Kutesa Kwa Zamu- Ikulu

Kutesa Kwa Zamu- Ikulu

Huruma,

Karibu, cha kwanza umeambiwa. Husitumie computa ya kazini kwako. Pili hizo documents hasa PDF zinz matatizo, ukienda kwenye properties ina record jina na time na computer ya last user aliye i save. Ushauri ni kuwa tumia mobile (laptop) computer au ya home. Komputer ya home sio rahisi kujulikana.

Ukitaka kutuma sensitive documents tumia internet cafe! hata ya home ni nzuri tu maana sio rahisi TCCL nzima au Zantel kukutrace kirahisi. Ingawa inawezekana.

Kwa upande wa JF nina uhakika siri itatunzwa milele! hofu ondoa.

Karibu sana tumkome nyeni giladi!

Amsha watanzania na wadanganyika waliokwisha danganyika!

Karibu mkuu, kuna private email (message) unaweza kuuliza watu vitu mbalimbali ya kukusaidia.
 
Nina maana utume PM ili upate jinsi ya kutuma docs bila tatizo (kuwa traced back)
 
Data Protection Act 1984,haihusiana na mambo yanayohusu Forum,Kimsingi fanya ufanyalo ,unalindwa na ibara ya 22 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Check ID yako Vizuri maana ni rahisi sana kwa mtu kutrace kwa kuscan document.Make sure Document zako zote ziko katika PDF then ndio uziweke hapa

Hivyo, bila kujali paragraph iliyotangulia, fuata hii bolded. Umeshaendesha pikipiki Dar? Sasa ukifuata haki yako ya barabarani, utakata rufaa ukiwa kaburini🙂
 
eheee, kazi ipo. Huruma hapa ndio makao makuu ya kuwakoma gladi mafisadi. Fuata ushauri wa FD halfu lete vitu.
 
Vipi tena mbona umepotea mheshimiwa, au ndio inabidi ukitoka kazini upitie cafe? Hii thread very soon itakuwa hot, lakini kama utarudi na vitu. So far ulichosema kila mtu anaweza kusema!
 
Huruma

trust nobody..............duniani na hata mwezini!! karibu JF

najua wewe ni mtu makini...........pia unafahamu unachofanya...............hukukurupuka tu na kuandika ulichoandika................so wee mwaga mavitu tu mzee
 
tunakoelekea mie naamini humu hata Mzee Mkapa atajisajili ili ajibu tuhuma za ufisadi,Nchimbi yumo humu pamoja Ritta Mlaki!
 
Kikwete,Lowassa na E.Hosea- $ BoT 2005 wote lao moja watanzania ndiyo wanaoumia ikulu haina heshime kabisa ni business center JK na Lowassa 75% wanao zungumza nao ni wafanyabiashara, iliyo baki ni wasomi na walalahoi. kuna kauli zinatika kwenye famili za viongozi wanasema kutesa kwa zamu. maana yake ni nini?

Baada wao kuchukua pesa nyingi Benki kuu za kusaidia kampeni ya CCM,Rostam Azizz alikwenda London kuwa na maongezi na Hosea na kumuofa hiyo nafasi JK alimtuma kwasababu mambo nyeti JK atumii simu kabisa kutokana na kurekodiwa maongezi yake JK anawatu wake special wakuwatuma kupeleka ujumbe, au akumtumia watu wasiyofanya kazi serikalini kupeleka ujumbe,

timu iliyo pangwa katika uongozi wa serikali ya awamu ya nne wanajuwana wote akuna atakaye weza kumsemea mwezake, ndiyo sababu kila mtu ananguvu kwenye nafasi aliyo nayo anaweza kufanya anachotaka bila kuongopa nini kitatokea.

wafanyabiasha wengi wanaingia ikulu usiku na mchana kwa kishindo wengine wanaingizwa na magari ya ikulu bila kupita kwenye sehemu ya kuchekiwa, kama watanzania wangelipata kujua haya yanayotendeka hapa ikulu basi wangeliamua waishi maisha ya namna gani, hakuna maisha bora kwa watanzania, hii ni ndoto.

Hosea alipewa nafasi hii kwasababu yeye ndiyo mtoa taarifa kwa viongozo kuhusu ufisadi, viongozi wote wanajijua wako sawa kwasababu akuna mtu wakuwageuka.

kuwa na serikali yenye matatizo kama hii inatokana na uwezo mdogo wa Kufiki wa Rais na washauri wake jinsi ulivyo.

kuna list ya watu waliyo pewa nafasi za uongozi kwasababu walikuwa wakotehari kumwaga mboga kwa wale waliochafuliwa kwenye kampeni,waliousika na wizi wa kura,walio chukua pesa chafu zikatumika kwenye kampeni, watu wajinga wajinga tu.

hapa kazini wafanyakazi wengi na makundi mengi kila aliye karibu na muheshimiwa basi na sauti yake inakuwa juu,

Samahani kwa mtoa hoja nimekuwa msomaji mzuri hapa ofisini kwangu watu hafanyikazi asubui kabla hawajasoma hapa hii Jambo Forum imekuwa bora kuliko magazeti.

ninaoba nijiunge na nyiye hapa ni wape maoni yangu kama mtaniakikishia usalama wa maisha yangu na familia yangu na kaumri pia kamesogea nimechoka na kunyenyekea watoto wasiyokuwa nanizamu kwa wazazi wao kwa sababu ya madaraka mimi siyo mwana siasa mimi nimesoma ninaelemu nzuri ndiyo sababu wakanipa kazi nipo kwenye nafasi kubwa na mengi machafu ninayo mezani kwangu, jamani simnajua nikiandika kisomi itakuwaje nyiye mnachotaka ni ujumbe ufike ''usiangalie kiswahili changu''nitatoa na ushaidi wa copy kama mtahitaji.

ninaomba samahani niliingia bila kukaribishwa kama mwanaJF MTANZANIA kunikumbusha asante nina kushukuru sasa ninaomba kutoa hoja

Huruma

Karibu mzee Huruma JF,

Fanya kile moyo wako utakachokutuma kufanya na fanya mema kwa manufaa ya nchi yako. Kuna watu wengi tu kama wewe ambao tayari wamehatarisha maisha yaona vyeo vyako huko Tanzania na hapa ili kuokoa taifa letu.

Karibu sana na fanya chochote kile moyo wako utakutuma kufanya hapa JF ambapo siri zote za serikali zinapitia hapa kisha kwenda kwenye magazeti Tanzania directly and indirectly.
 
Lakini sasa naona jamaa mwenyewe alikuwa anapiga mkwara maana naona kaingia mitini kabisa. Nilitegemea angeibukia kwenye cafe kama alivyoshauriwa na FD. Anyway ngoja tumpe mpaka kesho labda atakuwa ameibuka tena.
 
Lakini sasa naona jamaa mwenyewe alikuwa anapiga mkwara maana naona kaingia mitini kabisa. Nilitegemea angeibukia kwenye cafe kama alivyoshauriwa na FD. Anyway ngoja tumpe mpaka kesho labda atakuwa ameibuka tena.

Kitila,

So far inaonekana anaendelea na mawasiliano ya chini kwa chini na some memberz hapa ili kuamua kama atumie FedEx, DHL, au posta na simu!

Wewe nawa mikono ujiandae kula vya JF ambavyo kama Mwanakijiji anavyopenda kusema huwa vinaletwa vikiwa moto kabisaaa kabla havijapelekwa mezani kuliwa
 
Kitila,

We acha tu, mimi mwenyewe namsubiri alete vitu. Aisee niliibuka hapo UDASA jumapili kwa ajili ya ugali wa muhogo na nyma ya swala, sikupata nyama ya swala lakini ugali wa muhogo na samaki aina ya changu ilikuwa bomba sana! Ilikuwa lunch time. Nitakutafuta siku ingine.

Samahani wengine, kwenda kwenye PM saa nyingine taabu kidogo!
 
Kitila,

So far inaonekana anaendelea na mawasiliano ya chini kwa chini na some memberz hapa ili kuamua kama atumie FedEx, DHL, au posta na simu!

Wewe nawa mikono ujiandae kula vya JF ambavyo kama Mwanakijiji anavyopenda kusema huwa vinaletwa vikiwa moto kabisaaa kabla havijapelekwa mezani kuliwa

Kwi kwi kwi kwiii We Mwafrika hujatulia kabisaaa! itabidi unilipe gharama ya matibabu kwa kunivunja mbavu!
 
Kwi kwi kwi kwiii We Mwafrika hujatulia kabisaaa! itabidi unilipe gharama ya matibabu kwa kunivunja mbavu!

Pole sana FD kwa maumivu,

nipe account namba ya daktari wako ili nitume pesa kwake moja kwa moja ili usijetumia pesa ya matibabu kwa mambo mengine bure kwi kwi kwi
 
Nitakupa, ngoja niwasiliane na mwanasheria wangu, kama mimi sistahili kupata kitu hapo...

Huruma anapanga mafaili, mpeni muda kidogo..
 
Huruma,

Karibu, cha kwanza umeambiwa. Husitumie computa ya kazini kwako. Pili hizo documents hasa PDF zinz matatizo, ukienda kwenye properties ina record jina na time na computer ya last user aliye i save. Ushauri ni kuwa tumia mobile (laptop) computer au ya home. Komputer ya home sio rahisi kujulikana.

Ukitaka kutuma sensitive documents tumia internet cafe! hata ya home ni nzuri tu maana sio rahisi TCCL nzima au Zantel kukutrace kirahisi
.
.

Bwana Huruma karibu sana.
Nashukuru wana JF wameshakupa tahadhari zote na niliyotaka kukueleza tu naona nimeyakuoti hapo juu.Wewe kama kweli unatoka hapo jikoni, basi kwa sasa hata hilo jina halikufai,maana kama wanasoma watakuwa tayari wanakujua endapo unatumia PC za hapo kazini.Kwa ushauri wangu tafuta mtu unaye mwamini awe anatutumia hiyo michapo.Ukifanya wewe watakufuatilia kama mkia.
 
Huruma anapanga mafaili, mpeni muda kidogo..
__________________
FD

Anapanga mafaili, ama anafuatilia kupata reaction ya "Chambo" alicholishia?

Kwa mfano akitokea mtu akasema, "Hata mimi sijapendezwa kabisa na yule .... alivyopewa cheo eti kwa sababu siku ile pale ..... tulikwenda naye kuchukua fedha pale kwa ..... lakini mwenzangu kapewa ujiko, au ...... alipopewa ubalozi eti kwa sababu tu alisema asipopelekwa nchi ile, atamwaga siri zote... au nanihii ambaye pale ofisini mimi ndiye namfanyia kazi zake zote, lakini mwenzangu kaula nimebaki peke yangu".... hapo kaka Huruma atakua amefanikiwa kwa kuwajua wale wote wasaliti ambao wako ndani ya jumba jeupe la magogoni ama maeneo yanayofanana na hayo, ambao wanatoa taarifa na kuziingiza humu JF ama kule katika magazeti tukutu kama MWANAHALISI, THISDAY, TANZANIA DAIMA NA SASA RAIA MWEMA.

Lakini kama kaka HURUMA kweli ana huruma na watoto na wajukuu wa taifa hili na kama kweli yeye ni Mtanzania na raia mwema, namshauri asiogope wala kukata tamaa, na hata ikitokea wakamjua hawawezi kumuua sana sana watamuwahi na yeye kupelekwa nje kama wengine walivyofanyiwa..

ENDELEZA MAPAMBANO KAKA
 
Kazi kwenu wana JF ambao munafanya kazi na Huruma, muwe makini kama ambavyo nayeye Huruma anapaswa kuwa makini,,, hakuna sababu ya wote kufahamiana, cha muhimu ni maneno kwa MASLAHI NA USALAMA WA TAIFA NA VIZAZI VIJAVYO, SI MASLAHI NA USALAMA WA WACHACHE AMBAO WENGI NI MAFISADI
 
Nitakupa, ngoja niwasiliane na mwanasheria wangu, kama mimi sistahili kupata kitu hapo...

Huruma anapanga mafaili, mpeni muda kidogo..

FD,

Nakupa majina mawili tu ya Lawyers nitakaowakubali - Lisu au Mvungi wa Mlimani ambao naamini kuwa watakuwa fair kwangu pia. Ukitumia wengine kama fisadi Mkono itabidi nikate rufaa kabla kesi haijasikilizwa kwi kwi kwi..

BTW, I dont why lakini from no-where ninaamini kuwa Huruma ni real deal kwa hiyo hapa nimeshawasha oven kuandaa maakuli ya JF
 
NIMEONA "Nyoka" kama wawili humu ndani wananusa nusa....
 
Back
Top Bottom