Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA?

  • Zitto Z. Kabwe

    Votes: 180 15.3%
  • Wilbrod P. Slaa

    Votes: 996 84.7%

  • Total voters
    1,176
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Atutaki wazee safari hii,ZITTO katimia idara zote, kosa fitna sasahivi angekuwa mwenyekiti.
 
Hii nidharau kubwa.Huwezi kupambanisha Barcelona FC na Lipuli ya Iringa.

Zitto bado anatakiwa awe na muda wa kumature, anaweza kuwa kiongozi mzuri hapo baadaye, lets have at least ten years za pumpitisha kwenye testing ... IQ,uaminifu, Rushwa,.
Slaa amepita vigezo hivyo vyote
 
Najaribu kusikiliza hotuba yake hapa on line akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani bungeni kuhusu Wizara ya Fedha, huyu bwana ni jembe sana hata kama ana mapungufu yake kadhaa, hotuba nzuri imejaaa tafiti lakini pia kariba ya flowing nzuri sana hatumii nguvu na jazba kama wenzake.
 
he is very controversial though.
otherwise, big up for the good things he is doing for his beloved country
 
Mwisho wa siku mtoa mada utakuja ujue kuwa tofauti na ulivyotegemea kuwa unmuimarisha unaempigia debe badala yake umemdhalilisha. Angalia trend ya votes!
 
Hii thread imeanzishwa na mtu mwenye mtazamo wa udini. Ukisoma katikati ya mistari utagundua kuwa thread hii iko katika makusudi mawili muhimu; kwanza kuwachonganisha viongozi waandamizi wa CHADEMA lakini pili ni kutaka kuonyesha udini ndani ya CHADEMA kwa vile huyu mwanzilishi anajua kabisa kwamba ukimpambanisha Dr.Slaa na Zitto Kabwe katika hali yoyote ile Dr.Slaa ataibuka mshindi kwenye kura yoyote ya maoni.

Kumlinganisha Dr.Slaa na ZZK ni sawa kulinganisha Mlima(Dr.Slaa) na Kichuguu(ZZK)!Huo ni ukweli mchungu kwa wote wanaoichukia CHADEMA na hata wale wapenzi na washabuki wa ZZK. Napenda kumhakikishia huyu mwanzilishi wa hili wazo hata kama angemchukua Dr.Slaa akampampanisha na Jakaya Kikwete bado Dr. angeibuka kidedea. Hilo halina ubishi!

Nimalize kwa conclusion ifuatayo: Kwamba hii yote ni kazi chafu ya Magamba at work. Tumesikia mengi sana kuhusu CHADEMA kutoka kwa kina Nnape,Mchemba,Wassira kina Kova na wengineo. Kwamba CHADEMA hakina miaka hata 2 ijayo kitakuwa kimekufa kabisa!!!Sasa mipango ya kuiua CDM ndiyo kama hii ya kijinga ya kutaka kuwafanya Watanzania majuha na hawamnazo. CCM wanatapatapa na kubabaika kila kukicha hasa wanapoona M4C ikijipenyeza kwa kasi mpaka vijijini. Hizi ni dalili njema kwa CDM na dalili mbaya sana kwa CCM!

Tunajua kuna kitengo maalumu ndani ya UWT(TISS)kimeundwa kuhakikisha kuwa CDM haifiki mwaka 2015! Huu ni wendawazimu. CCM na serikali yake wanafikiri CDM ni kama kikundi fulani cha saccos,NGO,au kitchen party ambacho unaweza kukisambaratisha kwa mikakati kama hiyo.

CCM wanasahau kwamba CHADEMA ni chama cha siasa na kina wanachama,wafuasi na mashabiki ambao wako tayari kukipigia kura za ndiyo ili kiingie Ikulu kuwakomboa kisiasa,kiuchumi na kimaendelea baada ya kupigika kwa miaka 50! Huo ni ukweli ambao CCM wanatakiwa waujue. Style wanayotumia CCM kutaka kuimaliza CDM ni sawa na kilekile walichokifanya kwa Dr. Ulimboka kwamba ukishamuua kiongozi wa Chama basi umemaliza kazi!!Tumesikai mipango ya kutaka kuwaua viongozi waandamizi wa CHADEMA akiwemo Dr. Slaa,Mhe. Freeman Mboew,Mhe.John Mnyika na viongozi wengine wa chama mabao ni tishio kwa serikali ya CCM. Katika orodha hiyo ya mauaji jina la Zitto Z.Kabwe halijatajwa! Kwa watu makini wanaweza kujua mchezo unaochezwa na CCM na serikali yake. Mimi nasema huu ni ujinga na upuuzi wa CCM ambao hautawasaidia asilani kwani mwisho wa siku watajikuta wametwanga maji kwenye kinu. Poleni sana wana CCM na serikali yenu ya kifisadi. Fainali ni T 2015 CDM.
 
sababu ziko nyingi kijana msomali ila kwa sababu umehitaji NNE tu,basi hizi hapa:-
Kwanza ningempa Dk.Slaa kwa sababu nne zifuatazo:-
1,Hotuba zake zote alizowahi kutoa zinagusa umma wa watanzania hasa wa hali ya chini.
2,Hajawahi kuwa na kashfa mbaya za msingi ukimlinganisha na zitto
3,Ameonyesha msimamo wa pekee na nia ya dhati kuwasaidia watanzania
4,NI mtu kwa namna moja au nyingine anafahamu vema matatizo na changamoto halisi
zinazowakabili watanzania wa aina yoyote(tajiri au maskini).
 
Mleta mada ana lake jambo, Zitto ana kitu gani mpaka atake amfananishe na Dr. Slaa?

1. Zitto sina shaka na uwezo wake wa kujenga hoja ila ni mnafiki anayependa cheap popularity.
2. Zitto ni ndumilakuwili hivyo siyo mtu wa kumwamini.
3. Dr. Slaa yuko stable, Shupavu na mwenye kutumia reasoning ya hali ya juu.Dr. Slaa pamoja na umaarufu wake, kupendwa sana na watu hajawahi kuonyesha kuwa yeye ni zaidi ya chama. Wakati mwenzake mara nyingi amekuwa akituonyesha kuwa yeye ni zaidi ya chama.
 
1 Zitto ajibu hoja za BARICK LTD. Walisha mnunua bado hajajibu
2. Zitto alikula posho mbili, Takukuru wakimtaka saa yo yote wanamdaka, ni kwa vile ni mtu wao.
3. Zitto ana mahusiano ya karibu na mkurugenzi msaidizi TISS aliyechakachua kura za Dr Slaa.
4. Zitto hakumpigia kampeni Dr Slaa, akamnadi kikwete kisiri kigoma na NCCR. Aeleze kwanza.
5. Zitto alipigia debe kununua mitambo ya Richmond aka downs.
6. zitto alikuwa na gari liliingia bongo kwa jina la Rostam, aeleze vizuri ilikuwaje? wakati yeye majuu ni mwenyeji?
7. zitto ni fisadi kama wengine abishaye alete data hapa.

Naunga mkono hoja
 
Mbona hii mada ipo neutral,labda tatizo lipo kwako.

Mwisho wa siku mtoa mada utakuja ujue kuwa tofauti na ulivyotegemea kuwa unamuimarisha unaempigia debe badala yake umemdhalilisha. Angalia trend ya votes.
 
Kuna haja ya kuweka definition kamili juu ya neno kashfa, maana Nape huchukua maisha ya mtu binafsi kama kashfa na ufisadi wa ccm kama utakatifu.

sababu ziko nyingi,umehitaji NNE tu,basi hizi hapa:-
Kwanza ningempa Dr Slaa......1,...
2,Hajawahi kuwa na kashfa mbaya za msingi ukimlinganisha na zitto
 
Na kama anataka umaarufu basi afungue chama chake ,
m nlikuwa nasikia watu zamani wakisema watu wa kigoma hata umkute ana akili sana ila itatokea siku akarudi kuwa kama illiterate maana elimu aliyoipata haikai kichwani inapita kama upepo tu na kumwacha kama alivyozaliwa.
Nadhan ndo haya tunayoyashuhudia kwa huyu mropokaji-binafsi na mtaka madaraka kwa pupa zitto

acha upumbavu jaribu kuficha your illiteracy mada haihusiani na mtu anatokea sehemu gani jaribu kujadili kwa kutumia hoja co et kisa mtu anatokea kigoma,nyau we
 
CHADEMA haina udini wala ukabila wowote kwani katiba na sera za chama havionesh udini ila kuna watu ndani ya chadema ndio wana mambo hayo hvyo basi hatuna budi kuwaepuka watu hao mtu yeyote anaechangia mada hii kwd kuwajudge dr slaa na zitto kabwe kutokana na dini zao na mahali wanapotokea yeye ndio mdini na mkabla
 
Kuna haja ya kuweka definition kamili juu ya neno kashfa, maana Nape huchukua maisha ya mtu binafsi kama kashfa na ufisadi wa ccm kama utakatifu.

sababu ziko nyingi,umehitaji NNE tu,basi hizi hapa:-
Kwanza ningempa Dr Slaa......1,...
2,Hajawahi kuwa na kashfa mbaya za msingi ukimlinganisha na zitto


Msingi wa uongozi unaanzia katika ngazi ya familia,hakuna ubishi Dr Slaa ameshindwa kwa hilo.Tofautisha kupiga kelele majukwaani na kuongoza watu.Slaa hafai kuwa rais amechoka ni heri aje azibe pengo la Bob Makani katika baraza la wazee.
 
ni kweli ulichokisema kuwa kati ya Zito na Slaa nani awe Rais.Mm nathubutu kusema kuwa hawo wote hawana sifa za kuwa rais coz tunaitaji rais ambaye yupo kwa maslahi ya taifa nasiyo maslah ya chama wala maslahi ya dini yake,pia aongoze inch kwa kuheshimu dini zote bila upendeleo.lkn cha msingi haya yote yanayotokea leo ni makosa yaliyofanywa na waliotangulia.Nawashauri wanaJF kwamba tumchague rais bila kuangalia chama chake km mtu yupo chadema anauwezo apewe nafasi nasio chama,pia hata wabunge tuangalie mtu pia ninaimani kuwa kuna watu wapo chadema lkn hamna kitu,kuna watu wapo CCM wanauwezo WANA JF ELIMIKENI MSIWE BENDELA FUATA UPEPO!!!
 
Ni kumkosea Adabu na heshima Dr Slaa kumlinganisha na Zitto, ningewaelewa kidogo kama Zitto angeshindanishwa na mtu wa level yake kama Mnyika. Dr Slaa ni habari nyingine kabisa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom