Kweli wakubwa mmenena kweli tupu huyu jamaa anawalakini maana ongea yake ni kama muimbaji wa mipasho, pale politics hakuna ila alibahatisha tu by chance! Mimi nilichogundua kwake japo nikwamuda mfupi ni kwamba jamaa anakuwa anataka atoe hoja zake kwa style wanayotumia vijana machachari wa CDM huku akiwa amesahau kuwa wenzake wako well detailed na wanajiamini kwakuwa hawana hofu ya kumuuzi yeyote na baadae kuja kukosa uteuzi kama Mzee Shelukindo bali wanawakilisha wapiga kura wao na kuangalia maslah ya taifa kwa ujumla. Pia anaonekana hana ufahamu wa mambo mengi kwa kina maana hoja zake zote ni kudandia nadhani huyu jamaa anapenda ajulikane kwa kuonekana kilakitu kachangia japo ni pumba. Kwa kifupi hana dhamira ya dhati katika mambo ya msingi kwa taifa. Kama atapinga hoja hii basi namsihi awe jasiri aombe mdahalo na kijana yeyote pale CHADEMA ila asiwe Mbowe, Dr. Slaa, Tundu Lisu, Zito, Lema, Wenje, Mnyika, Msigwa wala Halima Mdee maana hao kwa mtizamo wangu hata viongozi wake wa juu wanawaogopa kuliko ukoma!