Mmwanaume rijali kama kweli ni rijali, una hela na maisha mazuri umefikia umri wa kuitwa mtu mzima basi ni lazima uwe na mke, kama hujaoa hapo lazima tujiulize mara kumi kumi. Something is not right here. na kwa nini usoni mbona kama amejichubua awe mweupe????
Mimi siwezi kutoa maoni.....kumuweka dr.slaa na zitto kishoka nadhani ni dharau sana......zitto hajafika hata robo ya dr.slaa kwa hiyo kura ya maoni ni dharau kwa kiongozi mwenye heshima km dr.slaa.....sijui labda zitto umshindanishe na shibuda ingefaa kwani hata kwa mnyika au lema haingii
tuacheni dharau kwa rais wetu
Katika imani yako umekuwa spoiled,
unaamini kwa dhati kwamba,
maoni kinyume na imani yako,
ni batili na ni dalili ya upendeleo.
katika kura hii una nafasi ya,
kutumia nafasi yako kama member,
kumchagua umpendaye,
au kuto piga kura kwa kula jiwe,
una haki ya kutoa maoni yako binafsi,
huna haki ya kuingilia haki za watu wengine,
maelezo yako ni maoni yako binafsi,
yatoe lakini usiyafanye msahafu kwa wengine,
Padri, sheikh, mufti, askofu,kuhani,mzee wa busara?
uchaguzi ni wa mtu binafsi,
Hapa JF wote ruksa kujiunga,
nasikia tu kwamba,
80% ya population,
ya watu wa dini na imani moja kuu,
ni zaidi ya nusu ya Watanzania wote,
pia kundi hili la waumini,
ni watu wa kheri amani na unyenyekevu.
Naamini pia kwamba kundi hili la waumini,
ni 75% ya wanachama wa JF,
Sasa ikitokea kundi hili kumpenda zaidi Dr Slaa,
kwa sababu ya uwingi wao na tafakari yao,
wewe ni nani hata upinge na kubeza chaguo lao?
pia kuwa na mawazo ya kudhani ni upendeleo?
Waswahili husema Wengi wape.
Zitto anafaa zaidi
Ni wewe na wengine wachache mno ambao mlikuwa bado mnajua Hayati Mwl Nyerere bado Rais wa TZ ndiyo hamkumjua Dr. Slaa.Heshima aliyonayo DR Slaa ni kwasababu tu alikuwa kiongozi wa kanisa na umri alionao kulinganisha na zitto, zitto amekuwa kwenye siasa muda mfupi sana kulinganisha dk Salaa lakini amekuwa na mafanikio makubwa sana kutokana na uwezo wake,amekuwa maarufu sana hayo yote ameyapata muda mfupi tu. Watanzania wengi hatukuwa tukimjua dk Slaa hadi pale alipogombea uris 2010, kwahiyo heshima aliyonayo dk Slaa ipo kidini zaidi kwa waamini wake sio kisiasa, heshima na umaarufu alionao ZZK unatokana na uwezo eake mkubwa ktk siasa, kwahiyo kisiasa zzk yuko juu zaidi kuliko dk Slaa
"Kwa kuwa ‘my conscious is clear', (dhamira yangu safi) sina mashaka, uzushi, uongo na siasa za majitaka hizi zitaumbuliwa na ukweli.by ZZK