Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA?

  • Zitto Z. Kabwe

    Votes: 180 15.3%
  • Wilbrod P. Slaa

    Votes: 996 84.7%

  • Total voters
    1,176
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Unajadili suala la 'kusadikika'...huijui kesho hata ulowapendekeza hujui watakuepo au la,tafakali
 
Dr slaa my luvly president.hao vigeugeu,wauza sura hatuwataki.kwanza cku hiki kirusi kitatoka CDM nitarukaruka kama ndama.
Dogo anapenda publicity huyo,kama clouds fm ameshaifanya kama yake
 
Mshangao wangu mimi ni kwa nini Zitto anapendwa sana na Pro-CCM? Kwamba wanaitakia mema CHADEMA au? Na Zitto ajiulize kwa nini Vijana wengi sasa hivi wanamchukia kuliko ilivyokuwa mwaka 2007 alipoibuka na hoja ya Buzwagi?

TUMBIRI (Upanga, Dar es Salaam),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Last edited by a moderator:
Unajua Zitto huwa simwelewi! ukimwangalia anakuwa kama kigeugeu hivi, anakosa subira na kiongozi mzuri subira, umoja, upendo, busara na heshima kwa viongozi wenzako muhimu.
 
Naomba kutoka nje ya mada kidogo, nadhani sio fair kumpambanisha Zitto na Dr. Slaa...sio wa uzani mmoja jamani!

Zitto hata akipambanishwa na Dr ktk category ya vijana tu, bado hawezi pata theluthi moja ya kura....na hapo ndipo palipokuwa panaonekana kwamba ZZK ana ushawishi mkubwa, so naomba usimamishe mpambano huu ili kumnusuru ZZK.

Tena ukizangatia hali ya siasa ilivyo sasa hususan ufisadi wa umeme nchini na tetesi za maslahi ya Zitto upande mmoja wa sakata la kashfa hii, ndio atazidi kuumizwa.

Baada ya kusema hayo, kura yangu ya NDIO ni kwa DR. SLAA.
 
Nimestuka sana kwa mjadala wa aina hii kwani mbona tuna muda mwafaka wa kujadili suala hili bila kuathiri Utawala unaoporomoka kila kukicha hebu fikiria miaka mitatu ijayo ni mingi sana kuwepo na mabadiliko makubwa kwa wagombea Urais watarajiwa kwani kati yao hakuna aliye ongea na mungu na akaridhia kugombea kwake.acheni kutupotezea muda wetu wa thamani kwa masuala ya kufikirika.
 
Kama ni udini bora nifukuzwe lakini kwenye ukweli dr slaaaa ni zaidi ya kiongozi, tusianzishe yale mambo tuliolewa sifa hata baadhi ya majimbo tuliokuwa na nguvu kama tarime tukapoteza kwa kuweka mgombea yeyote tu hata wakurya wakashtuka hii ngoma 2015 kama mungu akimpa uhai dr slaa na tukamuunga kwa moyo mkunjufu wakati wetu wanyonge kuona haki utakuwa umewadia
 
Haraka yote hii ni ya nini? Bado tuna miaka miwili mbele yetu ili kufika wakati muafaka wa kuzungumzia wagombea uongozi katika nafasi mbalimbali.
Hii kura ya maoni hapa haitusaidii chochote, sana sana itapalilia makundi ndani ya chama ambayo yanaweza kukivuruga chama na kuondosha mshikamano miongoni mwa wanachadema.

Kama ninavyoshauri kila mara, wanachadema tuachane na hizi sarakasi za uraisi kwa sasa. Tujielekeze katika kujenga na kuimarisha chama ngazi za chini-misingi, matawi na kata kwakuwa huko bado hakuko stable.
Rai yangu kwa wanachadema na wanaoiunga mkono chadema hapa JF naomba tuachane na mijadala isiyo na tija kwa maendeleo ya kisiasa na kidemokrasia. Tusipoteze muda kujadili mambo ya uraisi kwa sasa hakuna tija yoyote kwa mustakabali wa nchi yetu.
 
Mtu mzima dawa Mh.ZZK anapaswa kumpa heshima Dk. Slaa kwakuwa kamzidi, pamoja na hayo Kiongozi bora ni muhimu lkn wananchi twapaswa kuwa bora zaidi ktk kumchagua huyo kiongozi, pia kuhakikisha tunamsimamia iliatimize wajibu wake inavyostahili
 
Zitto Zuberi Kabwe for presidency. Huyo Dr. Slaa has expired, akapumzike na mkewe huko hana jipya tena
 
zitto atapata kura nyingi akigombea urais kuliko slaa,Slaa ni mzee kwa sasa.
Labda uweke data vinginevyo hilo unalosema ni ndoto za mchana.. inaeleweka sasa hivi ndani ya ccm kuwa hatari kubwa kwao kwa upinzani ni Slaa na sii vinginevyo ndio maana wanafanya kila wawezalo kum-disqualify kwenye nguvu ya umma ili waondoe hicho kikwazo, lakini kwa bahati mbaya mbinu hiyo pia inafeli sasa.
 
Mimi siwezi kutoa maoni.....kumuweka dr.slaa na zitto kishoka nadhani ni dharau sana......zitto hajafika hata robo ya dr.slaa kwa hiyo kura ya maoni ni dharau kwa kiongozi mwenye heshima km dr.slaa.....sijui labda zitto umshindanishe na shibuda ingefaa kwani hata kwa mnyika au lema haingii

tuacheni dharau kwa rais wetu
Rais yupi, Kikwete? Ama?
 
ZZK ni kijana smart na anafaa kuwa Mgombea wa Urais, na kwa hakika ana uwezo na uelewa mpana sana wa mambo mbalimbali ukilinganisha na WPS(ambaye ni popular kwa sababu ambazo 'zinajulikana'). Semeni kweli jama, WPS hana hoja zaidi ya kupiga kelele na radicalism, siyo mbunifu na wala hana qualities za uongozi, labda kama uanaharakati. Pia ile kauli yake ya nchi 'haitatawalika' inamgharimu sana, maana watu wana hofu hata kama yeye atashinda na kuwa Rais hatoweza kutawala kwa amani, nchi inaweza kuingia kwenye machafuko maana wanaccm watamrudi na wao kwa hasira. Pia udini na historia mbaya ya kampeni zake za 2010 za makanisani ni mambo ambayo yatamrudisha nyuma sana 2015 kama atapewa bendera apeperushe.

kama CDM inataka kushinda iweke mtu mpya na mwenye mvuto na si WPS ambaye amezoeleka na bahati mbaya sana ni mzee tena mgonjwa.
Kosa mtakalokuja kufanya CDM ni kutuletea mgombea Urais kama Slaa, hivi akishinda itakuwaje ataongea nini sasa, ataendelea kumtukana Kikwete na viongozi waliotangulia kwa hoja yake moja tu aliyonayo ya 'ufisadi' ama ataanza kuhaha kushika hapa na pale? Slaa ni mtu asiye na objectivity na ninadhani ana matatizo kwenye elimu yake na msingi wake wa maadili, hafai kuwa Rais wa nchi! Kama kanisani kwa mungu walimwona hafai wakamfukuza sasa atakuja kufaa leo hii huku duniani?
ZZK amejifunza uongozi na ameiva, na ninadhani anafaa kupewa nafasi aoneshe kipaji chake, na akikosa mara ya kwanza CDM mtakuwa mmemuandaa kwa ajili ya baadaye! Maana umaarufu wenu unakuwa kwa kasi na ipo siku mtapata Urais wa nchi, sasa kuweni makini, msiwe na haraka msikurupuke, tumieni vipaji vya vijana wenu vizuri!

WPS hana sifa ya kugombea Urais achilia mbali sifa za kuwa rais kwa sababu ni mdini, ana taswira ya udini (hata kama atakuwa siyo mdini kivile bado sisi wananchi wa kawaida tunamuona ni padri!) na hivyo hafai kuongoza taifa la watu wenye imani mchanganyiko kama Tanzania. Mkitaka muishie pale pale pa 2010 wekeni WPS na mtaona hamtofika popote, mkitaka kusonga mbele zaidi ya 2010 wekeni ZZK ama Freeman Mbowe (hawa wana dini zao lakini hawana taswira ya udini). kwa kuwa kura ni ya ZZK vs WPS, basi nachagua ZZK zaidi ya WPS.

WPS amesomea dini tu, hana elimu nyengine ya kidunia, watu wengi wana mashaka na elimu yake. Pia afya yake ni mgogoro na umri umemtupa mkono hawezi kupiga kampeni nzito za kutafuta Urais nchi nzima hii
 
mbona kuna wengine katika bench la CDM wanaweza wekwa na dr. ya nini mweka Zitto pekee?Kwanza nani kaua kuwa dr. atagombea? by the way kwa hali ya Bunge zitto anaweza jikuta akitegemea fadhila za CCM asijikute kura za bunge kuvuliwa ubunge zinambana.Si ajabu akang`ang`aniwa na takukuru ili aachie jimbo si unajua magamba hawana dogo ?
 
Wanajamvini nitoeni hofu kwa swali langu linanikosesha raha maana namtambua Slaa ni mwanaharakati shupavu na mwiba kwa CCM. Wana CDM mchakato wetu usonge mbele.
 
Labda awe Rais wa karatu hii nchi ina wenyewe mtaangaika kugombea hadi mfe kwanza na umri wake ule mpaka atafia jukwaani Urais wa nchi hii hata kaa akasikia harufu yake.Labda Raisi wa kukomba wa.. za watu
 
unamatatizo wewe mdini mkubwa wewe, kanzu avae Zitto huku wewe uumie roho inakuhusu? kama na wewe unataka si uvae hiyo barakashee na kanzu? huna jipya usipende kumdharau mtu kama ungekuwa mstaarabu ungemchagua unayemtaka nakutoa sababu za kumchagua siyo unaropoka ropoka tu kama umekula uji wa mihogo we vipi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom