zitto atapata kura nyingi akigombea urais kuliko slaa,Slaa ni mzee kwa sasa.
Mkuu, yawezekana unachokisema kina ukweli kwa sababu vijana ni wengi kuliko wazee.
Ila ninaamini kwa TZ ya sasa, vijana wengi wanauelewa wa siasa na wanauchungu na hali mbaya ya maisha waliyonayo kuliko awali.
Wakimchagua kiongozi ni kwa ajili maendeleo yao kuliko ushabiki wa kisiasa.
Enzi hizo mtumishi wa umma akiibia serikali alikuwa akisifiwa kwamba "mjanja yule, kawaacha".
Leo hii tofauti, ukiwa na pesa zinazotiliwa shaka na jamii, wanakudharau na kukuchukia kwamba ni fisadi, na hususan vijana ndio wanaoongoza katika kuchukia mafisadi.
Hivyo, wanataka kiongozi mkweli, mwaminifu, atakayewajali, atakayeinua uchumi wa wote na si wachache, asiyependa ufahari, anayeridhika na mwenye uchungu wa dhati na nchi hii. Hizi ni baadhi tu ya sifa chache za kiongozi ambaye vijana wengi wangependa wamchague.
Kwa haya machache utaweza kujua ni nani.