Kweli hili jamvi lina mambo.. nimejaribu kupitia posts za wachangiaji wengi. Mhh inavyoonekana wasiokubaliana na Zitto wanakosa hata uvumilivu wa kumpa credit anazostahili.. hakika kuna credit nyingi anazostahili kupewa.
Zitto ni kati ya vijana wachache wasomi, wenye uwezo wa kujenga hoja, kufanya tafiti na kusimamia anachokiamini, na kupitia sifa hizo amejikuta baadhi ya makundi ya vijana hayamuamini na na pia haya mkubali, ila vijana hao wanasahau kwamba penye mvutano wa kifikra kama mawazo huru yanazingatiwa husaidia kutufikisha kwenye mafanikio.
Ni ajabu wengi humu hudiriki kusema Zitto hastahili kulinganishwa na Mnyika, Lema nk, lakini ukiichambua cdm utagundua kwamba Zitto anahistoria ndefu yaliyokiletea chama mafanikio.. yawezekana kabisa asilingane na hao anaolinganishwa nao. Tuweke ushabiki pembeni tujadili hoja, kisiasa kuna mengi ya kupitia na yeye kwa sasa kuna mambo kadhaa yanamgharimu (kama la kutangaza kuwania urais 2015) lakini historia ya mema aliyoyafanya haifutiki na si kigezo cha kumshusha hadhi kiasi cha kumlinganisha na Shibuda. Lema namfahamu naye ananifahamu.. ukweli ana safari ndefu ya kisiasa lakini anaonekana anaanza kuimudu. Mnyika ni komavu kwenye siasa za upinzani na bado anazidi kujijengea umaarufu kama wengine, hivyo kuna kila sababu ya kujali mchango wa kila mmoja kwa nafasi yake.