Kushukuru kwa Chakula au Kwa Mapishi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kushukuru kwa Chakula au Kwa Mapishi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, May 31, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wiki ya jana tulijiuliza swali zima la ni kipi kinatakiwa hasa kwenye suala la kuosha vyombo baada ya kula na ikaonekana watu wengi wamekubaliana kuwa vyombo vinatakiwa kuoshwa kwa pamoja lakini kama mmoja anajitolea basi si vibaya na si jambo baya. Ilikuwa ni elimu tosha kwa watu wa majumbani na wenzi wao kujifunza umuhimu wa kuangalia na kutunza vyombo wanavyotumia. Shukrani.

  Leo hata hivyo, mjadala wa leo unahusiana na jambo la kawaida sana lakini ambalo pia nimewahi likisababisha mgogoro wa aina yake. Vijana walikuwa wanajadiliana huku mmoja akionesha masikitiko yake kuwa mke wake kamnunia baada ya "kumshukuru" baada ya chakula. Kijana alisema "Nilimuambie mke wangu 'asante kwa chakula'" na yule mwanamke akaja juu. Kwamba, chakula ni haki yake, na ni yeye analeta vikapikwa hapo nyumbani kwanini ashukuru?

  Mke wake akaja juu na kusema anayetakiwa kushukuriwa namna hiyo ni "mama ntilie" kwani wao huleta vitu vyote wao wenyewe na "kukuuzia" kwa hiyo kuwashukuru kwa chakula ni jambo muhimu sana kama unataka kuendelea kula kwa mama ntilie yule yule, lakini pia kuwa "mama ntilie" wao hawajali hata hiyo asante yako wao wanachotaka ni pochi tu. Kumbe mwanamke alikuwa offended kushukuliwa kwa "chakula" kwani hakuwa anauza na ni haki ya baba mwenye nyumba.

  Kijana mwingine alipigwa na butwaa na kuanza kumcheka mwenzie huku akimshangaa:

  "Yaani wewe unamshukuru mke wako kwa chakula" alihoji kwa kebehi.
  "Sasa jamani ndivyo nilivyolelewa" alijibu kijana wa kwanza.
  "Wenzio ndani ya nyumba zao hawashukuru kwa chakula ni mwiko" alisema jamaa kwa msisitizo.
  "Really"? alihoji yule mwingine na kuongezea "sasa nifanyeje?"
  "Unatakiwa kushukuru kwa mapishi!" alisema na kuweka kituo.
  "mapishi!?" alihamaki

  Ndipo akaendelea kumuelezea kwa kirefu kuwa vyakula vinaweza kutumia vitu vile vile karibu sehemu zote lakini ufundi wa mpishi ndio unatofautisha utamu wa chakula. Sasa usipomshukuru mke wako kwa mapishi yake mazuri maana yake chakula alichokupatia hakina tofauti na vyakula vingine. Jamaa akapewa elimu kuwa wapishi wote hutofautiana hata kama wanatumia jiko lile lile!

  Ndio akaeleza ukiangalia sana kama mtu anapewa mapishi mazuri kwa 'mama ntilie' basi hata nyumbani atakula kwa kumridhisha 'mamii tu' lakini baadaye ataenda kupata bata wake wa kukaanga huko au samaki wa kukaanga! Na wakati mwingine mtu huufungia safari wali wa biriani maili nyingi kadhaa kwani mapishi yake huenda na mambo mengi.

  Jamaa alielewa na alirudi nyumbani na kumuomba radhi mke wake kwa kumfanya kama mama Ntilie. Walipomaliza kula usiku ule jamaa alijilamba na vidole na kuanza kumwaga sifa za mapishi na utamu wa karibu kila kiungo. Mke wake alifurahi na uso uling'aa kama mbalamwezi na tabasamu kama aliyeona hazina ya dhahabu.

  Jamaa alijua amemfurahisha mke kweli kwa kumshukuru kwa mapishi; kabla hajakaa sawa mamii akamuuliza "unataka desert?"
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  [​IMG]....kokolikoooooo! haya tena, Chakula na Mapishi.
  eti,..."Unataka Dessert?" eh hehhe!

  "Asante kwa chakula!" hujibiwa "Ahsante kwa kushukuru!"...hiyo asante kwa mapishi mnh?! haya.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  duh...........hii sikimbiliii ku comment kama ile....lol
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Akili kumkichwa...chakula hicho hicho waweza pata popote ila mapishi ndo ya kipekee!Hivyo basi asante kwa ‘chakula KITAMU...KIZURI...CHA KIPEKEE‘ is more appropriate!
   
 5. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  dahhh Asante
  lakini naona itakuwa ni vema
  "kushukuru kwa chakula na mapishi"
   
 6. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,167
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Sasa nimeelewa kuwa hata wale wanaotuambia kuwa utazunguka mabucha nyama ni ile ile!kuna ulakini hapo,yaweza kuwa ni ile ile kumbe wamesahau kuna jinsi ya Kuipika nayo ni mapishi yake!kweli umelonga kaka!
   
 7. mchakavumlasana

  mchakavumlasana JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  hahahahahah .....
  kweli asante kwa "mapishi?"
  maana samaki atakavyopikwa na HUYU tofauti na atakavyopikwa na YULE...
  kila mmoja ana ufundi wake....
  kila mmoja ana utaalamu wake...
  kila mmoja ana vikorombwezo vyake.....
  kila mmoja ana utundu wake....


  mmmmh:thinking:
   
 8. Taz

  Taz JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 305
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ni kushkuru kwa chakula kwanza, then unashukuru kwa mapishi. kupewa chakula tu ni wema ulioje?! kama pia mapishi yamekamilika basi ni additional reason ya kushukuru.
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  Essence ya usemi huo ni kuwa nyama haipikiwi buchani. Ukiileta nyumbani ukaipikia kuni zinazotoa moshi, usiiweke chumvi, thomu wala tangawizi usitegemee utamu.

   
 10. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  Mzee unazeeka vibaya sasa. Kushukuru kwa mapishi unatakiwa ufanye on the course of eating. Huku unampamba mpishi vyema. Ukishakula ukashiba unashukuru kwa chakula. Manake angeweza kufanya upishi hadi kikageuka sumu na si chakula atii!
   
 11. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Sio vibaya kushukuru kwa vyote yaani chakula na mapishi, kila kimoja kina umuhimu wake
   
 12. muuza ubuyu

  muuza ubuyu JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 2,639
  Likes Received: 745
  Trophy Points: 280
  du, nami kuanzia leo jioni ntaanza kushukuru kwa 'mapishi' nione tofauti yake na kushukuru kwa 'chakula'
  aiseeeee kunamambo!!!
   
 13. Taz

  Taz JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 305
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wanawake nao wanashukuru kwa mapishi?
   
Loading...