Kura ya maoni: Edward N. Lowassa v/s Bernard K. Membe

Kura ya maoni: Edward N. Lowassa v/s Bernard K. Membe

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CCM?

  • Bernard Membe

    Votes: 70 15.3%
  • Edward Lowassa

    Votes: 189 41.4%
  • None of them (Labda mwingine)

    Votes: 198 43.3%

  • Total voters
    457
  • Poll closed .
Laigwanan EL ni mchapa kazi na anaweza kutoa maamuzi magumu. Membe ni msafi lakini atakua Rais dhaifu kama ******.
 
membe anaonekana ni muoga na hajiamini na el ni mtuhumiwa wa ufisadi na muongo wa kuleta mvua
 
Bernard Membe anafaa sababu ni lesser of the devil, kama ulivyosema mwenyewe tunaweza chagua lesser of the two. Hope hio ni reason tosha kujustify uchaguzi wa yupi walau anafaa.
Usijidanganye neiwa jiulize kama lesser of devil vipi zile pesa alizopewa na marehemu Gadafi kwa ajili ya uchaguzi 2010 na akawasilisha sanduku moja tu? lile jingine kapeleka wapi? kama unataka kujua uliza wana ccm wengine
 
wote hawafai,coz wanatoka kweny system moja,so hakuna mwenye uwezo wa kuwawajibisha mafisadi zaidi ya kulindana!.......system hii haifai ht aje nani.Period!!
 
Ungeweka option ya tatu "Other/s", ingekuwa ni poll yenye objectivity na neutrality, vinginevyo ni kama umeshatuchagulia kwamba Rais kutokea CCM atakuwa ni aidha Membe au Lowassa;
 
Duuuuuh yani mtu ana lazimishwa kuchagua mchafu mmoja kati ya wachafu wawili!
 
Ongeza kitupe cha wote hawafai!
Wadau nawakilisha hili suala ili kupata kura za maoni za viongozi hawa ndani ya chama cha CCM.

Toa hoja na mawazo yako na upige kura pia kuona nani anafaa kati ya wawili. Zingatieni kuwa hatushindanishi na viongozi wengine ambao kila mmoja amekumbatia moyoni kuwa anafaa. Haijalishi wewe ni Chadema au CCM inachojalisha ni unaona yupi bora kati ya hawa wawili. Kuwa hata kama wote ni devils who is the lesser devil kati ya wawili?

Ni yupi unaona atafaa ama niseme nani angalau anatia matumaini kuwa walau anafaa kuteuliwa kuweza kuongea nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM kwa mwaka 2015?

Ni vema ukimataja utowe walau sababu zako ambazo unaona ni msingi wa maamuzi yako. Wadau hasira na pumba naomba ziachwe nje ya hii thread na tuweze kupata jibu thabiti.

Nawasilisha.
 
Bora lowasa kuliko joka la mdimu membe

Umesema kweli. Utendaji wa Lowasa unajulikana na ni jembe kweli kweli. Tatizo ni kuwa alichezewa ngoma ya kikwere ambayo hakuwa anaijua. Hii ndiyo inampaka matope hadi leo
 
Kimsingi uzi wako ni
swali ambalo kitaalamu liko katika muundo wa multiple choice. Maswali ya
aina hiyo huwa lazima swali liwe na jibu moja sahihi kati ya yote
yanayokuwa yameorodheshwa. Hakuna jibu sahihi hapo so naongeza mgombea
wa tatu aitwe non of the above. Huyu I hope atapata kura lukuki
akishindanishwa na hao matajiri bora kabisa barani Afrika.

Mkuu kuna option ya none of them pigia hapo.
 
None of them, (u would try none of the above) kaka kiingereza gani hiki tena? both are devils, once devil, devil, no lesser devil.
 
