Kura ya maoni: Edward N. Lowassa v/s Bernard K. Membe

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CCM?

  • Bernard Membe

    Votes: 70 15.3%
  • Edward Lowassa

    Votes: 189 41.4%
  • None of them (Labda mwingine)

    Votes: 198 43.3%

  • Total voters
    457
  • Poll closed .
tatizo wakiingia madarakani hawa wataannza kushughulikia wabaya wao pamoja na kulipa fadhila, mara miaka 5 imeisha...
 
Haituhusu hii wana chadema,magamba mtajiju na mashetani yenu awe mdogo au mkubwa hayo ni yenu......nyambaff mnasifia mapepo?
 
Kimsingi uzi wako ni swali ambalo kitaalamu liko katika muundo wa multiple choice. Maswali ya aina hiyo huwa lazima swali liwe na jibu moja sahihi kati ya yote yanayokuwa yameorodheshwa. Hakuna jibu sahihi hapo so naongeza mgombea wa tatu aitwe non of the above. Huyu I hope atapata kura lukuki akishindanishwa na hao matajiri bora kabisa barani Afrika.
 
hii poll ni magumashi ukitaka kuvote inakataa mweka thread anazingua ili aweke kura za itifaki aka maruhani kwa mtu wake! Joka la Mdimu. Mnatisha hata hii meaningless vote mnaiba
 
Joka la mdimu hafai kwanza ukaribu wake na Riz1 na mama salama na baba mwanaasha inamaanisha anakubaliana na kila kitu wanachofanya hawa wanaukoo
 
Na unge wapambanisha hao na chizi au kichaa yeyote wamirembe mi ninge mpigia kichaa wa mirembe sio hao!
 
Mi nahisi lowassa atapeta ccm, umeona kura alizopata membe kwenye nec?
Mwaka 2002 kwenye uchaguzi kama huo JK alikuwa mtu wa 18 kati ya nafasi 20 zilizokuwepo na mwaka 2005 alishinda uchaguzi mkuu kwa kishindo na kuteuliwa na chama chake na baadaye na wananchi wote kwa zaidi ya 80%. anatakiwa a-maintain uadilifu wake, ajenge mtandao wa watu wa kumsaidia kila kona na ajisogeze karibu zaidi na watu. Lowassa kwa sasa hana nafasi tena, kwanza anaumwa hata kutembea tabu, kutoa mkono shida
 
mwanzoni nilisema haya ni maajabu, Membe kuongoza kura ya maoni mpaka sasa! Nimeamini watu wengi wanauchukia ufisadi, hii pia ilijidhihirisha kule Dodoma pale wajumbe walipokuwa wakigombania kupiga picha na Membe
 
mi nimechagua membe kwa sababu ana elimu bora ya mambo ya diplomasia na pia ni mtu mwenye uzoefu wa kutosha kwenye siasa za mambo ya nje - ukizingatia tanzania ya leo hii inazungumzia sana mambo ya economic diplomacy

pili, alinifurahisha sana alipoamua kujitokeza hadharani na kumuunga mkono Spika Sitta alionesha anajali vipaji vya watu wanaosimamia ukweli na pia alipojitokeza kuwataja akina Chenge na mafisadi wengine

tatu, ameonesha jitihada za dhati katika kurudisha mabilioni ya rada na huwa anaibuka kujibu tuhuma kila mara anapotajwa - hii inaonyesha kwamba huyu jamaa ni muadilifu na ni rais anayefaa

nne, hafanyi siasa za makundi huyu maana hana kundi hata moja
 
Lowassa anafaa amekuwa mvumilivu ktk misukosuko mingi na mtu wa vitendo na sio maneno.
 
ongeza electives (option), mfano: wote hawa fai, EL/Membe, only kama itabaki hivi, Kama wote hawafai nani kati ya hawa? a) Mwakyembe. b) Magufuri, c) Makamba jr d) Sitta. mbona umejibana sana kuto tadhimini elekevu???
 
Back
Top Bottom