ya mambo ya ndani.Kinachonishangaza ni kuona baada ya kuzungumzia matatizo ya wananchi waliyomtuma kwa ku-link matatizo hayo na wizara husika yeye muda wote anaumalizia kwenye kurusha vijembe na kuwashambilia wapinzani.
Huyu huyu ndie jana aliyeomba muongozo wa kuwataka wabunge waletewe daktari awapime akili mda mfupi tu baada ya mbunge wa cdm kumaliza kutoa mchango wake,lakini kumbe nimegudua kuwa yeye ndiye anatakiwa kupimwa akili maana baada ya kutoa michango ya kuitaka serikali ililetee jimbo lake maendeleo yeye ndio kabsaaaa kageuka kuwa Waziri wa wizara husika na kuanza kuitetea serikali.

Unafikiri alizaliwa Mtera kwa makosa?? Mungu aliamua kumweka karibu na Mirembe hospital ili mambo yakichachamaa juu awe karibu na familia.
 
Teh teh , lusindi kilaza sana, maana hata angeenda darasani hangekuwa ameelimika
 
nilipomwona jana akiomba mwongozo na kutaka wabunge wapimwe akili nilifikiri yeye hayumo kwenye list kumbe ndio Na 1....alinyoosha kidolo kimoja kumbe vinne vinamwangalia yeye
 
Maskini Lusinde wa watu. Kwahiyo hajajibu hilo dongo? CCM jamani akh!
 
duh, jamaa upupu kweli...Nilitamani kuzima TV kuliko kumsikiliza, lakini busara ikanituma niendeelee kumsikiliza.Mwishowe nikatapika..agrrr agrrriiii agriiii ****y you..Anatia hasira na kinyaa at the same time....
 
Wenje anasema elimu ni haki na si upendeleo, CCM imeifanya elimu kwa wananchi ni previledge na matokeo yake ni kunyima fursa watu kusoma na kumtolea nafasi mheshimiwa Lusinde kuwa matunda ya mfumo huo wa CCM, amekosa elimu kwa sababu tu muono hasi wa CCM na kumsihi Waziri Nahodha alione hilo....
Hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!

Mkuu Lusinde hajaomba mwongozo kutokana na speech ya wenje?? ama hakuwepo bungeni?
 
Lusinde ni mmoja kati ya majuha ambayo hayajui yalienda mjengoni kufanya nini,aliniuzi sana jana baada ya mbunge wa chadema kumaliza kuongea,ina maana wabunge walio upinzan ni machizi?alafu na mwenyekiti jenista anafurahia upuuzi wa lusinde kana kwamba alichokisema kilikua na tija kwenye hotuba ile.
 
Nimempenda Wenje anasema kuondolewa bungeni na kuwekwa lumpango kwa wabunge wa upinzani 'it's not a big deal'kwani hyo ndo parliamentary democracy kwani huko nchi za nje watu wanatiana mpaka makonde na amewapongeza wabunge wote waliopigwa ndani kwamba hata yeye anajivunia hilo na akawaambia hata yeye leo yuko tayari kupelekwa jela kwani hata wakati wa kudai uhuru waafrika waliteswa na wengine kukatwa mikono na bado uhuru ulipatikana...people's...!!

Alienda mbali zaidi akasema maandamano yako pale pale,ametolea mfano Malawi maisha yamepanda bei watu wanaandamana sasa hapa Tz nchi iko gizani kwa nini tusiandamane
 
kwani lusinde hajasoma?
naona wanamsema yule mbunge lamerk wa mwanza ambaye kashagoma kabisa kuhudhuria vikao vya bunge kisa anasema anataka kuwa bega kwa bega na wapiga kura wake. kumbe anakimbia hoja za upinzani - jamaa ni seven ya miaka ile ya 80.
 
It was lovely and nice presentation. Wenje Big up.

Alisema eti mawaziri wanapiga deal kam Rich,Rada etc na wanafanya sherehe wakichaguliwa meno nje kusaini kikataba
Je trafic kwanini aile elfu ishirini. Wakubwa waache na wadogo pia waache. Trafic fine zikomeshwe tuanze utaratibu wa adhabu za kufagia town.
 
Du! Kweli CDM itawatoa tongotongo wengi waliofikiri siasa ni mchezo wa kuigiza na uongo uliokomaa. Siasa ni kazi kama kubeba zege; wacha wanaume waongoze, sisi tuko nyuma yao, hongera, hongera CDM!! Nani anaesema CDM hawana adabu bungeni ? Nani asiye na adabu kati ya CDM na wao wanakubali kuchezewa na wanamagamba hali wametulia kama maji mtungini? Wacha hoja na ngumi zilindime adabu itakuja baadae automatically.
 
bado anawazia lile gari la padri lililozaliwa nahisi lipo clinic alikuwa anawahi kupewa taarifa kama linaumwa nn ili aje atutangazie tena
 
Back
Top Bottom