FD,
Maneno yako ni mazito na machungu lakini ni ya ukweli.
Kitu kimoja natahadharisha though wale wanaofurahia umaarufu wa ccm vijijini ni hili. Hali za maisha ya watu vijijini zinadumaa na hiyo si sign nzuri. Watu wa vijijini wakiendelea kuwa nyuma hivi na kuwa marginalized like this matokeo yake ni mabaya.
Angalia vita vya ndani vilivyotokea kwa majirani zetu Rwanda, Congo, Burundi, Uganda, nk kisha ujibu maswali haya. Hivi hao rebels walianzia mijini au vijijini? Ilikuwaje rahisi kwa rebel leaders kupata wafuasi?
Jibu rahisi ni kuwa, makundi yote hayo yalijengeka vijijini ambapo watu wengi wamekwisha kata tamaa. Kama ccm itaendelea kushinda kwa kutumia nguvu ya watu walioko vijijini at the same time ikitumia mabilioni kujenga majengo ya BoT huku hao wapiga kura wake wakifa kwa njaa na magonjwa yanayotibiwa, basi ccm itabidi ijilaumu yenyewe siku hao wajinga wa vijijini wakichoka na maisha.
hili pia litauma masikioni mwa wengi ila ni ukweli.