Kutoa ajira kwa waliofeli divisheni 4 tena kuanzia point 28 mpaka 31 ni kutuharibia jamii

Hicho ni kigezo kidogo sana chakumpima binadamu , je wote waliofeli hawajaweza kufanikisha chochote katika maisha yao!?
Je waliofaulu wote wamefanikiwa !?
Kufeli elimu haimaanishi your useless still unaweza ukafanya jambo. Wamepewa nafasi wacha waitumie.
 
Mleta mada ni KILAZA na pia huwezi jua position ambayo hao watu wanahitajika
 
yaani haya unayoyatetea ndiyo unajiona msomi wa ku quote plato????

elimu yetu ni shida tupu watu kukalili majina ya wanafalsafa wanaona wamejua.

narudia tena tangazo la ajira la serikali la kusema tunaajiri form 4 divisheni 4 pointi 28 mpaka 31 limetoka kwa kilaza anayetuharibia jamii. Tutajenga jamii yetu kwa kutengeneza ushindani ambao kila mwanajamii ataona anayejitahidi kusoma kwa bidii au kufanya kazi kwa bidii ndiye anayefanikiwa.

Lakini waliokalili sijui kuna makundi ya plato, kwamba plato alisema wanaopata sifuri ndiyo wenye akili hivyo akitaka kuajiri nafasi za umma anaita wenye sifuri hao siyo wasomi bali wamekalili tu
 
Mleta mada ni KILAZA na pia huwezi jua position ambayo hao watu wanahitajika
kilaza ni yule anayeamini kuna nafasi za vilaza hutakiwi kuweka watu wenye uelewa.

kama uliapata divisheni 3 na huna jambo lolote unalofanya, hukuendelea na lolote na mwingine akapata 4 ya 28 naye hana analolifanya yupi kilaza kati ya mimi ninayesema waite wote walinganishe na uchukue kwa kuchanganya na vigezo vingine na wewe unayekubali eti aitwe divisheni 4 tena pointi 28 mpaka 31 tu. huyu mwenye 2, three na four za mwanzoni hawana vigezo.

hizi ni hoja za watu waliofeli kulazimisha kuwa wao ni bora kuliko waliofaulu kuwashinda.
 
Hahahaaaaa, yani nimecheka sana.Ktk nchi ambazo watu wanaelewa maana ya jeshi huwa raia wake hawakimbilii kujiunga na jeshi.Bali hujiunga na jeshi baada ya kushawishiwa sana aidha kimaslahi au kipropaganda. Nashangaa Bongo watu wanapigana vikumbo kujiunga jeshini.
 
Form 4 akikuuliza wewe kama msomi umebuni nini zaidi yake ili upewe ajira halafu yeye anyimwe utamjibu nini? .
Wewe hio digrii yako ninamashaka nayo makubwa sana, unavyotetea usomi halafu unapingaba na kanuni walizoweka wasomi.
Wewe nani anakutambua mpaka umpinge plato,tafiti gani umefanta au falsafa zipi umeanzisha?
Kwa taarifa yako nchi na mifumo inaongozwa kwa mifumo waliotunga kina plato, carlmax nk kama utaendelea kubisha hio digrii unyang'anywe haina tija.
 
Wewe ni mbuzi labisa kabla ya hiyo elimu ya form 4 watu walikuwa hawafanyi kazi?

Ujinga unakusumbua kinachofanya kazi siyo elimu ni ubongo wa mtu ni wangapi wamfaulu na hawawezi kazi?

Ni wangapi hawajafaulu na wanaweza kazi?
 
Kwani sasa hivi hakuna digrii holder shule ya msingi, mbona mambo yapo vilevile.
Suala ubora wa elimu ni pana sana linahitaji kitabu kizima kulielezea.
Walimu wa upe wamewafundisha mpaka mmeota mapembe halafu mnawadharau.
 
Tanzania hatua tuliyo nayo haihitaji mtanzania mwenye akili. Yaani kama una akili wanakuua/kuku frustrate wasiokuwa na akili mpaka uchanganyikiwe au uozee kabulini. Ila ipo miaka itafika ambapo wenye akili watahitajika.
 
Acha kutetea vilaza mkuu. Kwa hiyo huyo division 4 anaweza fanyaa vizuri mambo ya kiteknolojia ukilinganisha na watu waliosoma mpaka degree level?

Ni kujaribu ku'justify" ujinga tu.
 
Acha kutetea vilaza mkuu. Kwa hiyo huyo division 4 anaweza fanyaa vizuri mambo ya kiteknolojia ukilinganisha na watu waliosoma mpaka degree level?

Ni kujaribu ku'justify" ujinga tu.
Ukute ulifundishwa na walimu waliopata division 4 za O- level lakini unavyojitutumua kuponda!
 
wewe ego kweli ni kiazi grade 1 na unafananana jina lako EGO

watu wameajiriwa kutokana na level zao za kielemu kama hiyo wizara ina anjiri watu wa division basi hao ndio wanaitajika kwenye hiyo kazi, endapo wangeitaji wstu wenye division 1,2, na 3 basi wangetangaza ajira kw hao wenye division hizo.

wewe hujui kwanini hiyo wizara ina hitaji watu wa division 4 unakuja na mawivu yako na husda kwanini eti kwanini wanaajiri division 4

cha kikuelesha ni kwamba hizo ajira zinawafit watu wa division 4 ya 28 ndio maana yakuitwa, kama zikitokea ajira za kuwafit nyie wa division 1 na nyie mtaitwa kwa wakati wenu

you are so EGO! mr ego
 
Sekta kama magereza, uhamiaji, polisi na jeshi walitakiwa waajiriwe watu wenye elimu kuanzia form 6, diploma, degree na kuendelea.
Lengo la kuwajiri waliofeli ni kuendelea kutumika kisiasa leo hii jeshi la polisi limekuwa la kisiasa.
Matumizi ya silaha na nguvu hayahitaji diploma wala divisheni one.
Kimsingi majeshini hakuhitaji maarifa ya vitabuni.

Kule utafundishwa mahalifa ya kupigana, kushambulia na kujihami.

Ndio maana utakuta makundi ya waasi pamoja na kuwa yanaundwa na watu waliokosa shule ambao ni kizazi cha watoto wa mitaani na hata umri wao unakutabmpaka miaka 7 tu lakini wanakuwa na uwezo mkubwa sana wa kupigana na kuyatoa kamasi majeshi rasmi ya serikali.

Kwa kifupi majeshini hakuhitaji mbwembwe za div one sijui degree ama masters.

Huku wanatakiwa std 7 maana hawa ndio wenye moyo na morali wa kupigania kile walichoelekezwa na wakubwa wao, hao wenye mavyeti na madigree wanafuata maslahi tu na vita ikianza wanaogopa kufa.

Kwa upande wangu naona wasomi ndio wameharibu majeshi maana wako kimaslahi zaidi kuliko utendaji.
 

Yani huyu kapataje English F?
 
Ndio wasomi wanahitajika ila wachache sana.
Matumizi ya nguvu jeshini huwezi kuyapitisha wakati hata sikumoja.

Utimamu wa mwilinndio nguzo ya jeshi. Pamoja na masayansi na matekinolojia bado majeshi makubwa duniani yanaajiri kwa wingi vijana kuanzia 18yrs na kuwapakia kwenye madege kwa ajili ya kwenda kupigana kwenye majabali na majangwa ya mashariki ya kati kwenye mazingira magumu sana.

Labda tuseme Jeshini kwa sasa wanahitajika vijana mafundi na wanasayansi wachache lia darasa la saba wanatakiwa jwa wingi zaidi maana hawa ndio wenye kazi ya kukesha nje na kulala macho wakati wenye digree walalala usingizi fofofo wakilindwa na hao std 7.

So wasomi si mhimili wa jeshi bali hawa std7 ambao ndio junior officers.

Wasomi wanataka waingie jeshini ili waendeshe maisha mazuri ila hawako tayari kukaa vikosi vya maporini kulala macho.
 
Hujui kitu we Mbuni, jeshi linahitaji wataohudunu kwenye vyeo vidogo kwa mda mrefu sasa ukimuweka bachelor holder unadhan ni kwa mda gani atahudumu kama Private?
 
Umeeleweka sana mkuu. Wasomi sio wafia nchi bali ni wapigadili tu jeshini hamna kitu mle sema tu mambo yameshakuwa magumu siku hizi.

Tangu mwanzo majeshi yalikiwa ni kazi za watoto wa familia maskini na watu wa mkoa wa mara.

Wakati ajira hazijawa shida na jeshi kuboreshwa kimaslahi na kimuundo watoto wa masikini tu ndio walikuwa na option pekee ya jeshi.
 
Kuna vyuo uchwara wanatangaza redioni/ runinga nafasi za masomo, uuguzi n.k. wanaweka ufaulu wa chini kabisa kama kigezo cha kujiunga nao. Unajiuliza ni mkunga au muuguzi wa aina gani atakayetoka hapo akutibu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…