Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA?

  • Zitto Z. Kabwe

    Votes: 180 15.3%
  • Wilbrod P. Slaa

    Votes: 996 84.7%

  • Total voters
    1,176
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Ni kumkosea Adabu na heshima Dr Slaa kumlinganisha na Zitto, ningewaelewa kidogo kama Zitto angeshindanishwa na mtu wa level yake kama Mnyika. Dr Slaa ni habari nyingine kabisa.

Ni kweli mkuu lakini itasaidia kukata kilimilimi cha wafuasi wa Magamba hapa jamvini.Na ndiyo maana vibaraka nguli wa Magamba hapa JF wanachungulia tu hii thread na kukimbia.
 
Wote wanafaa hasa kwa kumridhi JK lakini Dr. Slaa anafaa zaidi kwa sababu ya exposure aliyonayo, si kijana kifikra lakini anatambua mahitaji ya makundi yote ndani ya jamii lakini Dr. Slaa ni mtu anayetambua namna ya kutunza image yake ndani ya jamii kuliko Zitto ambaye amekubali kuacha maswali mengi kwa watanzania huku akijiaminisha kuwa wabaya wake hawamwezi. Kujiamini huku kwa Zitto kupita kiasi ndiyo doa lake kubwa.
 
Kura ya maoni kati ya ZITTO KABWE na WILIBROD SLAA inayoendelea hapa JF imeashiria jinsi matokeo ya mwisho yatakavyokuwa. Sasa je! Nani anafaa awe Waziri Mkuu wa Tanzania?.
Pendekezo lako litamrahisishia rais kufanya uteuzi sahihi hapo 2015. Taja jina moja kisha toa sababu zaidi ya moja ambazo zitatumika kama kigezo cha kumpata Waziri mkuu bora wa nchi hii.
 
Jamani wanachama wapenzi wa chadema na wapenda mabadiliko watanzania wenzangu, tusijidanganye kuwa 2015 CDM itaingia madarakani kirahisi muda huu badala ya kuanza kupiga ramli ya urais au waziri mkuu tuanze kuangalia mianya yote ambayo ccm wanatumia kuiba kura na kushinda tuizibe kunako mapema, pia tuanze kufikiria mambo ambayo tutaingiza kwenye ilani yetu ya 2015 ili kuvutia wapiga kura na kubwa zaidi tuelekeze elimu ya uraia vijijini tuunge mkono kwa vitendo m4c CCM sio rahisi kiasi hicho lazima kujiandaa kila mtu anajua kilichotokea 2010 sasa kuanza kujiaminiha ushindi 2015 ni kujiweka hatarini ccm ipo kama nyoka ukitaka kumuua lazima ukate kichwa kabisa!!
 
Mimi siwezi kutoa maoni.....kumuweka dr.slaa na zitto kishoka nadhani ni dharau sana......zitto hajafika hata robo ya dr.slaa kwa hiyo kura ya maoni ni dharau kwa kiongozi mwenye heshima km dr.slaa.....sijui labda zitto umshindanishe na shibuda ingefaa kwani hata kwa mnyika au lema haingii

tuacheni dharau kwa rais wetu
Nakunaliana nawewe kuwa Zito hajafikia wala pengine hatafika kushindana na Dr. Slaa ila sikubaliani na wewe katika ulinganifu wa pili. Zito kwa tabia na hulka zake anaangukia kwenye kundi la kina Lema. Lema ni size yale zito kabisaaaa!!!!. Mnyika yuko dunia nyingine ya mtu anayeonekana kuwa na sifa hasa za kiongozi.
Tutofautishe vitu viwili. Kuna wapiganaji lakini pia kuna viongozi. Zito, Lema, Wenje, Kafulila, Vincent Nyerere, Silinde, Mkosamali, Mbatia, sugu na wengine wanaolekea kwenye hulka zao wako kwenye kundi la wapiganaji. Dr. Slaa, Prof. Lipumba, John Mnyika, Maalim Seif na Tundu Lisu wako kwenye kundi la viongozi. Mnaweza kuwaongeza wengine au kuwapunguza kwenye makundi haya mawili.
Kitu kimoja tu tujue tunahitaji haya makundi yote mawiliakatika mustakabali wa nchi yetu. Tutakuwa na heri pale tukimpata mtu mwenye sifa ya kiongozi kuwa kiongozi wetu. Tukimpata mpiganaji inategemea hali ya siasa ikoje lakini ikiwa kuna mvutano wa kisiasa wapiganaji wanaweza kuyumbisha nchi na mara nyingi hawana busara za kutosha kutuliza hali inayovurugika kisiasa.
 
Hivi na ninyi mnahangaikia kufikiria nani mkali kati ya zitto na slaa? Mbona jibu liko wazi hapo? au mnaangalia anayejitangazia kuwa lazima agombee? Kwanza mimi naona mtu kung'ang'ania kugombea kwa sasa sio kabisa, suala ni kusema atachukuwa fomu ya kumtafuta mgombea wa urais na sio kusema lazima nigombee, unless otherwise waruhusiwe wagombea binafsi!
 
Kweli hili jamvi lina mambo.. nimejaribu kupitia posts za wachangiaji wengi. Mhh inavyoonekana wasiokubaliana na Zitto wanakosa hata uvumilivu wa kumpa credit anazostahili.. hakika kuna credit nyingi anazostahili kupewa.

Zitto ni kati ya vijana wachache wasomi, wenye uwezo wa kujenga hoja, kufanya tafiti na kusimamia anachokiamini, na kupitia sifa hizo amejikuta baadhi ya makundi ya vijana hayamuamini na na pia haya mkubali, ila vijana hao wanasahau kwamba penye mvutano wa kifikra kama mawazo huru yanazingatiwa husaidia kutufikisha kwenye mafanikio.

Ni ajabu wengi humu hudiriki kusema Zitto hastahili kulinganishwa na Mnyika, Lema nk, lakini ukiichambua cdm utagundua kwamba Zitto anahistoria ndefu yaliyokiletea chama mafanikio.. yawezekana kabisa asilingane na hao anaolinganishwa nao. Tuweke ushabiki pembeni tujadili hoja, kisiasa kuna mengi ya kupitia na yeye kwa sasa kuna mambo kadhaa yanamgharimu (kama la kutangaza kuwania urais 2015) lakini historia ya mema aliyoyafanya haifutiki na si kigezo cha kumshusha hadhi kiasi cha kumlinganisha na Shibuda. Lema namfahamu naye ananifahamu.. ukweli ana safari ndefu ya kisiasa lakini anaonekana anaanza kuimudu. Mnyika ni komavu kwenye siasa za upinzani na bado anazidi kujijengea umaarufu kama wengine, hivyo kuna kila sababu ya kujali mchango wa kila mmoja kwa nafasi yake.
 
Ila umesahau kuwa kinachomgharimu ZZK 2010-2015 ni kujiweka mbali na chama na kujitazama yeye binafsi tofauti na yule ZZK wa 2005-2010. Kama anapitia hapa jf, basi achukue mambo haya kama changamoto na autathmini upya mwenendo wake kichama.
Kweli hili jamvi lina mambo.. nimejaribu kupitia posts za wachangiaji wengi. Mhh inavyoonekana wasiokubaliana na Zitto wanakosa hata uvumilivu wa kumpa credit anazostahili.. hakika kuna credit nyingi anazostahili kupewa.

Zitto ni kati ya vijana wachache wasomi, wenye uwezo wa kujenga hoja, kufanya tafiti na kusimamia anachokiamini, na kupitia sifa hizo amejikuta baadhi ya makundi ya vijana hayamuamini na na pia haya mkubali, ila vijana hao wanasahau kwamba penye mvutano wa kifikra kama mawazo huru yanazingatiwa husaidia kutufikisha kwenye mafanikio.

Ni ajabu wengi humu hudiriki kusema Zitto hastahili kulinganishwa na Mnyika, Lema nk, lakini ukiichambua cdm utagundua kwamba Zitto anahistoria ndefu yaliyokiletea chama mafanikio.. yawezekana kabisa asilingane na hao anaolinganishwa nao. Tuweke ushabiki pembeni tujadili hoja, kisiasa kuna mengi ya kupitia na yeye kwa sasa kuna mambo kadhaa yanamgharimu (kama la kutangaza kuwania urais 2015) lakini historia ya mema aliyoyafanya haifutiki na si kigezo cha kumshusha hadhi kiasi cha kumlinganisha na Shibuda. Lema namfahamu naye ananifahamu.. ukweli ana safari ndefu ya kisiasa lakini anaonekana anaanza kuimudu. Mnyika ni komavu kwenye siasa za upinzani na bado anazidi kujijengea umaarufu kama wengine, hivyo kuna kila sababu ya kujali mchango wa kila mmoja kwa nafasi yake.
 
Zittn yu kigeu geu na mara kadhaa tumesikia akifanya alliance na Rostam Aziz pamoja na Jk hvyo hafai.
Dr Slaa ni chaguo sahihi kwa uraisi wa Tanzania.
 
Yaani mnamlinganisha Zitto na Dr Slaa,mnamatatizo nyie!Slaa ni habari nyingine!
 
Ni kweli mkuu lakini itasaidia kukata kilimilimi cha wafuasi wa Magamba hapa jamvini.Na ndiyo maana vibaraka nguli wa Magamba hapa JF wanachungulia tu hii thread na kukimbia.
ndo waliofungua ID nyingi nyingi mpya ili wampigie kibaraka mwenzao kura lakinibado naona hazitoshi, nimeshangazwa kupata 15% badala ya 0.001%
 
Weka kura yangu kwa daktari, Mfumo wenu unakataa kunipa fursa ya kupiga kura
 
Niwekee kura yangu kwa Dr Slaa maana huyu kwangu ndio kila kitu,hakuna cha Zitto wala nn maana amekua kibaraka cha wezi
 
Ni kweli mkuu lakini itasaidia kukata kilimilimi cha wafuasi wa Magamba hapa jamvini.Na ndiyo maana vibaraka nguli wa Magamba hapa JF wanachungulia tu hii thread na kukimbia.

Kumbe kelele nyingi sana za vyura ni 15.78% tu?. Hizi kweli hazitamzuia tembo(84.22%) kunywa maji. Pro ccms wanajilaumu sana kwenye kura hii ya maoni.
 
Kumbe kelele nyingi sana za vyura ni 15.78% tu?. Hizi kweli hazitamzuia tembo(84.22%) kunywa maji. Pro ccms wanajilaumu sana kwenye kura hii ya maoni.

Na tena hizi ni baada ya juhudi kubwa za Magamba kusajili ID mpya mpya kibao ili waondoe aibu.Laiti ingekuwa ni wanachama wa CDM tu wanashiriki hili zoezi basi matokeo yangekuwa ni 99% Vs 1%
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom