Serikali Kujenga Vituo vya Polisi Kupunguza Vitendo vya Uhalifu Kata ya Machame Mashariki

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Kutokana na kuripotiwa kwa matukio mengi ya uhalifu ambayo yamekuwa yakisababishwa na wananchi wenyewe kwa wenyewe Serikali imedhamiria kujenga vituo vya polisi kwaajili ya kupunguza matukio ya uhalifu ambayo yamekuwa yakiripotiwa ya mara kwa mara.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Khamis Hamza Chilo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Saashisha Elinikyo Mafuwe alilotaka kujua mpango wa Serikali kufuatia matukio ya uhalifu yaliyoripotiwa na kukithiri katika Katika Kata ya Machame Mashariki alilouliza kuwa “Je? Serikali inampango gani wa kujenga kituo cha polisi katika eneo hilo?” Mhe. Saashisha Mafuwe

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Chilo amekiri uwepo wa matukio ya uhalifu kuripotiwa ambayo yanafanywa na wananchi katika maeneo husika ambapo miongoni mwa jitihada za kudhibiti matukio hayo ikiwa ni pamoja na kununua magari kwaajili ya kufanya doria

"Ni kweli kwamba kumekuwa kukitipotiwa baadhi ya matukio ambayo mengi yao yanafanywa na wananchi wenyewe kwa wenyewe Serikali haijalala ipo makini kuhakikisha kwamba tupo makini dhidi ya vitendo vya uhalifu ikiwemo kuhakikisha kwamba tunatafuta magari kwaajili ya kufanya doria na ukaguzi wa mara kwa mara na kujenga vituo vya polisi kwaajili ya wananchi kwenda kupeleka changamoto zao na kuweza kutatuliwa kwa haraka" - Mhe. Khamis Hamza Chilo

yyy.jpg
ll.jpg
 
Back
Top Bottom