Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Hivi karibuni kumetokea kuongezeka kwa vitendo vya kihalifu hasa katika jiji la Dar es Salaam.
Leo hii kwenye taarifa ya habari imetangazwa kuwa wahalifu hawa wameua mtu mmoja eneo la Kawe.
Haya yanatokea kukiwa kumemalizika kikao cha wakuu wa polisi ambapo Rais Samia aliwaeleza mambo mengi sana polisi ikiwemo kuwaachia watu endapo upelelezi haujakamilika.
Leo kwa maslahi mapana ya nchi yangu napenda kumshauri Rais wangu mpendwa Samia kuwa, tunajua anapenda sana haki, anataka haki itendeke, ila kwenye kushughulikia wahalifu na uhalifu ni vizuri aviachie vyombo vyetu kufanya kazi ambayo wamekuwa wanaifanya kila siku katika kushughulikia wahalifu.
Kwa Tanzania yetu kuna watu bila kuwa ndani hawawezi kuacha uhalifu na wanawekwaga ndani kwa sababu maalum ikiwemo kuhakikisha kwenye jamii yetu kunakuwa na amani na utulivu. Ukitaka kuwaweka ndani ukiwa na ushahidi hutapata huo ushahidi kwa namna wanavyofanya matukio yao na kwa namna nchi yetu ilivyo nyuma kiteknolojia. Wenzetu wako vizuri kiteknolojia ikiwemo kuwa na kamera za mitaani na teknolojia ya DNA na database za wanachi wote ndo mana likitokea tukio upelelezi unakamilika haraka.
Nakuomba Rais wangu mpendwa, waachie polisi wetu wafanye kazi yao dhidi ya hawa wahalifu kulingana na mazingira yetu yalivyo. Kila nchi ina mazingira yake, Sio kwamba Marekani alishindwa kutawala Afghanistan ila kwa jinsi Afghanistan ilivyo nchi haiwezi kwenda bila utawala wa manguvu na ndo mana Leo Taliban karudi kutawala Afghanistan tena kwa baraka za Mmarekani yuleyule aliwafurusha pale mwanzoni