Edo N Lowasa

Kwasababu ni mtu mwenye uthubutu wa kujaribu.
Anashaurika
Msikivu
Mvumilivu
Mpiganaji
Amekomaa kisiasa/anaijua vizuri siasa

La mwisho linahusu ufisadi naomba tuelewane kitu kimoja, hata umweke mchungaji/padre/shekh wataiba tu! Angalieni Kenya na kashfa zao mfano anglo gold hizo epa na meremeta ni cha mtoto lakini angalieni Nairobi ilivyo sasa sisi tumezingua meli kuukuu wao wemeweka Nairobi Commuter Train na flying over zenye njia nne!

Tunataka kiongozi atakae weza kusogeza mbele nchi na kuwaneemesha wananchi!
 
ongeza electives
(option), mfano: wote hawa fai, EL/Membe, only kama itabaki hivi, Kama
wote hawafai nani kati ya hawa? a) Mwakyembe. b) Magufuri, c) Makamba jr
d) Sitta. mbona umejibana sana kuto tadhimini elekevu???

Tayari Mkuu kuna option ya none of them pigia hapo.
 
Wadau nawakilisha hili suala ili kupata kura za maoni za viongozi hawa ndani ya chama cha CCM.

Toa hoja na mawazo yako na upige kura pia kuona nani anafaa kati ya wawili. Zingatieni kuwa hatushindanishi na viongozi wengine ambao kila mmoja amekumbatia moyoni kuwa anafaa. Haijalishi wewe ni Chadema au CCM inachojalisha ni unaona yupi bora kati ya hawa wawili. Kuwa hata kama wote ni devils who is the lesser devil kati ya wawili?

Ni yupi unaona atafaa ama niseme nani angalau anatia matumaini kuwa walau anafaa kuteuliwa kuweza kuongea nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM kwa mwaka 2015?

Ni vema ukimataja utowe walau sababu zako ambazo unaona ni msingi wa maamuzi yako. Wadau hasira na pumba naomba ziachwe nje ya hii thread na tuweze kupata jibu thabiti.

Nawasilisha.
Kumchagua Membe ni kuendeleza utawala wa Kikwete kwa kipindi kingine....ni mwendawazimu tu ndu anafurahi kutawaliwa na Kikwete.....je kibaraka wake itakuwaje??
 
TEAM EL: Reasons

1. EL ni Mchapakazi: Utendaji wake unaotofautiana na wengine ulionekana vizuri alipokuwa wizara ya maji, alipokuwa wairi mkuu mambo mengi yalishughulikiwa kwenye muda mfupi, ikumbukwe alipoteuliwa kuwa PM alifanya vizuri sana kushughulikia tatizo la njaa lilokuwepo that time

2. EL ni mvumilivu:Amevumilia wakati J K Nyerere alipowakatalia yeye na J Kikwete kugombea urais, alimwachia JKikwete nafasi iliyokuwa wazi kwake kugombea urais kwa uvumilivu kwamba angekuwa next, amevumilia pale watu walipomwita fisadi wa kashfa ya Richmond kwa kumbeba Rais ambaye kiukweli ndie muhusika na amewahi kumwabia JK hadharani

3. EL ni makini: Alivunja mkataba wa ilokuwa city water na serikali iashinda kesi hiyo katika mahakama ya kimataifa ya usuluhishi, Alimshauri pia rais JK kuvunja mkataba na Richmond JK akakataa

4. Hakati tamaa hata pale tuhuma anazopelekewa zinapokuwa nyingi sana. Mara nyingi husema nina mipango ila 'Nitavuka daraja nikilifikia'

5. Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa fadhila. Mara nyingi huwa hajibu/hashindani na wale wanaotaka ashindane nao.

6. Hasahau kiapo. 'Mimi na Kikwete hatujakutana barabarani'. Hivyo hata kiapo cha kuilinda na kutetea katiba anakiweza

7. Ni Jasiri: Hushughulikia mambo kutokana na udharura wake; hasubiri

8.Just few to mention
 
Back
Top Bottom