Ingawa Mada ni ya kichokozi, '' Mimi nimeshindwa kumuelewa zito anapotanagaza mapema kuhusu dhamira yake ya kutaka Urais. Ingawa si kinyume na sheria lakini hazitendei haki kanuni za Umoja wa kichama hasa wakati huu ambapo chama kiko katika harakati za M4C kujiandaa kushika dola 2015. Zito haonekani mara nyingi katika harakati na matukio ya kichama. Hakuonekana Uzinduzi wa M4C pale Jangwani na katika Routes nyingine za M4C. Nadhani huu si wakati wa kutangaza nia, kuna mambo mengi ya Msingi na Muhimu kwa wanaCDM na waTZ kwa ujumla wanapaswa kuyaona na hivyo kuwaandaa kuwa chini ya dola itakayoongozwa na CDM. Tuwaandae waTZ kwanza, kisha tuwaombe ridhaa ya kuwaongoza..