Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA?

  • Zitto Z. Kabwe

    Votes: 180 15.3%
  • Wilbrod P. Slaa

    Votes: 996 84.7%

  • Total voters
    1,176
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Jamani mimi nina mashaka na huyu dogo. Ukitazama picha zake nyingi utaona akiwa na watu wa CCM anakuwa yu mwenye furaha sana as if hao jamaa ni wenzake.
 
HUna hoja wewe,una tofauti ni Nape, sisi hatupo kiccm ccm kama ulivyo wewe ! Unaombea cdm ivurugike karaga bao,imekula kwenu!!!!!!!!!!!!! Hoja nyepesi ina reflect ubongo dhaifu.
 
Dr. W. Slaa
1. Ni kiongozi shupavu asiye na woga katika mambo yake.
2. Umri wake, si rahisi kumuhusianisha na kashfa za ujanami.
3. Anasifa za nzuri za kielimu na ujuzi mkubwa wa kiuongozi tena kwa uadilifu mkubwa.
4. Amejitoa kwa ajili ya kusaidia mamilioni ya watu wa tanzania.
 
Hii ni karne ya vijana kwani ndo taifa la leo, wazee wanafaa kuwa ma prime minister or watapewa nafasi za ushauri...!! Tumewaachia sana for the past 50yrz zinawatosha. The world is so fast and with rapid unexpected changes kila kukicha so inabidi kuwa na kijana anaeweza kwenda na hiyo kasi ya mabadiliko..!! We still apriciate michango na ushauri wa wazee kwenye kuelekea mabadiliko haya hasa mzee wetu Dr slaa....!! Aluta continua...
 
lkn usisahau vijana wa sasa mna haraka sana nchi itamalizika mf waziri wa madini aliyepita,waziri wa maliasili inatutia mashaka sana vijana wetu
 
Tuache kelele nyingi, kama ungepewa mamlaka ya kumteua kati ya Zitto Zuberi Kabwe ama Wilbroad Peter Slaa kugombea nafasi ya urais mwaka 2015. Ni nani ungemteua? Na Kwa Nini? Toa sababu kuu nne TU.
Nitamteua MH: DR.WILBROAD PETER SLAA,Mh zitto anaonekana ana uchu wa madaraka na mwalimu Nyerere alishaonya ya kwamba ukimuona mtu anakimbilia ikuru muogope kama ukoma, mimi nasema muogepe kama ukimwi
 
subiri uone udini wa chadema watakavyomrukia ZITTO. wanajua zitto ni kichwa kupita hata huyo slaa lakini slaa wanampenda kwa kuwa ni PADRI.
Wewe unaonekana una mtazamo finyu hoja kubwa yako ni udini, kwa taarifa yako Zitto hana sifa hata kidogo ya kshindana na kamanda DR. Slaa ni sawa na mtoto wa darasa la saba ashindane na mtu wa masters.Magamba ndiyo wadini kamati kuu ya magamba ina wajumbe 35 kati ya hao 22 ni waislam na waliobaki ndiyo wapagani na wakristo, au ndiyo nyani haoni kundule?
 
Hao wote ni wezi slaa mwizi na zitto nae mwizi kwa hy hawafai ktk serikali yetu
 
Wana JF, Mie ningeendelea kumchagua Dr. W.P Slaa. Ningefanya hivi si kwa sababu simpendi Zitto. Ni kwa sababu Dr. Slaa, amekomaa, hana papara (ukizingatia kuwa alikuwa kiongozi mwenye wadhifa mkubwa akiwa katibu wa AMECEA), tumeendelea kushuhudia busara zake alizotumia kipindi hicho zinaendelea katika kukiendeleza chama chetu japokuwa amehama field. Akipata wasaidizi kama kina Zitto, anaweza kufanya maamuzi magumu, ambayo tunahitaji katika nchi hii, ni mwanafalsafa ambaye hayumbishwi (hii inatokana na kuachia ngazi ya daraja lake la kipadri na kuishi maisha ya kilei).

Upande wa rafiki yangu Zitto, bado ni kijana sana (ingawa mwaka 2005 rais wa Georgia alikuwa na miaka 36), akipata washauri wazuri wenye uzoefu wa kiungozi anaweza kuelekea kuwa kiongozi mzuri.
 
Tuache kelele nyingi, kama ungepewa mamlaka ya kumteua kati ya Zitto Zuberi Kabwe ama Wilbroad Peter Slaa kugombea nafasi ya urais mwaka 2015. Ni nani ungemteua? Na Kwa Nini? Toa sababu kuu nne TU.



Usimjaribu jirani yako.Akishajua kuwa unamjaribu atakuaibisha. Hoja yako haina mashiko kwa sasa.Imejaa chokochoko nyingi zenye ukakasi. Majibu ya sifa au sababu za mtu anayetakiwa kuwa rais 2015 kati ya hao watu uliowataja, wewe ndiye unayezifahamu. TIME WILL TELL YOU.
 
wanachadema huu ni mtego wa kutaka kuleta makundi kutoka kwa kada wa ccm tuwe waangalifu tuko na kazi ya kuijenga nchi na chama hebu waambie waweke mpambano kati ya sitta na Lowassa au Lowassa na Membe , au upime ubora wa utawala wa Mkapa na Kikwete watang'aka hao
 
na ukiingiza mpambano wa ccm utashangaa unatolewa na moderator
 
Ujana wake nayo ni sifa? kwani ukiwa mzee huwezi kuwa rais?
sababu za kuto mchagua Zitto Kabwe
1. hana sifa ya kugombea urais coz hajatimiza umri unaotakiwa na sheria
2. hana sifa ya kugombea coz ana uchu wa madaraka
3. hana sifa ya kugombea urais coz hana Busara na hekima
4. hana sifa ya kugombea coz anatumiwa na ccm
Mkuu kweli huyu kijana hafai hata kuendelea hata kuwa mbunge yeye wenzake wanajenga chama kupitia M4C, Yeye yupo kwenye kutangaza nia ya kugombea urais, hata uchaguzi bado,Ila mwalim nyerere alishaonya ya kwamba ukimuona mtu anakimbilia kwenda ikuru kama Zito muogope kama UKOMA mimi nasema, muogope kama UKIMWI.
 
Nina wasiwasi mtoa mada anatumiwa na ........ Hizo ndio propoganda za kisiasa.Chadema kuweni makini na hilo kwa sababu mnakaangwa na mafuta yenu wenyewe .......Masalaaaaaaaaam.
 
zitto ana uchu na urais. Nahisi Akiupata ata binafsisha(ziwe zake binafsi) migodi na tanesco.
Ila kigoma watafaidi nyimbo nyingi zaidi na show za bure ijumaa mpaka j2 all year round
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom