Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

Mimi naisubiri sana siku atakapojiuzulu sababu ya afya ...ili aepuke aibu iliyo mbele yake...alidhania uraisi ni rahisi hivyo???apumzike sababu ziko nyingi sana kubwa iwe afya.....inatosha aichie nchi.........hana jipya wala hajawahi kuwa nalo
....Mkuu,hebu fafanua kidogo kwa hilo la AFYA....je unamaana akajiuzulu kwa sababu nyingine licha ya hiyo ya Afya Nchi haitamuelewa au??,najua hapa Nyumbani(TZ) Afya za watu/public figures huwa ni siri binafsi je Mkulu anahistoria yeyote ya matatizo ya Ki-afya??
 
Hio hutuba haijaanza? Please hebu tupeni mlenda nasi tushushie
 
hivi wakuu, huu utaratibu wa kuhutubia 'wazee' umekaaje nchi hii? Hao wazee ni kina nani hasa na mtu anatakiwa awe na umri/qualification gani ili aweze kuingia kwneye hicho kikao cha 'wazee'? Je ni wale waliopigania uhuru? Kama ndivyo ni wangapi wapo hai, na kama wapo, wana uelewa gani wa mambo yanayoendelea sasa hivi duniani?

Naombeni msaada wenu katika hili, maana kila kukicha nasikia mara raisi analihutubia taifa 'kupitia wazee' mara leo atahutubia wabunge....jamani wabunge.....kupitia 'wazee' vilevile....sasa sijui tunakoelekea ni wapi? Na hapa sina maana ya kuwadharau wazee, hapana, ningependa tu kujua hao 'wazee' wa miaka yote ni kina nani hasa? Tangu uhuru?

wazee ni grease ya taifa!
 
Bunge letu linaanza vikao vyake leo asubuhi. Naomba wadau tupeana habari na kujadili hoja mbali mbali zitakazo tolea.

Title ya thread ni yaliyojiri bungeni leo lakini mada inayojadiliwa ni hotuba ya JK atakayosoma leo Dadoma tena kwenye Hoteli ya Kilimani ikiwakusanya baadhi ya wabunge na wazee na wafurukutwa.

Yaliyojiri bungeni leo kulikuwa na Mzozo kwenye kupitisha muswada wa sheria makatibu wa wizara wasiwe kwenye bodi mbalimbali na baadhi ya watendaji na Mgogoro ulikuwa kati ya Zito na waziri Ghasia zito akitaka na wabunge wasiingie kwenye bodi palikuwa patamu hata hivyo alishindwa kwa wingi wa wabunge wa CCm wanaoona ulaji utapungua na muswada kupitishwa kwa mbinde
 
KWELI BADO TUPO KIZANI. YANI WATU WANATARAJI KITU KUTOKA KWA JK

HAPO HAKUNA KITU NI POROJO TU, NA NDO MAANA KAKIMBILIA KWA WAZEE.....WATAPELEKWA KWA USAFIRI WA FEDHA ZA WALIPA KODI, WATAPEWA KAPOSHO....BAADAYE WATATOA KAHOTUBA KALIKO EDITIWA NA WANA-CCM WENZIE

Kwa mtu yeyote aliyekulia ndani ya ccm na kufanya kazi ccm basi ujue ni porojo tu na majungu

nenda ofisi ya ccm sasa hivi ukaone wanachofanya....wanafikiria uchaguzi, posho kwisha

TANZANIA WILL NEVER EVR DEVELOP UNDER CCM
 
Haya tena!!
msanii wetu kutoka maeneo ya chuo cha sanaa Bagamoyo amekuja na jipya!! kwa nini asingekuwa na hotuba ya wazee wa Dodoma halafu akawa na hotuba na wabunge hasa tukichukulia wakati huu ambao ni muhimu sana kwake na kwetu wananchi kutokana na nchi yetu kuwa katika hali tete kwa kuzingirwa na ufisadi huku serikali ikiwa na mateka wa ufisadi huo?

Mimi naona huyu jamaa anacho kifanya sasa ni ujanja ujanja tu sioni cha maaana anachokifanya! KWA NINI? anapuuza mambo muhimu katika wakati muhimu? kwani kanunuliwa bei gani na hawo mafisadi, nilitegemea angetoa hutuba yake Bungeni ilil tujue anamsimamo gani na mambo muhimu yanayoikabili nchi kama Kagoda, Epa na hili la mgodo wa mchuchuma. huyu jamaa kalogwa na nani?

mimi naona sasa ni wakati wetu watanzania kuikemea tabia hii mbaya ya Raisi kukwepa mambo pale anapo ona atakoselewa, kwa nini ikulu ijenge mazingira ya kutokusokosolewa?
 
Hawezi kwenda bungeni maana hakun hata moja alilofanya na hao wazee atawadanganya kwa kusema:
1. Swala la UFISADI liko mahakamani wahusika wamesha anza kushughulikia na kuwauliza huku akicheka si mnaona wenyewe wanapelekwa mahakamani ktk luninga kwenye magazeti mnasoma.

2. Swala la mauwaji ya alibino nao wahusika washapelekwa mahakamani.

3. Umeme tunajitahidi kadri ya uwezo wetu utasambazwa nchi zima hadi vijijini hadi kufikia mwisho wa mwaka huu sehemu kubwa itakamilika.

4. Barabara tunajitahidi kutafuta wafadhili ili tuweke lami nchi nzima hadi kufikia 2015 tutakuwa tumemaliza kwa kuanzia tumesha anza hii barabara kuu dom hadi mwanza- HATAWEZA KUZUNGUMZIA UPAUZI WA BARABARA YA SEGERA CHALINZE MANA ANAJUA NI AIBU KUIPANUA WAKATI SEHEMU NYINGINE HAZINA BARABARA ZA LAMI

5. Swala la uchumi nchi yetu haija hathirika - kama Mkulo alivyotoa pumba zake kuwa TZ haiwezi kkumbwa na misukosiko ya kuporomoka kwa uchumi.

6. MAJI tunajitahidi kuweka mabwawa ya maji ktk ile mikoa yenye vyanzo vikubwa vya maji ili kilimo cha umwagiliaji kishike kasi tusitegemee mvua.

7. Hali ya SIASA nchi yetu ni mfanoo wa kuigwa na CCM imezidi kuimarika angalia tulichokifanya GEITA na bado BIHARAMURO TUTASHINDA huku akicheka.

8. Akimaliza kucheka atawahadithia wazee safari zake wa Marekani jinsi alivyokutana na Obama na Steven Sigal.

Baada ya hapo muda umekwisha wazee wanapewa pilu na soda,bia na kurudishwa makwao bila kusahau wale wakereketwa zaidi kufungiwa vibahasha vyenye msimbazi.
 
Katika Bajeti nzima ni 29% tu ndiyo kwa maendeleo, ni pesa kidogo sana hasa ukilinganisha ukubwa wa nchi, idadi ya watu,umasikini uliopo, nishati na huduma za serikali. Asilimia 29 ni kama $2 bilioni. Katika bajeti nzima ina maana Bilioni $5.3 zinaenda katika kununua mashangingi, safari za nje, mafuta ya mashangingi, mishahara hewa, kununua viyoyozi vya wakubwa, marupurupu ya mawaziri 60 wasiojua kazi, semina na warsha.
Itakuwa vigumu sana nchi hii kwenda mbele.
Nataka kusema ule msemo wa NN lakini nitakuwa ninaiba hatimiliki.....
 
Last edited:
May be Geoff Lakini afanye lipi kurudisha imani tuliyokuwa nayo????

NgomaNzito,
ZITTO awaache WASAFI WAONGEE!that is how politicians do!
unajua viongozi wetu 'uroho' umewatawala.wanashindwa hata kuimitate what the 'developed-countries' politicians' are doing.

ZITTO has lost his TASTE!he is TASTELESS.
awaache WASAFI WAONGEE!
 
Katika Bajeti nzima ni 29% tu ndiyo kwa maendeleo, ni pesa kidogo sana hasa ukilinganisha ukubwa wa nchi, idadi ya watu,umasikini uliopo, nishati na huduma za serikali. Asilimia 29 ni kama $2 bilioni. Katika bajeti nzima ina maana Bilioni $5.3 zinaenda katika kununua mashangingi, safari za nje, mafuta ya mashangingi, mishahara hewa, kununua viyoyozi vya wakubwa, marupurupu ya mawaziri 60 wasiojua kazi, semina na warsha.
Nataka kusema ule msemo wa NN lakini nitakuwa ninaiba hatimiliki.....

hivi ni kweli tuna mawaziri 60 tanzania duu kama ni kweli hii ni hatari
 
naomba atakayepata hotuba yake aiweke hapa ili nami niisome
niko mbali kidogo na nyumbani.

NB: kwa nini asihutubie wazee????!!!!
unajua ukiwa unaongea na mzee wa miaka 85,hata namana ya kuongea lazima iendane na umri wa mzee tofaut na ukiwa unaongea na mtu mweny miaka 45 had 55, msomi nk....
nasubiri hicho atakachowaambia wazee, niko huku natafuta nauli....
 
tutegemee porojo na kupotezeana muda kufuatilia hotuba na kuacha kazi zetu!!!
 
amechelewa mpaka sasa dk 20 zimepita bado hajaanza
 
Back
Top Bottom