Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA?

  • Zitto Z. Kabwe

    Votes: 180 15.3%
  • Wilbrod P. Slaa

    Votes: 996 84.7%

  • Total voters
    1,176
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Nadhani yapaswa kutofautisha kati ya uwezo wa kujenga hoja na uwezo wa kuongoza. Dr slaa anavyo vyote, zito ni mjenga hoja na sio kiongozi na tena ana uchu na madaraka kama ndugu yake kafulila.lakini tungependa tuone anatoka salama kwenye kashfa ya rushwa na kama atapatikana basi tutajua kumbe naye ni pandikizi la mafisadi
 
Kutoka fursa kwa wapiga kura ungeongeza C: Wote hawafai hivyo Mimi nachagua C
 
Yaelekea wengi humu si watu wa busara, mtoa mada kauliza swali.na.kaomba sababu basi kama wewe unaona Zitto anafaa au The Dr. anafaa zaidi toa sababu ulizoombwa.. ni vyema ukawa unatoa hoja na si kuponda bila hoja.
 
Dr. Slaa.

Ana msimamo thabithi, mjenga hoja, kiongozi bora na asiyependa ufisadi.
 
Dr.slaa 4rever.............!

Ni mjenga hoja, jasiri mithili ya God lema, hana bei, Mpiganaji kama mitili ya martin luther King Jr.
 
Zitto ashindanishwe na Shibuda, ndo viwango vyake na ndo mtu wa aina yake. Mwizi huyu kijana hafai kulinganishwa na wenywe busara na akili kama Dr. Slaa au Mnyika.
 
nawewe zuzu kweli, kutosusia kikao ni ni sawa na revenge! Hiyo red iko kwa kiingereza, hujaieewa STD VII
Hapo ktk red are you sure wat you talking? Dr Slaa na Zitto nani mwenye jazba nyingi? rejea mwaka 2010 wakati Zitto alivyokiuka maamuzi halali ya chama chake kususia hotoba ya raisi JK bungeni, yeye akuingia bungeni tena kana kwamba haitoshi kesho yake akafanya press conference hakaweka wazi kupingana kupingana na maamuzi ya chama chake.
 
Hatuhitaji mugabe wa tz. Slaa kikongwe kijizee
Hata Mnyika ni mkali zaidi ya Zitto, Zitto ni mbinafsi sana na hayupo na wenzake kabisa as teamwork, namkubali mnyika kuliko Zitto, dr SLaa Tunamwamini na Tunamhitaji kuwa raisi wa tanganyika
 
Umesahau, yale masharti ya mkataba wa kulipwa fedha nyingi kuliko wa mbunge for 5yrs sio ubinafsi, angeacha chama kimfikirie.
I support Zitto:
1. Zitto ni Chadema kweli, tangu akiwa 16 na hajawahi kuwa gamba, Slaa alikuwa gamba hadi alipotoswa kwenye uteuzi ndo akakimbilia Chadema
2. Nina wasi wasi Dk Slaa kwa umri wake anaweza kukutwa na yale ya rais wa Ghana
3. Dk Slaa ni muongo saana jamani. Tatizo la Chadema hatupendi kukosolewa. Kafulila alifukuzwa kwa sababu ya msimamo wake na kumkosoa Mbowe
4. Zitto ana maono. Ishu ya mitambo ya Dowans alishauri inunuliwe, watu, pamoja na Chadema, wakamponda sana wakasema amenunuliwa, cjui nn na nn, yaani upuuzi mwingi tu. Taifa likawa gizani wakati mitambo ipo, baadaye wabunge na wa Chadema wakiwemo wakabadilisha sheri na MITAMBO ILE ILE YA DOWANS ikanunuliwa, watanzania tukarudi mwangani. Chadema tusiogope vivuli vyetu. Najua Slaa tunampenda lakini hii haimfanyi Zitto awe mbaya
 
Usijidanganye slaa kufanya hayo, katiba itakuwa "diluted" rais yeyote ajae hatakuwa na madaraka mkubwa ya kuamua ancho taka. Jifunze toka kenya
Dr. atakuwa kiongozi mzuri ifikapo 2015, Isipokuwa apunguze jaziba:-
(1) Awahurumie wale wote walio wahi kukaa madarakani, hata wake walio mteka na kumtesa dr.
(2) Asiwapeleke the Hague, wale wote ambao kwa namna moja au nyingine walihusika katika machafuko ya zenj, miaka ile
(3) Asitaifishe majengo ya nyinyiemu, hasa makao makuu pamoja na viwanja vya mpira vya nyinyiemu kirumba, nk
(4) Asiwahukumu wale wote waliouza migodi na viwanda pamoja na majumba yote ya serikali
(5) ............................ nanyi endelezeni.
 
Umejuaje! nafurahia mjadala, hakuna mwana ccm atamsapoti mgombea yeyote kutoka cdm. Na huyo zito hata akigombea kwa tkt ya cdm, hatakuwa na
Magamba watakuwa wanafurahia sana hii mada Zitto is real a thorn in CDM flesh it must be removed somewhere somehow
 
Padri huwa hastaafu Slaa ni padri muasi ! Ameshindwa ya mungu ataweza ya Kaisari?
 
Dr slaa ni kiongozi mzuri,mwenye msimamo na mwenye kusimamia kile anachokifahamu,hana ubia na viongozi uchwara,ni mtu mwenye kuguswa na maisha ya mtanzania,moja ya wazalendo waliobakia ndani ya nchi hii,zitto siyo kwamba hawezi lakini bado analo jukumu la kuthibitisha uhalisia wa yale anayoyasema kwa watanzania ili kuondoa mashaka juu yake hivyo kwa miaka mitatu hii sidhani kama ataweza,dr slaa anaexperience sana na uchaguzi mkuu hususan nafasi ya rais hivyo anajua wapi pa kupeleka mashambulizi na anajua mapungufu ya uchaguzi uliopita,mwisho Dr slaa bado ni tumaini jipya kwa watanzania.
 
Tuache kelele nyingi, kama ungepewa mamlaka ya kumteua kati ya Zitto Zuberi Kabwe ama Wilbroad Peter Slaa kugombea nafasi ya urais mwaka 2015. Ni nani ungemteua? Na Kwa Nini? Toa sababu kuu nne TU.

Kijana Msomali kwanini hamjaweka technology rahisi ili na tusio na kompyuta tupige kura?. Maana ilinilazimu nisafiri hadi mjini CAFE nika-vote. Kwa simu inakataa.
 
subiri uone udini wa chadema watakavyomrukia ZITTO. wanajua zitto ni kichwa kupita hata huyo slaa lakini slaa wanampenda kwa kuwa ni PADRI.

huyu mtu mchonganishi,hajui chama,maana ya padre wala dini. Iam sorry kusema mropokaji chama cha udini tz kinajulikana mbona!
 
Dr. Slaa.

Ana msimamo thabithi, mjenga hoja, kiongozi bora na asiyependa ufisadi.

Hivi kulipwa mil 7 na ushee kwa kila mwezi huku makatibu wengine wakijitolea huo sio ufisadi!kusepa na mke wa mtu sio ufisadi hivi kusikiliza majungu sio ufisadi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom