Wapendwa ni matumaini yangu mu wazima na mko vizuri katika majukumu yenu:
Leo ninaomba kushare nanyi jambo ambalo limekua likinitatiza kwa muda sasa. Ninatambua kila mmoja wetu ana historia yake ya kimapenzi na wengi tumetendwa na wale ambao tuliwekeza mioyo yetu kwao kwa kuwaamini kwamba wataiendeleza furaha yetu, ila kwasababu mbalimbali au kwa bahati mbaya wengi hatukuweza kufikia matarajio yetu juu ya hao wenzetu....
Binafsi nilikua katika mahusiano na mtu ambae nilimpenda mno narudia tena nilimpenda tena mno. Na ndie mwanaume wangu wa kwanza ku........
Nae kwa upande wake alionyesha uaminifu na moyo wakujali,maneno yote mazuri yenye matumaini mtoto wa kike niliambiwa,Kifupi tulipanga uhusiano wetu uzae ndoa.
Ilifika hatua mwezi wa sita mwaka jana akaja Arusha kwalengo la kujitambulisha nyumbani kwetu. Lakini gafla katika hali ambayo sikuitarajia akabadilisha maamuzi yake akanipa visingizio. Baada ya muda mfupi kabla ya yeye kurejea kwenye makazi yake,nikamfumania akiwa na rafiki yangu wa karibu,rafiki niliye mchukulia kama ndugu yangu na kushare nae baadhi ya mambo.
Waliosalitiwa bila shaka wanaelewa uzito wa maumivu hayo. Ikabidi niwe mpole,na kuwaambia waendelee mbele,siku zilivosonga yule binti akaanza mambo ya dharau kwangu ila namshkuru Mungu nilipata moyo wa kumsamehe na kupuuza dharau zake. Ilipofika mwezi wa 9 yule binti aliacha kazi kwa shari na kurudi kwao.
Sasa kilichonifanya nije hapa mbele yenu leo,nikwamba yule mwanaume anataka kurudi kwangu na mimi moyo wangu unakua mzito kumrudia,nimetokea kumchukia.
Jambo linalonisumbua zaidi kila ninapoanza mahusiano mapya hua nashindwa kuendlea mbele,hofu ya kwamba huyu atanifanyia kama yule inanijia mara kwa mara na matokeo yake nakua sababu ya kuvunjika uhusiano huo.
Wapendwa nifanye nini kukabiliana na hali hii ya pili? Ninatamani sana hali hii iniondoke. Karibu kwa mchango wako kimawazo.
Kwenye makosa ya kiuandishi mnisamehe mana natumia cm.
Kwanza Pole kwa yaliyokukuta
2.Namna moja au nyingine unaweza ukawa unajilaumu kwa maaumuzi uliyofanya yakumpa papu.....
3.Unapoweka chuki moyoni kwa aliye kutenda kwa nia ya kumsahau na kumtoa moyoni hutatui tatizo ila unaongeza mlango wa shetani kukuingia kwa kutumia chuki na kuwachukia hata wasio kua na tabia kama za aliye kutenda
4.Ulivosamehe/ulivo wasamehe umefanya jambo lakiushujaa ambalo limefunga mlango mmoja wa chuki na mlango mwingine uliufungua kwa point 4.
5.siku zote UBAYA HUWA HAULIPWI KWA UBAYA/CHUKI HAILIPWI KWA CHUKI ingawa ni ngumu kuamini na kuliweka katika matendo
6.Sifa kubwa ya UPENDO/LOVE ni uvumilivu na kusitiriana
7.Kikawaida na tunavoamini na kutokana na xperience 1st love huwa ni VERY STRONG no matter umefail/win kupata kile mlichokitaamia.Matarajio yanapofaeli wengi hushindwa kujizuia ndo pale tunapoanza kutafuta kinga na dawa ya kupoza mioyo yetu kama vile kutafuta mwingine mpenzi/kunywa pombe/sigara/bangi/kulipiza kisasi
KOSA LAKO
Hukufanya uchunguzi wa kutosha wa kumjua mwenzi wako hata kwa 3% na mapungufu yake na mazuri yake ili vikusaidie mbeleni kwa ulinzi wako binafsi katika kuhakikisha kile unachokiona mbele je kitakamilishwa na huyo mwenzi wako au la
USHAURI
1.Jipe mda wa kutulia usithubutu kutoa mwili wako kwa mwingine
2.Ili kusahau tukio lililokuumiza tafuta marafiki wakike/wakiume ambao hutakua nao katika mahusiano kwa kupiga stori za maisha hata kama zitakua za mahusiano waweza jielezea mwenyewe kwa mifano hii itasaidia kukupunguzia msongo wa mawazo
3.Ukiwa na marafiki wa kiume usijaribu kuwakubalia mara moja(kuingia katika mahusiano) jaribu kuwaweka kama marafiki huku ukiwachunguza na kujipima kama mnaendana na wanafaa kuwa nae katika mahusiano
4.Sala kwa Mungu wako itasaidia sada KUYASHINDA MAMBO AMBAYO YAMESHINDIKANA KWA MAWAZO YANGU HAPO JUU
5.Fanya mazoezi na Kusanyika na watu wenye mawazo ya juu(Uwezo mkubwa wa kufikiria na kushauri) au waliokuzidi ili wakushauri kwa ilo(wanandoa watakusaidia zaidi)
6.Kama unampenda na unafikiria kumpa nafasi Jaribu kupunguza ukaribu uliouweka wakati wa nyuma mkiwa katika mahusiano,kama mtapanga kukutana mkutane mahali pa wazi ili msiingie au usiingie majaribuni-Huku ukiwa unamchunguza kwa nia yakujilidhisha kama atakufaa kuwa mume wako,na usiwe mtu wa kumtafuta yeye ndo akutafute
NOTE;
VANITY UPON VANITY IS VANITY :smile-big: