Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA?

  • Zitto Z. Kabwe

    Votes: 180 15.3%
  • Wilbrod P. Slaa

    Votes: 996 84.7%

  • Total voters
    1,176
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Dr Slaa kesha set standard za siasa za Tanzania. Ni yeye aliyedhubutu kuibua hoja ambazo awali hazikuweza kujadiliwa. Yafaa tumpe nafasi aweze kuiweka Tanzania kwenye njia itakayo faa lwa watanzania wote. Zitto ameweza kupata sifa kwa kuwa karibu na Slaa. Asijisahau akifikiri anaweza kuchukua nafasi wakati huu. Bado Slaa ni mwiba mchungu/mzito na wenye makali kote.


SLAA NI KIONGOZI SHUPAVU


Alhaj Ommari
 
Nyinyi mnaotumika kuleta migogoro mnapata faida gani!!? Mleta mada umejaza funza kichwani!!!

Usiwe na wasiwasi mkuu, Chadema wanajua jinsi ya kutatua migogoro yao. Huyu aliyeleta mada anajaribu kufanya hicho lakini hawezi kufanikiwa, Chadema know what they are doing
 
WAtasema sana lakini wanajua kwamba ZITTO ni jembe hakuna kama yeye Chadema.

Huo sio ukweli, Muondoe Zitto Chadema uone kama itatetereka? Chadema ina viongozi wengi wazuri tu, kila mtu na mchango wake.
 
....both dont deserve!.... Slaa is too aggresive to be a presd n Zitto has no true colors!
 
Zitto si saizi y Dr. Slaa kabisa, saizi yake ni akina Mnyika, Mdee na wenzake. Aache mdomo hana ubavu wa Urais bali anatumiwa na CCM. Na kuna siku tutamuanika peupee ili aache upopo wake ndani ya Chadema.

Asante! Nilifikiri ni mimi tu ndo naliona hili!
 
Tuache kelele nyingi, kama ungepewa mamlaka ya kumteua kati ya Zitto Zuberi Kabwe ama Wilbroad Peter Slaa kugombea nafasi ya urais mwaka 2015. Ni nani ungemteua? Na Kwa Nini? Toa sababu kuu nne TU.
1.Dr. Slaa keshamaliza ujana.
2.Hataenda kuitumia ikulu kama nafasi ya kujionyesha kuwa ni mwenye mamlaka.
3.He is serious...mpaka sasa hajanunulika(ingawa siwezi jua kwa undani....ila mpaka sasa haijatokea kashafa yeyote inayoweza kuthibitisha hilo) kwa case hii itakuwa ni vigumu kumuonea mtu haya.
4.Kwa kuzingatia uchaguzi wa 2010, jamaa hakushinda kwa sababu nya nguvu za mtu, alishinda kwa nguvu za umma, ni rahisi kuutumikia umma, so hatakuwa mtumwa wa matajiri na watu binafsi pindi aingiapo ikulu.

Ziko million...kunyume za hizo mpe zito.
 
Mimi nisingejali ukwasi wake lakini suala la uraisi kwa sasa tuwaachie wanachama wapime uweledi wa wale watakapambanishwa wakati mwafaka.
 
kwa hiyo hawa wana JF wote wanaomuunga mkono Dr Slaa ni wachagga?
 
Wadau nitafanyaje niwaone waliopiga kura? nataka niwajue pro-vatican

At the top of the Pyramid, Vatican na Mecca are the same...walioanzisha hizo zote mbili ni wale wale na kwa makusudi yale yale...

You will know them by the signs they use...chezea Illuminati wewe!
 
Naungana na wenzangu katika hili: Zitto ni mtoto mdogo sana kisiasa na hata wered ukimlinganisha na slaa, embu angalia uwezo wa kiutendaji wa zitto kama katibu msaidizi na slaa kama katibu mkuu, angalia pia msimamo katika mambo ya msingi yenye maslahi ya chama utamwona zitto yuko nyuma, zitto anafanya siasa za kisasa ambazo kwa Tz bado sana, isitoshe anashindwa kuendana na mikakati ya chama ili kufika malengo
 
Siku moja kwa mwanasiasa ni kama miaka mitano vile, kwa sasa Zitto Kabwe hana sifa hata ya kuwa balozi wa nyumba kumi, anahusishwa na hujuma za kupokea rushwa na kufanya biashara na Tanesco, Ukimpa urais atauza mpaka Hewa
 
Ndugu zangu wa Chadema naomba niwakumbishe jambo moja la msingi sana. Adui anaweza kutumia mbinu ya kitoto sana kukuangamiza. na mbinu hii inaitwa HILA. Hila ni pale adui anapokuletea jambo ukaliona kama ni zuri kwa muonekano wa kwanza ila ukishajiingiza linakurudi na linakuweka katika hali ambayo inakugharimu au kukuweka katika hali mbaya kuliko ulivyokuwa kabla ya kukubali kuingia kwenye mtego. CCM na mapandikizi yao wanatumia mbinu ya ya kuleta hoja kuujadili uraisi kwa sasa ili Wanachadema wajisahau wabaki wanalumbania uraisi halafu hiyo iwe chanzo cha migogoro na kujisahau kupambana na ufisadi na kukujenga chama, halafu wapate upenyo wa kuwamaliza Chadema. Ukiangalia viongozi wengi wa chadema hawajihusishi sana na suala la nani agombee 2015, wengi wako bussy kukijenga chama katika maeneo mbalimbali ya nchi. Huyu Dr. Slaa anayejadiliwa hapa nakumbuka katika mahojiano na mwandishi mmoja wa habari aliulizwa kama atagombea 2015, akajibu hivi: Vikao vya chama ndio vinamteua Mtu atakayeshika bendera kukiwakilisha chama katika nafasi ya uraisi, Hivyo mimi siwezi kusema sasa hivi kama nitagombea au la. Hayo ni maamuzi ya vikao wakati ukifika. Nawaomba wana CDM tuachane na hoja za namna hii kwa sasa. hoja yetu kubwa iwe ni kupambana na ufisadi na kukijenga chama. Ili tuweze kuwangoa hawa Magamba.

safi sana, wana CDM tutalumbana sana hapa lakini tukumbuke hata 2010 Dr.SLAA hakuchukua fomu ya kugombea peke yake, walikuwepo na wengine lakini yeye akachaguliwa na tukamuunga mkono, na hili la Zitto na Dr tuliache maana atakayechaguliwa hata kama siyo wao tutaweka tofauti zetu pembeni tumuunge mkono.
TUSIWE KAMA MAGAMBA 'CCM'.
 
Hivi nyie waklisto mboa wabaguzi? hivi sisi tunapowapigia kula waklisto hadi wanakwenda bungeni tumekuwa mabwege? kwanini hamuelimiki? mbona sisi Dr Slaaha tunampenda sana hatumbagui? kawakosea nini huyu Zitto asiyekauka midomoni mwenu? lakini kwakuwa wakristo wameanza kutubagua waislamu na sisi waislamu wote tunampenda ZUBERI ZITTO KABWE ndo swala zima tena niko tayari kuingia msikiti hadi msikiti kuwaambia waislamu wenzangu kuwa tusimchague slaa kwani ni mdini tutapata shida na dalili mmeshazianzisha yani mkianza hivyo mnavyotaka mbona 2015 kazi ipo, mana CCM mwaka 2015 lazima asimame mkristo mana katoka muislamu sasa kwanini na nyinyi msimsimamishe muislmu ambapo alitoka mklisto? kama mnapigania haki kwa maslahi ya waklisto mtachemka hakuna muislamu aliyezubaa kwa tgaarifa yenu

sijui haya yanatoka wapi kwa kweli, dini yako peleka kanisani au msikitini siyo kwenye siasa ya nchi. Tukichaguana kwa dini zetu mbona wengine watalia, tuchaguane kwa sifa za mtu na msimamo wa mtu kwa maslahi ya taifa na siyo misikiti na makanisa.
 
Waliosema Slaa wote wa mrengo ule wa CDU.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom